ITV na Wosia wa Baba wa Taifa

ITV na Wosia wa Baba wa Taifa

"KUKUBALI KUFANYWA VIKARAGOSI VYA VIONGOZI NI DALILI YA WOGA, SI DALILI YA HESHIMA; NA WOGA NA HESHIMA NI VITU VIWILI MBALI MBALI.
MAADILI MEMA YANATUTAKA TUWAHESHIMU VIONGOZI WETU, MA DHATI WANATIMIZA WAJIBU WAO.
MAADILI MEMA HAYATUDAI TUWAOGOPE VIONGOZI WETU. NA VIONGOZI MAKINI HUPENDA KUPATA HESHIMA YA WANANCHI WENZAO, LAKINI HAWAPENDI KUOGOPA.
KUOGOPWA NI SIFA NA ADA YA MADIKTETA, VIONGOZI HALISI HAWAPENDI KUSHIRIKI.
KUJENGA MAZOEA YA KATIE VIONGOZI HATA KATIKA MAMBO HARAMU NI DALILI YA WOGA, NI KUKARIBISHA UDIKITETA". Pg. 65
Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania.
Mwl. J. K Nyerere
ZIDUMU FIKRA SAHIHI
 
Mwalimu alikuwa mwanadamu na alipinga sana tabia ya wa kujitukuza au kutukuza mwanadamu mwingi. Mwalimu aliamini katika usawa wa haki kwa kila mtu.

Inawezekana tukaangalia aliyoyafanya wakati wake na katika muktadha wa wakati ule tukamwuona kuwa alikuwa mbaya sana kwa viwango vya sasa. Hata hivyo mengi ya yale aliyosema kama wosia wake kwa watu wa taifa aliloasisi yanaashiria kuwa anakiri kuwa kuna nyakati aliwahi kukosea katika maamuzi na inawezekana aliwaumiza watu.

Wapendwa, Mwalimu, hata hivyo alifanya na kusema mengi ya kutufundisha na kutuadibisha kama watanzania. Alitutaka tuishi kwa umoja na upendo; hakuwagawa watu katika makundi ya kikabila, kiitikadi au kiimani.

Baada ya Mwalimu hajatokea mwingine wa kufanana naye kwa namna yeyote kimaadili. Na kama tutaendelea kupalilia nidhamu ya woga kwa kuwafanya watu wasiwe huru kufunguka tutakuwa tunastawisha hasira ndani ya watanzania na iko siku italipuka.

Mwalimu aenziwe kwa kwa kuhakikisha upendo wa kidugu unadumishwa na huo hauwezi kudumishwa matamko ya vitisho na kejeli kwa demokrasia, bali kwa mifumo imara ya kikatiba itakayohakikisha UHURU na UMOJA wakweli.

Zidumu fikra za MWALIMU!
MUNGU Ibariki Tanzania!

Kila kitu kwa kiasi, hata uhuru unatakiwa kuwa Na kiasi.
Nchini ufaransa, uhuru ulizidi kiasi,Charlie Hebdo wakachora katuni za kumkashifu mtume Muhammad, kilichofuatia sote tunakijua, mauaji ya kutisha!
Mwalimu alipinga udikteta, lakini hata yeye alitambua kuwa uhuru unapaswa kuwa Na kiasi Na kuna wakati inahitajika kiongozi "kukaza kamba" kidogo ili Nchi iende.
Kama Nyerere angelegeza Na kuruhusu uhuru kupita kiasi, ishu ya Kambona ingeishia wapi?
Kipindi cha utawala wake wanafunzi wa UDSM waliandamana, alikaa kimya akaruhusu?
Je, walichokua wakidai hakikua haki?
Ifike mahali, siasa zisizo Na msingi tuweke pembeni Na tuangalie mambo kwa Upana wake,
Gaddafi aliitwa dikteta Libya, akauawa, Leo Libya ina hali gani baada ya kumuondoa "dikteta" Gaddafi?
Marekani ambako historia inatuambia ndiko demokrasia imezaliwa, ndio huko watu wanamiliki bunduki hovyo Na kila kukicha kuna matukio ya watu wasio Na hatia, wakiwemo watoto mashuleni kuuawa kwa kupigwa risasi,
Kwa nini matukio Kama Haya hayatokei Korea kaskazini au Urusi, nchi zinazotuhumiwa watawala wake kutawala kibabe?
Tuangalie mambo kwa upana wake,
Kila kitu kifanyike kwa kiasi, Ni asili yetu binadamu kutokuridhika!
Hata ikitokea tukapewa hiyo absolute freedom, kutatokea sababu nyingine ya kupinga mambo Na kulumbana Na mamlaka.
 
Baada ya kichapo cha fine ya million Tano za yule Mchungaji na na kiti cha Naibu mini subwoofer..... Pampa oyeee
 
Hivi aliyemuweka jela ya nyumbani marehemu Jumbe ni nani? Kutaka serikali 3 ni kosa? Na udikteta ni nini?
Harafu mbona aliacha katiba ya mwaka 77 wakati aliruhusu vyama vingi 92..... aliacha NEC inayo chaguliwa na captain wa timu pinzani, katiba ya chama kimoja bila kufanya mabadiliko makubwa.... kwa haya huwa simwelewi baba wa Taifa... japo mengi nampa big up, JKN alikuwa anaona mbali sana....
 
Kuna 1 waliweka ya ukabila,.ati hatumpi kwa sababu ni mkara? Yani kiukweli ndo tunayaona haya, mbaya zaidi hii ya jana anasema hasa viongozi wa africa
 
Bado mnamuamini Mwl Nyerere na demokrasia?
Ambaye yy mwenyewe demokrasia yake ilikuwa ya mdomoni tu
Mwl hakuweka demokrasia kwenye practical
Alicho mfanya Mzee Jumbe ni unyama mbaya sana
Anayemsikiliza hadi leo Mwl Nyerere na porojo zake anapoteza tu muda wake
Ukimpinga Nyerere kwa hoja uliishia jela akikuhurumia sana kizuizi cha nyumbani ufe taratibu
Kama kuna JEHANAM nitashangaa sana nisipomkuta Mwl Nyerere huko
Nyerere na hotuba zake zipuuzwe
 
Back
Top Bottom