ITV na Wosia wa Baba wa Taifa

Nimeona na nimeogopa sana ! Aliyosema nyerere wakati ule yanatokea leo ! Hakika Nyerere bado anaishi , Sijui kama ITV haitafungiwa kesho .
Kwani ITV ndio wamesema? Si ni wosia wa baba yetu wa taifa tunayempenda na kumheshimu sana? Si tunajitahidi kumuenzi kwa yale mema aliyotenda na kutuasa? Hili ni mojawapo, na ni la msingi hasa. Hongereni ITV kutuletea wosia huu wa baba.
 
Kwahiyo unajaribu kusemaje?
Heshima kwa JKN kwangu mimi ni visionary wa kiwango cha kimataifa. Lakini kwa kila mtu anayeishi duniani, kuna upande mzuri na mbaya. Huyo mtu niliyemjibu ameandika maneno fulani, mimi nimechangia mawazo yangu.
 
Kwenye toleo hili nukuu hiyo inapatikana ukurasa wa 71. Mwenye nafasi ajisomee
 
Heshima kwa JKN kwangu mimi ni visionary wa kiwango cha kimataifa. Lakini kwa kila mtu anayeishi duniani, kuna upande mzuri na mbaya. Huyo mtu niliyemjibu ameandika maneno fulani, mimi nimechangia mawazo yangu.
Si ndio uyaseme hayo mawazo yako kwa kumbukumbu zaidi!Wengine sisi huwa tunafukunyua nini mtu amesema leo na kesho baada ya heading kubadilika ila content ileile unakuta kabadilika kabisaa!
"Ulichojaribu kukiri ni kuwa hata Nyerere alikuwa Dikteta kama Magufuli so si mtu sahihi kutumia qoute zake kukemea udikteta",
Basi sawa
 
.
Siku hizi Lowasa ni share holder ITV. Sishangai
Unawazimu siyobure! Lowasa ndiye aliyemwambia mwl atoe hotuba ile iliyorushwa ITV! Lowasa ndo msambazaji wa hotuba za mwl ambazo zilizuiliwa kuoneshwa hadharani sasa kwasababu anamahusiano na ITV amehonga ili hotuba ile ioneshwe!!! Hivi ni kweli uwezo wako wa kufikiri ni huu tu!!! ipo shida utakuwa ulizaliwa kipindi cha njaa!!!!!
 
.
Acha jazba.
Pointi yangu ni rahisi: Mmiliki wa chombo cha habari anao uamuzi kuhusu nini kirushwe, lini na kwa nini.
Hata hili hulioni?
 
Hakuna kiongozi mwasisi wa bara hili ambaye katika uongozi wake hakuwahi kuonyesha chembe chembe za udikteta. Unapoongoza mamilioni ya watu ambao robo tatu yake hawana elimu kubwa kama uhalisi wa uongozi wa JKN ulivyokuwa, siku zote ni lazima uwe na aina fulani ya ubabe. Ni lazima CIF aheshimiwe, amiri jeshi mkuu asiyeheshimika, asiyeweza kusema NO na kila mtu akaheshimu kauli, huyo ni CIF wa kwenye sinema na sio kwenye maisha yenyewe. JKN alikuwa akishuka pale airport anamuuliza mkuu wa mkoa wa Dar mzee songambele (sidhani kama yu hai), kwamba "lipo"?, hapo akimaanisha sembe ipo kwa watu wa Dar?. JKN alimfikiria mtu wa chini kabisa, JPM anamfikiria mtu wa chini kabisa. Na kama unakuwa tayari kuwa dikteta kwa faida ya watu wa chini kutonyanyasika kimaisha, basi nina uhakika hata huko mbinguni wale malaika na manabii wanaokubali udikteta wa aina hiyo.
 
