`Itungwe sheria ya kudhibiti unyanyapaa` | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

`Itungwe sheria ya kudhibiti unyanyapaa`

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Serikali imeshauriwa kutunga sheria maalum ya kushughulikia matatizo yanayotokana na unyanyapaa, ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanaoishi na VVU.
  Aidha, imeombwa kuweka misingi bora itakayowezesha kuanzishwa kwa mahakama za kifamilia ili kuwezesha matukio mengi yanayohusu familia kujadiliwa badala ya kila tukio kupelekwa katika mahakama za kawaida.
  Changamoto hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na wakili Keregero Keregero wakati akitoa mada katika mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari juu ya kuandika habari zinazohusu unyanyapaa na ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wanaoishi na VVU.
  Keregero ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, alisema endapo hatua ya kuanzishwa kwa mahakama za kifamilia itafikiwa, bila shaka matatizo mengi yanayotokana na unyanyapaa yana ukatili vitapungua.
  "Hivi sasa kuna matoleo zaidi ya kumi ya sheria mbalimbali, ikiwemo ya ndoa ya mwaka 1971, ya watoto, ya ardhi ya mwaka 1999 na ile mpya kabisa ya Ukimwi ya mwaka 2008 ambazo zote zimeshindwa kukabiliana vilivyo na ongezeko la vitendo vya unyanyapaa na ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wanaoishi na VVU," alisema.
  Alisema karibu katika kila kabila nchini matatizo ya kuongezeka kwa vitendo vya unyanyapaa na ukatili vimekuwa vikiripotiwa, lakini kutokana na wingi wake imekuwa vigumu kutatuliwa katika mahakama za kawaida.
  Hata hivyo, wakili Keregero alisema wakati mwingine inakuwa vigumu kwa mahakama kupata majibu ya moja kwa moja kutokana na wanawake wengi kutokuwa tayari kutoa ushahidi pale wanapohitajika kutoa maelezo ya uhakika.
  "Hali hiyo inachangiwa na baadhi ya makabila kudhani kupigwa au kukandamizwa na waume zao ni sehemu ya kuboresha mapenzi yao jambo ambalo ni kinyume na linasumbua wakati wa kutafuta haki," alisema.
  Mafunzo hayo yameratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Ukimwi Tanzania (Ajaat) na kudhaminiwa na Watu wa Marekani (USAID) kupitia Futures Group International chini ya mradi wa Health Policy Initiative (HPI).
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wenye VV/UKIMWI ni kosa chini ya Sheria ya HIV/AIDS Prevention and Control Act 2008.Kanuni za kutekeleza sheria hii ziko kwenye hatua za mwisho ..hivyo mtaanza kuona kesi zikipelekwa kunakohusika soon.
  Aidha matatizo mengine ya ukatili na ubakaji yaweza kushughulikiwa chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana ( SOSPA 1998) au Penal Code ....
  Kifupi sheria zipo. Kama hazitekelezwi, haileti maana kuendelea kutunga sheria mpya ilhali zilizopo tena nyingine mpya kabisa bado hazijaweza kutumiwa.Kinachotakiwa ni kuendelea kuelimisha madhara ya unyanyapaa ili jamii ielewe kwa mfano kunyanyapaa kunafanya watu wajifiche, wasitafute huduma kwa mfano za ARVs na VCT... pia kunachangia kuongeza maambukizi kwa sababu watu walio na VVU/UKIMWI wataendelea kutokuchukua tahadhari na kuendelea kuambukiza wengine ikiwemo watoto wasiozaliwa bado ( mimba) na wale waliozaliwa kwa vile watanyonyeshwa maziwa ya mama mwenye UKIMWI/VVU.

  Anaposema Sheria za watoto zina matatizo..amefanya utafiti wa kutosha kujua ukweli? Mbona kuna sheria mpya ya Law of the Child Act 2009.... na hii ni moja ya progress laws so far katika nchi hii na ni mfano katika jurisdictions mbalimbali .
  For the first time, children in Tanzania now have legal protection of their rights unlike before where it was difficult to navigate through different pieces of legislation to identify provisions catering for the welfare and interests of children... now its all under one law.
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hiyo Sheria ya UKIMWI ni miongoni mwa sheria ambazo binafsi nina shaka nayo kabisa kama inafaa kuthibiti kwa hakika matatizo yahusuyo maambuziki ya Ukimwi, Unyanyapaa, kuwalinda waathirika na kuwasidia wale wanaohusika kwa namna moja au nyingine kuwahudumia watu wanaoishi na VVU.

  Wasiwasi nilionao mbali na ule wa ndani ya vifungu vya hiyo sheria, pia hata mfumo wa kuisimami hiyo sheria yenyewe na sijui nini kimekwamisha hiyo sheria ya Mwaka 2008 ambayo ilitungwa kwa mbwembwe nyingi ishindwe kuonyesha makali yake mpaka sasa (zaidi ya mwaka mmoja na kitu).
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  1.Haijaanza kutekelezwa kwa vile regulations/kanuni bado hazijakamilika
  2. Yako mengi hayajakaa sawa kwenye hiyo sheria lakini hatuwezi kuhukumu efficacy yake kabla haijaanza kutumika kikamilifu
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Why so long kwa Kanuni kuandaliwa?.. I thought hiyo sheria is lke other public laws such as Penal Code or SOSPA ambayo could have been in opertional even outwith Regulations.

  Kwani ishatangazwa kwenye GN tarehe rasmi ya kuanza kutumika au ndo inasubiri hizo Kanuni?
   
Loading...