It simply ain't fair

It simply ain't fair

Capt Nemo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2015
Posts
1,445
Reaction score
681
Rafiki yangu Mr. Pess baada ya kusota na kazi za "below degree level" na kuona mandeleo hayaji kaamua kujiwekea kijihakiba kwa kula mihogo na maji badala ya lunch. Baada ya kuipata hela ya kutosha kucover miaka mitatu ya chuo (or so he thought) karesign sehemu yake ya kazi (formerly an IT) na kwenda chuo kusomea U-Zakayo

Kahassle chuo kwa miaka mitatu..kwanza kufika mwaka wa pili ile budget aliyoaandaa ya miaka miwili ishakata kitamboo na home pana wife na one beautiful kid wanamuangalia.

Basi hivyo hivyo kimkanda mpaka kamaliza last year..mbilinge sasa kuitafuta ajira..application 1000+, interview 100+ nk..mpaka hivi majuzi kapata tip kuwa kuna application zinapokelewa mkoani kwa katika institution flani inajihusisha na mambo ya Credit and Lending....kapiga simu na kuambiwa ni kweli na application ya kwanza it is thru mtandao..Mr. Pess kaituma application. Jamaa kajifanyia tathmini kakumbuka mambo ya Customer Evaluation, CAMPARI, nk yanapanda

Baada ya siku kama 6 kapokea simu kutoka kwa mdada wa shirika hilo anamtaarifu kuwa interview ya ana kwa ana ni kesho yake saa 3 asubuhi...na mida hiyo anapokea simu ni saa tisa alasiri..jamaa kuuliza mbona taarifa kapata ya kustukiza mdada akamwambia simu yake ilikuwa haipatikani kwa muda flani...na kamsisitiza kuwa jina lake (Mr. Pess) liko second katika batch ya kwanza ambayo ni favourite kupata nafasi maana imearrangiwa kwa mpango huo..jamaa kadata

Home kashauriana na wife nini la kufanya..wakafikia muafaka wakwangue akiba yote, I mean yote ili jamaa achukue flight..huyooo mbio mkoani...kamuacha wife na mtoto na deficit budget!!!

Kesho yake kama kawaida interview ya kwanza ikafanyika..jamaa kamwagiwa sifa kishenzi..with words like.."You are the best among all aspirants"...we would be hanoured to work with you if the pannel selects you" na shombo nyingine kibao!!! Ila kwa sababu flani flani inabidi interview ya pili na ya mwisho ifanyike next week..jamaa hoi...kurudi Dar kwanza haiwezekani...huko home wife alimuacha na hela ya kuhesabu...Mr. Pess kapiga moyo konde kaamua kukomaa huko huko

Week ilofuata interview ikafanyika na jamaa wakaambiwa waende watajulishwa matokeo thru contact walizotoa..jamaa karudi guest house ana usawa wa kulipia chumba kwa siku hiyo na hela pungufu ya nauli...kwa bahati mbaya wakati anatoka Dar alisahau line yake moja ya simu ambayo ina contact za watu hivyo namba za jamaa wa karibu hana....kachekecha akili kaamua kumchek mtu wasiyefahamiana hata kwa sura..akalia shida na jamaa kamtumia amount ya kutosha kumaliza tatizo la kurudi town

Basi jioni hiyo jamaa akaamua kwenda mahali kuangalia taarifa ya BBC..kajikunja mezani Bar na soda yake..mara meza jirani wakakaa jamaa kama wanne hivi..wakati wanapiga story jamaa akastukia wanaongelea lile shirika alilofanya interview na wanaongelea habari ya zile ajira zilizotangazwa..BOTTOM LINE YA MAZUNGUMZO NI KUWA WATATU KATI YA WALE JAMAA WALIKUWA WAMEAJILIWA WEEK 2 KABLA!!!! na all along applicants walikuwa wanaambiwa nafasi ni tatu tu!!! Jamaa kabaki hoi

Complain yake sio udanganyifu wa kuwapa watu kazi na kuwafanyisha wengine interview, hilo kwa sasa ni common place...yeye anauliza:

was it necessary to go thru the motions ambazo zinamsababishia mtu kukurupuka na ndege wakati akiwa mjini usafiri luxury kwake ni bodaboda?

is it fair kumtoa mtu Dar mpaka Mwanza, kumfanya a-incur costs za guest houses, usafiri pale Mwanza, Chakula, nk kwa ajili ya kucover tu njia chafu za kutoa ajira?

Knowing kwamba yupo Dar, lisingekuwa jambo la busara kwa wale waajiri kuuchuna tu au kumwambia at least kuwa hajameet vigezo?

This ain't fair!!!!
 
Mwambie mateso ya aina hiyo yakizidi ujue faraja ipo karibu. Batter pray.
 
Siyo fair, mwambie aendelee kuwa mvumilivu, au kama anaweza kujiajiri ajiajiri, kupata kazi ni ngumu sana, watu wanaajiri watu wasiokuwa na vigezo mwisho wa siku wanaharibu kazi.
 
Back
Top Bottom