ITV mualikeni Gidabudai kwa pongezi

ITV mualikeni Gidabudai kwa pongezi

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
2,026
Reaction score
3,113
Miaka kadhaa iliyopita ITV walikuwa wakifanya coverage ya karibu sana na bwana Gidabudai. Moja kati ya vitu mabavyo navikumbuka ni kauli yake ya kusema "kama Tanzania itapata medali yoyote kwenye mchezo wowote basi nitachoma vyeti yangu vyote hadharani"

Alikuwa alisema hivyo kwa kuangalia namna kamati ya olimpiki ya kipindi hicho ilivyokuwa inaboronga chini ya mzee Bayi.

Leo Gidabudai ameuchukua usukani na kwa Mara ya kwanza tangu kuumbwa dunia, Tanzania tumechukua medali ya shaba kupitia mwanariadha Aliphonce Simbu.

Gidabudai anastaili pongezi, na kwa sababu aliweka mipango yake hadharani kupitia ITV, ni vyema wakamuita kumpongeza.

Hongera Gidabudai, hongera Simbu.
 
Sijaelewa..alitumia satire au nn? Kuchoma vyeti vs kupongezwa
 
Siku hizi naye ni kiongozi wa riadha ndo maana tumebeba

ITV wamtafute kumpongeza na sio kumchomea vyeti

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Gidabudai alionyesha nianya kurudisha hadhi ya riadha hapa nchini,alikua analalamika jinsi viongozi waliopita jinsi walivyokua wanahujumu chama cha riadha.
Sasa tumeanza kuona matunda ya timu yake.
 
Back
Top Bottom