Itanichukua muda gani kusajiri kampuni brela? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Itanichukua muda gani kusajiri kampuni brela?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kalunguine, Apr 22, 2012.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nnahitaji kufungua kampuni in partnership na mtu ambaye si mtanzania, process zote zitachukua muda gani hadi kupewa certificate? Ni vitu gani ntahitaji ambatanisha napoenda sajiri?
  nmeshapitia website ya brela, ila nahitaji majibu ya mtu ambaye ameshafanya hili.
   
 2. A

  Akiri JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  unataka kampuni ya aina gani ,? sole proprietor, partnership au limited. unataka usajiri wa blela peke yake ? vp TRA na licence, nipe kazi hiyo nikufanyie ndani siku 21 kwa ltd co. na 14 days kwa sole proprietor. 0657 14 5555. 0686 200 117 , 0755099 291
   
 3. POLITIBURO

  POLITIBURO Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Akiri acha kabisa mchezo huo! Ebu mjibu haraka maswali yake yafuatayo:-
  1. Process za usajili wa kampuni itamchukua muda gani hadi kupata Certificate of Incorporation?
  2. Ni vitu gani (Docs) awe nazo wakati wa kufanya usajiri BRELA?
   
 4. m

  mchambakwao Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama upo mjini we nenda Dar pale jengo la ushirika mtaa wa Lumumba ukaulizie chochote unachopenda kukifahamu kutoka kwao.Humu utakutana na akina Akiri wengi,kuwa makini mjini hapa.Watu wanajenga na kununua magari kwa kazi kama hizi kwa watu wasiojua taratibu za mambo mbalimbali
   
 5. Doyi

  Doyi JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 747
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Kaka wala usijusumbue kichwa.Nakukutanisha na mdau mwaminifu sana na ameshasaidia wadau weng humuhumu Jf.Anakufungulia kampuni na mambo yote ya lesen na TIN number ndani ya wiki 1 unapata kila kitu kwa uaminifu mkubwa.Kama hutojali mcheki kwenye0714074040,0767074040,0783074040
   
 6. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Kuna namna mbili kiutaratibu na kimjini
  kiutaratibu(kichwakichwa) : kwanza unaanza na name search ,hii ilitakiwa iwe solved through BRELA website,lakini ili wasife njaa (wenyewe wanajua) wanahakikisha haiko updated na haina msaada wowote. Hivyo utachukua wiki 2-3 au zaidi kwa ajili ya kupata jina ambalo halijatumika bado ili uweze kulitumia wewe.
  Pili kutayarisha MEMART(Memorandum and Articles of Association) mpaka ipitishwe itakuchukua zaidi ya wiki tatu.Kwa hiyo utahitaji takriban miezi miwili au zaidi ili upate usajili.Na hii ni chamtoto,ngoma nyingine ipo kwenye TIN(ingawa ni bure na inatakiwa iwe straight forward lakini this is bongoland!)

  Ki-mjinimjini(kiutaratibu lakini mikono mitupu hailambwi): Hii huchukua maximum wiki mbili kupata Registration Certificate,MEMART na TIN Certificate.Kila kitu kina mwenyewe,haina ubishi.Sasa hapo waweza pima mwenyewe kati ya hizo njia mbili itakayokufaa!
  Unless uwe umekaa sana nje ya TZ ,otherwise utajua cha kufanya.All the best
   
 7. C

  Cousin New Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nami nime elimika japo nataka jua je? kama nina kitabu changu nataka sajili taratibu zikoje?
   
 8. m

  missilicious Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo TIN inatolewa kitengo gani pale TRA? nu lazima itolewe makao au??
   
 9. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Waheshimiwa,sasa mambo ya mtu wa kati ya nini? I mean do we need middlemen in this if all the procedures are straight forward? Suala hili la watu wa kati nasikia hata mahakama za Dar lipo. Mtu unakesi, bado wapo watu wanakula kwa 'kusema wanakusaidia' kwa mh hakimu! Sijui nchi gani tunajenga, ama ndo kuendeleza upindishaji wa sheria na taratibu? Kama tunakuwa hatuna majibu, basi tukae kimya badala ya kusema tunaunganisha na watu....sijui huu ni msaada gani kama taasis anayoendea ni ya umma na inapaswa ku-operate kwa uwazi? Unless mnataka kutuambia BRELA kuna suala la kujuana!
   
 10. T

  Tafakuru Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15

  Mwana jamvi, naona unakosa experience na hii nchi kwa kiasi kikubwa sana. Siku ukidil na BRELA utaelewa tu kazi ya middle men sasa ivi naona msaada wa kukuelimisha sina Experience will teach you beta
   
 11. POLITIBURO

  POLITIBURO Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF mimi naamini hapa ni sehemu ambayo Great Thinkers think deeper and sharpen their thinking. Mwanajamvi anatoa hoja inajadiliwa na siyo kuteka hoja kwa style ya Makuwadi wa Soko Huria! Mwanajamvi anapohitaji msaada wa mawazo au maelekezo hatuna budi kuwa positive katika kumpa msaada anaohitaji na siyo kuteka hoja yake kwa kigezo "nikusaidie". Daima middleman anamuongezea mlaji gharama zisizo za lazima. Udalali wa namna hii naufananisha na mimea uota na kukulia mgongoni mwa mimea mingine ambayo hunyonywa hadi inakufa. Huu ni unyonyaji. Si nzuri. Mi nakwambia kwa anayehitaji huduma ya BRELA nenda ofisini kwao utapata huduma nzuri. Watanzania hizi short cut and violation of stipulated laws, rules and regulations siyo tabia nzuri. Ebu tukemee makuwadi wa soko huria.
   
 12. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Utakesha.....kwa system ya nchi hii,huduma yeyote bila middlemen/vishoka mambo hayaendi.....dah!sijui wewe wa wapi!
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,841
  Likes Received: 2,772
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu wa-TZ huwa tunakurupuka. Unataka kusajili kampuni unalazimisha mambo yakamilike ndani ya siku 3, wapi na wapi wewe? Hapo ndipo vishoka tunawapa nafasi. Kwa nini usiruhusu zoezi lichukue mkondo wake? Vumilia hata kama itachukua muda wa miezi miwili. Mie nilijaza fomu zao nikawaachia hapo baada ya mwezi nikaenda chukua cheti changu! Jamani tubadilike, vinginevo tutanyonywa mpaka basi!
   
 14. MSeush

  MSeush Member

  #14
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na wote wanaosisitiza kufuata utaratibu ktk kufanikisha jambo lolote,tatizo kubwa wa Tz.tumekuwa watu wa kutafuta sn njia za mkato ndio sababu kila kitu tunalazimisha kutoa vijisent ili kupunguza mchakato.Nakushauri nenda Ofisi za brela utapata utaratibu wote na achana na Vishoka.
   
 15. C

  Ctanda99 Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka usidanganywe na mtu,kitu cha kwanza kabla ya kwenda brela tafuta mwanasheria akutengenezee memorandum na article of association wanasheria wanajua,baada ya hapo nenda straight brela watakupa maelekezo,TRA unaenda baada ya kupata certificate of incop. Gharama zote hazizidi 600,000 kaka kuwa makini!
   
Loading...