Itanisikitisha sana kwa mataifa ya afrika!

Itanisikitisha sana kwa mataifa ya afrika!

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
8,596
Reaction score
5,584
Yakiendelea kupeleka majeshi kwa kivuli cha umoja wa mataifa au umoja wa Afrika katika nchi ambazo kwa namna moja ama nyingine vita zake zimeanzishwa na wakoloni. hili litakuwa ni sawa na kuunga mkono ukoloni wao, na si hivyo tu bali pia iko siku nasi tutakuwa wahanga wa matukio ya aina hiyo. Viongozi wetu wanapaswa kufikiri kabla ya kumfuata MBWA KIPOFU ambae ATATUTUMBUKIZA katika SHIMO tusilolijua!

Nikiangalia DEMOKRASIA ambayo MAREKANI na WASHIRIKA wake wanayoitaka LIBYA, IRAQ, AFGHANISTAN, MALI, SUDAN KUSINI na kwingineko. Kisha nikitafakari akili za watawala wa KIAFRIKA SIPATI PICHA! maana wakubwa hao wanaobabudiwa na watawala wengi wa kiafrika wakishasema tu, mataifa yetu huwachukua kaka na dada zetu kwenda kulinda amani ambako wao hukutwa na vifo ambavyo visingelikuwa na ulazima kwani wanaopaswa kumaliza matatizo hayo ni wale walioyaanzisha. Je tunyamaze mpaka lini? Hapa ndipo namkumbuka mzee Madiba, Mola ampe pumziko la amani.

HERI TUNGEKUWA WATUMWA WA MWILI KULIKO UTUMWA HUU WA AKILI.
 
HERI TUNGEKUWA WATUMWA WA
MWILI KULIKO UTUMWA HUU WA
AKILI

we chizi kweli. nenda uarabuni ukatumikishwe basi.

sitetei hao wakoloni, lakini hilo ni wazo puuzi mno.
 
Back
Top Bottom