Itakuwa vipi endapo ripoti ya tume no2 ikitofautiana na ile ya tume no 1?

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,846
5,057
Najiuliza swali kama hilo juu ya taharuki itakayoikumba Tanzania pale tume namba mbili iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mchanga itakapokuja na matokeo tofauti kabisa na Yale ya time no mbili? Rais atavhukuwa hatua gani?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Maswali magumu,pia hata matokeo yakifanana,lazima italeta maswali zaidi,na kuna uwezekano hii tume ya pili ikalazimishwa kuchana karatasi ili iandike upya kuendana na tume ya kwanza

Ripoti zikifanana tutaomba mkemia mkuu wa serikali kupitia kitengo cha DNA awapime wajumbe wa tume zote mbili,inawezekana wakawa identical twins

Identical twins ni mapacha wanaofanana sana wengine hufikia mmoja akiugua(akipeleka ripoti ya mchanga),basi utasikia na mwenzie anaumwa(ripoti itafanana)
 
Najiuliza swali kama hilo juu ya taharuki itakayoikumba Tanzania pale tume namba mbili iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mchanga itakapokuja na matokeo tofauti kabisa na Yale ya time no mbili? Rais atavhukuwa hatua gani?
Unayafahamu majukumu ya tume ya pili?
 
Tume ya pili lazima itofautiane na ile ya kwanza kwani hii ya pili inakuja kutuonesha athari za kiuchumi tulizozipata kwa ajili ya wizi huu wa mchana
 
Hivi hata baada ya waziri mkuu kuongea leo bungeni bado hujajua matokeo ya tume ya pili?. Kifupi ni kwamba wameshasalim amri,tume ya pili inakuja na mambo ya sijui mikataba,sheria za madini sijui mambo ya mahusiano ya kimataifa na bada ya hapo mchanga unakwea pipa kama kawa. "Akili za Mchanga"
 
Tume ya Pili nadhani inajikita zaidi katika Uchanganuzi wa sheria, Mikataba pamoja na athari za Kiuchumi.

Kwa namna yeyote ile hazitagongana wala kufanana.
 
Tume ya pili lazima itofautiane na ile ya kwanza kwani hii ya pili inakuja kutuonesha athari za kiuchumi tulizozipata kwa ajili ya wizi huu wa mchana
Walijuaje kama kuna athari wakati iliundwa kabla ya ile ya kwanza kuleta majibu?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Najiuliza swali kama hilo juu ya taharuki itakayoikumba Tanzania pale tume namba mbili iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mchanga itakapokuja na matokeo tofauti kabisa na Yale ya time no mbili? Rais atavhukuwa hatua gani?
Inaelekea hili sakata hujalifuatilia vizuri
Kwani kila tume ilipewa majukumu mawili tofauti
Tume ya kwanza ilikua inachunguza kiasi cha madini kilichopo kwenye mchanga
Tume ya pili yenyewe inachunguza athari za kiuchumi na sheria
Hivyo ripoti haziwezi kufanana
 
Najiuliza swali kama hilo juu ya taharuki itakayoikumba Tanzania pale tume namba mbili iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mchanga itakapokuja na matokeo tofauti kabisa na Yale ya time no mbili? Rais atavhukuwa hatua gani?
Never, wata harmonize
 
Hivi hata baada ya waziri mkuu kuongea leo bungeni bado hujajua matokeo ya tume ya pili?. Kifupi ni kwamba wameshasalim amri,tume ya pili inakuja na mambo ya sijui mikataba,sheria za madini sijui mambo ya mahusiano ya kimataifa na bada ya hapo mchanga unakwea pipa kama kawa. "Akili za Mchanga"
Tume ya pili itamwambia mkuu kwamba mikataba imebana,huna pa kukwepea,ruhusu mchanga uende!
 
Najiuliza swali kama hilo juu ya taharuki itakayoikumba Tanzania pale tume namba mbili iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mchanga itakapokuja na matokeo tofauti kabisa na Yale ya time no mbili? Rais atavhukuwa hatua gani?
tume # 2 ataitumbua kwa madai ya taarifa za kiinteligensia kuwa kuna baadhi ya wajumbe wachache wa tume "wanaotumiwa na majizi" wamevuruga uchunguzi!
afu itaundwa tume # 3 ya wajeda watupu dadeki!
 
Back
Top Bottom