ITV na Wosia wa Baba wa Taifa

ITV na Wosia wa Baba wa Taifa

WALIKUWA WAMEMLENGA DIKTETA UCHWARA JOHN POMBE MAGUFULI ( mzee wa kufyatua watoto/ baba jesca/ mikurupoko/ katilii/ mkojorea katiba)
Duh!! Mkuu kilaza mjanja maneno yako makali sana. Angalia usije ukawa-mhanga wa kale kasheria ketu kaleee!! Labda kama haupo ndani ya mipaka yetu.
 
Hizi si dalili nzuri kwa ustawi wa Taifa na Watu wake...Kuna sehemu tumejikwaa kama Taifa. Kweli Utumwa Unarejea taratibu . Japo kuwa minyororo haionekani hadharani lakini tayari Taifa linafungwa minyororo na waliopewa dhamana ....
 
Kila kitu kwa kiasi, hata uhuru unatakiwa kuwa Na kiasi.
Nchini ufaransa, uhuru ulizidi kiasi,Charlie Hebdo wakachora katuni za kumkashifu mtume Muhammad, kilichofuatia sote tunakijua, mauaji ya kutisha!
Mwalimu alipinga udikteta, lakini hata yeye alitambua kuwa uhuru unapaswa kuwa Na kiasi Na kuna wakati inahitajika kiongozi "kukaza kamba" kidogo ili Nchi iende.
Kama Nyerere angelegeza Na kuruhusu uhuru kupita kiasi, ishu ya Kambona ingeishia wapi?
Kipindi cha utawala wake wanafunzi wa UDSM waliandamana, alikaa kimya akaruhusu?
Je, walichokua wakidai hakikua haki?
Ifike mahali, siasa zisizo Na msingi tuweke pembeni Na tuangalie mambo kwa Upana wake,
Gaddafi aliitwa dikteta Libya, akauawa, Leo Libya ina hali gani baada ya kumuondoa "dikteta" Gaddafi?
Marekani ambako historia inatuambia ndiko demokrasia imezaliwa, ndio huko watu wanamiliki bunduki hovyo Na kila kukicha kuna matukio ya watu wasio Na hatia, wakiwemo watoto mashuleni kuuawa kwa kupigwa risasi,
Kwa nini matukio Kama Haya hayatokei Korea kaskazini au Urusi, nchi zinazotuhumiwa watawala wake kutawala kibabe?
Tuangalie mambo kwa upana wake,
Kila kitu kifanyike kwa kiasi, Ni asili yetu binadamu kutokuridhika!
Hata ikitokea tukapewa hiyo absolute freedom, kutatokea sababu nyingine ya kupinga mambo Na kulumbana Na mamlaka.
Ni kweli, kila kitu kwa kiasi. Katiba nzuri kuliko iliyopo na inayopendekezwa ingesaidia sana kunyoosha mambo. Kwa sasa tuendelee kufanya kazi!
 
Msimtumie mwalimu ili mpate kiki ya jukwaa,wakati wa mwalimu kulikuwa na maandamano kwa mfano sherehe za mei mosi,mwalimu alikuwa anahamasisha wananchi waunge mkono maazimio kwa mfano la arusha.MIMI USHAURI WANGU NI HUU TULIUNGE AZIMIO LA KUHAMIA DODOMA TWENDENI DODOMA KILA CHAMA KITOE ANGALAO WATU MIA TUTEMBEE KWA MIGUU MPAKA DODOMA. ACHENI UJINGA WA SIJUI UKUTA, SIJUI HAKUNA KULALA.
 
Leo ITV wamekuja na Wosia wa Baba wa Taifa kuhusu udikteta ambapo wameonyesha sehemu ya Hotuba ya Mwalimu Nyerere akikemea udikteta hasa wa viongozi wa kiafrika na tabia ya madikteta hao kuminya uhuru wa habari.
1471332323737.jpg
 
WALIKUWA WAMEMLENGA DIKTETA UCHWARA JOHN POMBE MAGUFULI ( mzee wa kufyatua watoto/ baba jesca/ mikurupoko/ katilii/ mkojorea katiba)
Utafungwa ndugu yangu, Omba tu Rais awe amepata ule uvumilivu wa JK aliyokuwa akiuomba.
 
WALIKUWA WAMEMLENGA DIKTETA UCHWARA JOHN POMBE MAGUFULI ( mzee wa kufyatua watoto/ baba jesca/ mikurupoko/ katilii/ mkojorea katiba)
Mbona lugha yako siyo ya kistaarabu?umetumbuliwa sasa uko nje ya nchi.
 
Msimtumie mwalimu ili mpate kiki ya jukwaa,wakati wa mwalimu kulikuwa na maandamano kwa mfano sherehe za mei mosi,mwalimu alikuwa anahamasisha wananchi waunge mkono maazimio kwa mfano la arusha.MIMI USHAURI WANGU NI HUU TULIUNGE AZIMIO LA KUHAMIA DODOMA TWENDENI DODOMA KILA CHAMA KITOE ANGALAO WATU MIA TUTEMBEE KWA MIGUU MPAKA DODOMA. ACHENI UJINGA WA SIJUI UKUTA, SIJUI HAKUNA KULALA.
Maandamano na matembezi ni vitu viwili tofauti, rudi shule.
 
Hivi aliyemuweka jela ya nyumbani marehemu Jumbe ni nani? Kutaka serikali 3 ni kosa? Na udikteta ni nini?

Sawa, lakini Mwalimu aliona mapungufu yake alipokuwa madarakani na akaamua kutoa wosia wa kusaidia vizazi vya sasa na vijavyo. Angalia madudu yooote yaliyofanywa baada ya mwalimu kuaga dunia, ni rais gani mstaafu amainua mkono wake na kukemea? RIP Mwalimu
 
His excellency president for life field Marshal Alhaj Dr. Idd Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of all the beasts of the Earth and Fishes of the seas Conqueror of the British Empire in Africa in general and Uganda in particular. Hizi ni baadhi tu Mkuu ila yule mtukufu alikuwa na title/a.k.a za kila namna.
Ahahahahha conquer of "British Empire", sijui waingereza walikua wanajisikiaje?
Msumari wa moto ni "the lord of all the beast of earth"
 
Back
Top Bottom