.
Acha jazba.
Pointi yangu ni rahisi: Mmiliki wa chombo cha habari anao uamuzi kuhusu nini kirushwe, lini na kwa nini.
Hata hili hulioni?
Unamanisha kwamba hotuba ile ikosawa lakini iltakiwa irushwe mwezi wa 12 lakini Lowasa amehamasisha ikarushwa wa 8. Fikiri vizuri! kila funzo lolote hutolewa kutokana na mapungufu yaliyoko katika jamii! kwa hiyo ITV kulirusha wakati huu ni halali kabisa! Wewe Lowasa kahusikaje katika hilo au ndo mana walipigwa faini majuzi!! bado hujanishawihsi!
 
hapa na pale wamentaja Nyerere katika nafasi ya 5 katika "Top Ten Greatest African Leaders of All Time". upende usipende Nyerere NI, (siyo ALIKUWA) great leader.
 
Kipindi cha Nyerere nchi ilikuwa imetoka chini ya utawala wa Mkoloni!Hiyo demokrasia bado tafsiri yake sahihi ilikuwa inaendelea kutolewa!Kipindi hicho kilikuwa kipindi cha mpito na ilibidi twende hivyo!Baada ya hapo ikawekwa misingi ya demokrasia,Nyerere aliihubiri sana!Akaona kwa katiba iliyokuwepo mamlaka ya Rais ni makubwa sana na kama akitokea asiye mweledi anaweza fanya mambo ya ajabu!
Leo hii tunaye kiongozi ambaye ni zao la demokrasia lakini anataka kutawala kidikteta!Kiongozi ambaye aliapa kwa imani yake mbele ya kadamnasi kuwa atailinda na kuiheshimu katiba!Leo hii anavunja katiba inayotambua demokrasia halafu unasema Malaika mbinguni wanamfurahia!Hofu ya Mungu iko wapi wakati unavunja kiapo ulichoapa huku ukiinua na mkono juu?
Hapana,kiongozi yeyote anayevunja katiba si wakumtetea!kuna namna bora ya kuwasaidia wanyonge kuliko kutumia mabavu!Mabavu ambayo pengine unaweza ukawa unamdulumu mtu haki yake kwa kisingizio eti wanyonge!
 
Ndugu yangu hakuna nchi inayofanya siasa za kienyeji kama Tanzania. Kila nchi inakuwa na mtu mwenye sauti ya mwisho, sauti yenye kuhitajika kuheshimiwa na kila mtu. Ni lazima tuondokane na "anarchy", ni lazima tuondokane na uhuru uliopitiliza ambao unashindwa kufanana na wajibu. Hakuna nchi duniani ambayo rais anatoa maagizo halafu anatokea mwanasiasa mwingine eti na yeye anatoa maagizo, hakuna kitu kama hicho. JK alivumilia mengi kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye uwezo wa kupuuzia, matokeo yake wanasiasa wa upinzani wakafikiri kwa anarchy ni haki yao. Hakuna suala la udikteta, kila mtu anakumbushwa umuhimu wa kufanya kazi ya halali ili mkono uende kinywani.
Ndio maana DJ akaambiwa kama anataka kufanya siasa aende jimboni kwake, asilete siasa za anarchy kwa kisingizio cha demokrasia.
Hao wanaotufundisha maana ya demokrasia wanaheshimu ule uwepo wa mifumo ya uongozi ambapo mwenye mamlaka anaheshimiwa. Sisi ambao bado tunaendelea kujifunza demokrasia eti tunataka kutengeneza aina yetu ya mfumo wa maisha wa kisiasa ambao haupo sehemu nyingine ile duniani!!.
 
Kwamba Rais akiamua kuanzia leo marufuku ofisi za vyama kufunguliwa basi ndio iwe kauli ya mwisho na utekelezaji ufanyike!Kwako wewe lolote akiamua Rais basi ni utekelezaji tu!Ndio maana taifa linaenda kimwendokasi!Rais alisema gawa sukari yote itakayokatwa,TRA wakamwambia hapana,sukari iko kihalali na imelipiwa kodi!Ukifanya hayo utalazimika kuwalipa fidia,yako wapi,sukari ilikagawiwa?Ndio ujifunze kuwa sio kila tamko la Rais linatekelezeka!Ndio maana anatakiwa ashauriwe ili kuepuka kuingiza nchi kwenye hasara!Wewe unasema Mbowe akafanye mkutano Hai,katiba ibara ya 18 na 21 inampa haki ya kukusanyika kokote ndani ya mipaka ya nchi!
Comment zako za awali walau zilikuwa na ujumbe unaopimika,kwa mchango huu umepiga porojo tu!
 
