Itel yawakumbuka watoto yatima

Itel yawakumbuka watoto yatima

Joined
Mar 5, 2020
Posts
18
Reaction score
28
Kampuni ya simu za mkononi ya Itel imetembelea kituo cha watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chalula na vifaa vya shule.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo jana, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Fernando Wolle alisema kuwa wameona ni vyema kusherehekea siku ya mtoto wa Afrika kwa kujumuika na watoto hao.

“Katika kusherehekea siku ya Mtoto wa Afrika tumeona ni vizuri kutembelea katika kituo hiki cha watoto yatima na wao kujiona kwamba wapo katika mazingira kama wayoishi watoto wengine walio na wazazi wao.
Na siyo mara ya kwanza kutembelea kituo hiki na tutakuwa tunafanya hivi mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma na Mbeya, alisema Wolle.
Unnamed QQ Screenshot20200617183228.png

Ofisa Uhusiano wa kampuni ya itel, Fernando Wolle (kulia) akimkabidhi zawadi msimamizi wa kituo hicho


Naye msimamizi wa kituo hicho, Hassani Hamisi alisema kuwa wanaishukuru Kampuni ya Itel kwa kuja kituoni hapo na kujumuika na watoto hao.
“Tunaishukuru Kampuni ya Itel kwa kuwa siyo Mara ya kwanza kuja katika kituo chetu na kuwapa matumaini watoto yatima tulionao katika kituo chetu na tunawaomba watu pamoja na makampuni mengine yaje kwa ajili ya kutoa msaada kwa watoto hawa, alisema.
Unnamed QQ Screenshot20200617183735.png

Wakiwa katika picha ya pamoja.
 
itel ni vimeo aisee khaa! Miundo mibayaaa.
.
BTW mmefanya jema kurudisha kwa jamii.
 
Back
Top Bottom