Itifaki imekaaje hapa

Heshima ya Jeshi ipo wapi?

Uadilifu wa wanajeshi wetu upo wapi.

Kama wanafanya hivi hadharani je huko kwenye makambi yao inakuwaje.

Uafisa wao umelowa pombe.

Sasa Imefika Maafisa wetu waende kwenye sherehe wakiwa na nguo za kiraia. Hii hapo ni kudhalilisha jeshi na Jemedari wetu mkuu kwa vyeo alivyowavika kuvifanyia mchezo.
 
Kama kuna tatizo au kama hakuna tatzo hiviiiii
 
Ni kweli huwa wanalikosea adabu hilo vazi la jeshi. Wangetafuta style zingine za kupongezana kisha lisindikizwe na wimbo wa 'Nani kamwaga pombe yangu'
 
Ndugu zangu huu ni utaratibu wao pale mwenzao anapoacha ukapela... Harusi zao huwa zinakuwa hivi, kwa hio hakuna tatizo hapo maana huwa inafanyika kwa kufuata taratibu siyo kwamba wanakurupuka tu... kwa wale ambao wamewahi kuhudhuria harusi za maaskari hili sio geni!!!
 
Akitoka hapo anaenda kuvua hizo nguo anavaa suti...!! Sasa lijamaa limekimbia toka huko kolomijeee linaletaa umbea hukuu utadhani halijawahi ona sherehe za makamandaa...
 
Akitoka hapo anaenda kuvua hizo nguo anavaa suti...!! Sasa lijamaa limekimbia toka huko kolomijeee linaletaa umbea hukuu utadhani halijawahi ona sherehe za makamandaa...

Mkuu sio kila mtu anaufahamu wa haya mambo... muelewe tu mleta mada!
 
Na wao ni binadamu, wanautashi wa kutaniana kama wasanii wanavyojiachia.

Nilisikia kofia na silaha ndo kitu muhimu yaani vikipotea hivo huna kazi, japo hawaruhusu mavazi yao yavaliwe na mtu mwingine. Ukikutwa nalo ni ama zao ama zako. Pichani simuoni na kofia wala silaha nadhani hayo wamezingatia.

Jambo afande...!!
 
Jaaa afanteeeeee.....
 
Tena bia zenyewe safari πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Tatizo la wabongo ni washamba na wanaanza ku comment kwenye picha ambayo, kwaza hawakuwepo wakati inapigwa, hawajui lilikuwa ni tukio la aina gani, taratibu za taasisi husika hawazijui. Kwa taarifa yenu hiyo ilikuwa ni ndoa ya kijeshi na ndio shamra shamra za ndoa hizo huambatana na kumwagiwa pombe. Hiyo ni officialy katika majeshi mengi duniani. Kwa nini pombe? pombe ni kiungo kikubwa sana cha mwanajeshi ndio maana hata kwenye mabwalo yao pombe ipo kwa bei poa. Na hata tafsiri ya vita (WAR) wameitafsiri W= WOMEN, A=ALCOHOL, R= RIFLE.
 
nzurii sanaa...!!
 
Za makuruta wanazimwagiaga tope....... Hata hizi si kitu mbele ya medani ya kivita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…