Kaka inafika wakati maishani lazima ukubaliane na mabadiliko, iwe unayapenda au huyapendi. Ibara za katiba kumpa uhuru ni suala moja na yeye kupoteza muda wa watu wa kufanya kazi kwa sababu ya kumsikiliza yeye jukwaani ni suala jingine. Unapozama kwenye masuala ya kisiasa, usisahau umuhimu wa kuwahamasisha kufanya kazi wananchi hao hao wanaokupigia kura. Hayo masuala ya sukari ni vita kubwa kuliko unavyoyasikia wewe kwenye vyombo vya habari, ndio maana waziri mkuu kwa kushirikiana na wazalishaji kama mtibwa wanapanga kuongeza uzalishaji.
Mwambie DJ na wengine washughulike na umasikini wa waliowapigia kura na sio kupenda popularity kupita kiasi. Inafikia wakati Tundu Lissu anasema wazi bungeni "nasikia umeme umekatwa huko nje", yeye anatatua shida za wananchi au anapenda kutazamwa kupitia kwenye runinga?. JK aliwapa uhuru mkubwa mkashindwa kuwa na heshima.
Mnapodai haki za kidemokrasia, mkumbuke na kutimiza wajibu, pia mkumbuke kuwa yale yaliyowapa ubunge mwaka jana wakati wa uchaguzi, huu ndio muda wa kuyatimiza.
Waonye wabunge wa upinzani, hizi kura walizopata mwaka jana ikifika 2020 wanaweza kupata nusu yake kama watajisahau na kubakia kuwa wanaharakati badala ya kufanya kama EL alivyowashauri, juu ya kubadilisha tamaduni za kisiasa.
 
Huoni Rais anavyozunguka nchi nzima akipoteza muda wa watu kufanya kazi kwenda kumsikiliza!Shule huwa zinafungwa kumpisha Ngosha!Hayo anayoyasema Jukwaani full comedy.,anawaambia watu wafyatue tu watoto!Shame
Kama walifanya siasa 2010-2015 wakati wa JK,nilitegemea wapungue!Wananchi wamewaelewa zaidi na wakaongezeka zaidi!Magufuli alikurupuka suala la sukari na maumivu tunayo mpaka leo!Asikilize washauri wake!
Katiba ndio kila kitu,hata Rais yuko hapo kwa mujibu wa katiba!Hata majeshi yanamheshimu sababu ya katiba!Anavyoanz kuminya haki za RAIA kikatiba anajipalia kaa!Siku zote watu wa hivi hawaridhiki!Hata Nkurunzinza alianza hivi!
 
Hakuna haki ya raia iliyominywa zaidi ya watu kuhimizwa kufanya kazi. Mind you yeye ni mbunge wa Tanzania nzima, tofauti na kina DJ na wengine wote, anayo haki ya kwenda popote na kufanya lolote. Anayo haki ya kuingia msikitini na akahutubia, anayo haki ya kusali katika makanisa ya madhehebu yoyote yule na hakuna atakayemfanya lolote. JK alijishusha sana kiasi ambacho taasisi ta urais ikaonekana ni ya kawaida yenye kustahili kuvunjiwa heshima. Hakuna anayeminywa, ni kukumbushana maana ya heshima na nidhamu kwenye nchi. Huwezi ukaishi maisha yasiyokuwa na nidhamu, maisha yaliyozoea short cut halafu ukatengeneza taifa lenye kustahili kuheshimiwa. Lazima tufike mahali tuzoee maisha mapya. Yale maisha ya mwaka mzima watu wamesimama wanamsikiliza mwanasiasa fulani, ambaye hana heshima wala utii kwa mamlaka, hayawezi kuendelea kuwepo. Kisaikolojia tuendelee kukabiliana na mabadiliko ya kweli, na sio yake ya kuzungusha mikono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…