Itafutwe formula mpya ya ruzuku kwa vyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Itafutwe formula mpya ya ruzuku kwa vyama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Feb 2, 2010.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Feb 2, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,311
  Likes Received: 1,078
  Trophy Points: 280
  Sheria ya vyama vya siasa Tanzania inaruhusu kila chama kupata ruzuku kutoka serikalini kwa kufuata uwiano wa idadia ya wabunge watokanao na chama kile. Kama chama hakina wabunge kabisa basi huenda hakipati ruzuku kabisa.

  Kwa tanzania ambayo haina infrastructure, kuendesha kampeini ya kitaifa ni gharama kubwa mno kiasi kuwa ni vyama vyenye rasmilali nyingi tu ndivyo vinavyoweza kufanya hivyo kwa ufanisi. Njia ambazo zinaweza kukiingizia mapato bile kutegemea serikali ni pamoja na ada za wanachama, michongo ya wafadahili, na vitega uchumi.

  Mapato ya vyama yatokanayo ni ada za kawaida za wanachama hayatoshi kabisa kuendesha kampeini za uchaguzi kitaifa hata kama kina wanachama nusu ya watanzania wote.

  Matumizi ya michango ya wafadhili ni jambo ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa makini kwa sababu tumejifunza kuwa wafadhili wa chama kinachokuwa madarakani baadaye hugeuka kuwa na sauti nzito sana katika serikali ingawa wao wenyewe hawana madaraka. Sababu za kihistoria zimeonyesha kuwa wafadhili wengi wa aina hiyo wanakwenda CCM kwa kuamini kuwa ndiyo iko madarakani na kuna payback kubwa. Tatizo la ufisadi linalotukumba sana ni mojawapo ya matokeo ya wafadhili wa aina hiyo, hivyo ingekuwa vizuri sana kukawa na sheria inayothibiti michango ya wafadhail.

  Mapato kutokana na vitega uchumi pia ni jambo ambalo bado lina utata sana hapa Tanzania hasa kwa vile CCM imebaki kuwa mmiliki wa vitega uchumi vilivyochangiwa na watanzania wote wakati wa chama kimoja. Vyama vilivyoanziswha baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza havikutendewa haki na serikali iliyokuwa madarakani katika mgawanyo wa mali zilizokuwa zinamilikiwa na CCM kabla ya mfumo huo vyama vingi kuanza.

  Njia kubwa inayobaki katika kusaidia vyama kujiendesha ni ruzuku ya serikali. Hata hivyo kwa vile ruzuku hii inawiana na wingi wa wabunge, ambao wanapatikana kutokana na kufanya kampeini nzuri, ambazo zinategemea pesa, utakuta kuwa vyama vipya vinapata wakati mgumu sana kushindana na CCM kutokana na ukosefu wa raslimali: duara jeuri (vicious circle) la umaskini wa vyama. Kwa hali hiyo ni wazi kuwa ruzuku ya serikali haisadii kukomaza demokrasi nchini kwa vile inalinda status quo ya "CCM ndiyo wenyewe" na kuacha vyama vidogo vibaki kuwepo kwa jina tu vikingojea kufutwa na msajiri. Ninashauri sheria hiyo ya ruzuku itazamwe upya. Kwa vile tunatumia utaratibu wa mtu mmoja kura moja, basi matokeo ya uchaguzi yasitumike katika formula hiyo ambayo kwa sasa inaruhusu utaratibu wa "the winner takes all" na hivyo kuipa upendeleo mkubwa CCM.

  Kuna formula za aina nyingi zinazoweza kutumika. Endapo matokeo ya uchaguzi ndiyo njia pekee inayoonekana kuwa yenye haki, basi tubadilishe utaratibu wetu wa uchaguzi kwa kuruhusu wapiga kura kuchagua zaidi ya mgombea mmoja katika uchaguzi. Njia nyingine ni pamoja na kutoa ruzukua kufuatiwa idadi ya wanachama wa chama katika kila quota ya miezi mitatu mitatu (wanachama wanaweza kuhama chama) kadri watakavyokaguliwa na ofosi ya msajiri wa vyama; vile vile ruzuku inaweza kufuata bajeti ya chama kadri itakavyokaguliwa na kuhakikiwa na Mkaguzi mkuu wa serikali ili kuondoa inflated numbers na matumizi yasiyokuwa ya lazima.

  Nina imani kuwa kuna njia nyingi sana zinazoweza kutumika ili kuvipa uhahi vyama vyetu vya saisa, lakini huu wa ruzuku uliopo sasa siyo njia nzuri.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...