Inaonekana huko bongo hilo neno ni popular kwa sasa, nafikiri kwa siye tuliopitwa na mambo huko nyumbani nahisi linamaanisha kitu kama "Bitoz" au "Tozi" au "brazamen" au "bishoo"au "bishololo".
Sina hakika sana, mwenye kujua atujuze wandugu ili nasisi tukaporudi nyumbani baada ya kumaliza utumishi wetu wa kubeba maboksi huku ughaibuni tusiwe wageni wa misamiati mipya.
Video yake haijanifurahisha kushirikisha watoto ilihari madhila ya wimbo wake unaongelea na kulilia mapenzi. Nafikiri watoto hao kawapa image mbaya na ambayo mtaani iliwachukua/itawachukuwa muda kuiacha.