Itazame safu ya bodi na menejimenti ya ACACIA Mining Tanzania kisha utaelewa tatizo liko wapi

hii ndo raha na heshima ya JF...Mkuu kashapuliza kipenga kwenye sekta ya madini sasa ni wajibu wetu kila mtu acheze kwa nafasi yake tuhakikishe mwisho wa mchezo hatufanyi makosa.
 
Bodi yao ina mtanzania mmoja tuu anaitwa balozi Juma Mwapachu

Tazama hapa chini:

Board of Directors

Huyu naona ndio kiungo chao Tanzania na mambo ya Government relations etc. Sijajua ana shares ngapi hapo Accacia (hakuna dhambi kwa Mtz kuwa shareholder) lakini inawezekana vipi hii kampuni iwe isha operate Tanzania kwa zaidi ya miaka 2 owe imejaa wazungu na foreigners kwenye hiyo bodi?

Sasa ukija kwenye menejimenti yao utashangaa zaidi kuona kuwa mtanzania ni mmoja tuu (Deodatus Mwanyika) na kazi yake ni hiyo propaganda aka PR. Hivi mnataka kutuambia kuwa hakuna watanzania waliosoma na wenye uwezo wa kufanya hizi kazi wanazofanya hawa wazungu?

Menejimenti hii hapa:

Management Team

Huko kwenye migodi yao sijajua nafasi wanazo nani lakini wana JF mkae mkijua kuwa hili tatizo sio ACACIA MINING pekeee bali ni makampuni mengi makubwa ya nje yanayo operate Tanzania.

Sasa ngoja ninny kwenye makampuni ya oil and gas ili mpate kuona tulips kama nchi. Yaaani kazi za kufanywa na wa Tanzania tena ambao ni wana experience, capable, competent na wana elimu zinafanywa na wageni na vibali vinatoka.

Kuna umuhim sana tukawa na sheria ya uwezeshaji wazawa au local content ama sivyo hali itazidi kuwa mbaya zaidi ya tuliyonayo kwa sasa.

Hawa wazungu wakija wanweza kuwa mabosi si chini ya miezi 6 kisha waondoke ili wazawa wafanye kazi zao. Hii inawezekana sana ni kuthubutu tuu
ACACIA MUST GO. WAONDOKE: TUNAJUA WANA NGUVU YA KIFEDHA NA WANAWEZA KUMRUBUNI YOYOTE BUT THIS TIME LAZIMA TULALE NAO MBELE. Hakuna Mchanga Kwenda Nje ya Nchi, Hawataki - WAONDOKE
 
Sasa kampuni yao, wameianzisha wao kwao huko. Huyo Mwapachu wamemuweka kwa sababu kuna sharti .

Hiyo PR wameona ni strategic choice kumuweka Mtanzania mwenzetu, ikibidi hata Kiswahili aongee nasi.


Unataka kuwapangia?

Kwa nini usiseme hao Watanzania wenye uwezo wajiunge waunde kampuni yao?

Kwa nini unataka sana Watanzania wapewe kazi kwenye makampuni ambayo si yao, tena top management.

Kwa nini unawapangia watu nani wa kumuajiri? Kwani wao wanakupangia wewe?

Wewe ibane serikali ichukue kodi, iwabane wafanye social development program kusaidia jamii za karibu hapo. Iweke labor laws kuhakikisha wanaoajiriwa kutoka nje ni essential staff na top management.

Ungekuwa na point sana kama ungesema wameleta mpaka madereva wazungu sisi waafrika tumekosa hata udereva wakati sheria za kazi zinasema haitakiwi kuwa hivyo.

Lakini wewe unalalamikia top management kuwa watu wa kwao? Kampuni ya nje?

Hata sijakuelewa bado.

Tengeneza kampuni yako.

Acha kutamani za wenzako ambazo zishatengenezwa.
acha upoyoyo Mkuu vinginevyo labda sio Mtanzania wewe....na wao kama kampuni zao mali na hawataki kufuata sheria za nchi kuhusu uwekezaji basi wangewekeza huko huko kwao wanapotoka acha kutudharau watanzania.
 
Tunahitaji serekali makini kama ya jpm ccm iko kando sasa hivi raisi haingiliwi na mtu yeyote tuliibiwa sana tunataka mapato bodi hazina faida na sisi
 
Kwani ACCASIA ni shirika la Umma? Sidhani kama wanaajiri Kwa kuangalia utaifa, wenzetu ni Result oriented
 
Huyu jamaa uchungu ameanza kuuona lini? amekuwa mbunge na waziri for twenty years, wenzake walipokuwa wanapiga kelele kuhusu hiyo mikataba ya kinyonyaji yeye alikuwa mzee wa ndio tu, aache unafiki, heri ya mchawi kuliko mnafiki.

Sasa yeye ndio kashika rungu kwanini hiyo mkataba wasifanye review kama anaona watz wanazulumiwa maana naona analilia tu, au anatafuta sababu kuna mtu anamtafuta kama kawaida yake mzee wa visasi, maana LUGUMI watu walipiga kelele wala hakuona huo unyonyaji ina maana macho yake yanaona dhuruma upande anaotaka yeye tu sehemu zingine haoni magamba kwa double standard, acheni undugu na shetani vinginevyo moto unawasubiri kuwameza wenyewe haujari kama uliwahi kuwa president.
 
Kwani ACCASIA ni shirika la Umma? Sidhani kama wanaajiri Kwa kuangalia utaifa, wenzetu ni Result oriented
Issue hapa ni local content participation
Haiwezekani Manji alate secretary kutoka filipino kuja kufanya typing pale Quality Group huo ni wazim
 
Issue hapa ni local content participation
Haiwezekani Manji alate secretary kutoka filipino kuja kufanya typing pale Quality Group huo ni wazim
Hapo ndipo tujiulize, kama anaweza kuwagharamia hao na bado akapata faida, anafanyafanyaje
 
Kampuni ya wenzio unataka wajae watz, washauri wabongo nao waanzishe zao ili wajazane huko....nyerere aliwaanzishia makampuni kibao mkayaua na hizo shule zenu sasa naona unata mjazane mkayaue...halafu muanze kutafutia PhD kwa kuandika paper kwanini yamefail.

Ni kweli mkuu, kwanini tuwapangie?
 
Upinzani umeshindwa kuibua hii umekazana na issue za kina Ney,TLS,Clouds mpaka Magufuli anakuja kuibua hili halafu tunaponda jambo la msingi ni kwamba huo mchanga uchenjuliwe nchini kwa sababu mashine hizo zinaweza kujengwa hapa
 
Kampuni ni ya wazungu, hakuna ajabu mabosi wa juu kuwa wazungu katika kampuni yao. Ukiona kuna mtanzania naye ni bosi hapo basi ujue ni Kibaraka wao au Kivuli tu ili kuturidhisha wadanganyika.

Tuwaache na kampuni yao, sisi tukomae kurekebisha sheria zetu na kukusanya kodi na mrahaba. Tukiweza tuanzishe kampuni zetu ili tufanye tunachokitaka.

Halafu usisahau kuwa watanzania wengi ni sifuri kwenye biashara na wezi wa mali, ukiwapa nafasi wanaweza hata kufilisi kampunj.
 
Back
Top Bottom