Israel yaomba nafasi AU.

Israel yaomba nafasi AU.

Bahati furaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
3,077
Reaction score
1,439


Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu


WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema, nchi hiyo inakuza uwepo wake na kuzidisha uhusiano na Afrika kwa kuwa ina imani na hali ya baadaye ya bara hilo na inalipenda.

Alisema angetamani kupata nafasi hata ya kuwa mwangalizi ndani ya Umoja wa Afrika (AU) akisisitiza kuwa Israel inaweza kuboresha maisha ya watu popote, lakini kwanza barani Afrika na kuongeza kwamba katika kufanikisha hilo, Israel inafungua ubalozi jijini Kigali, Rwanda.

Kwa sasa Balozi wa nchi hiyo anaishi Ethiopia akitoa huduma za kidiplomasia kwa nchi za Rwanda, Burundi na Ethiopia. Mwaka 2015 Rwanda ilifungua ofisi ya Balozi jijini Tel Aviv, Israel.

Waziri wa Nchi, Mambo ya Nje, Ushirikiano na Mambo ya Afrika Mashariki wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe alisema, kufunguliwa kwa ubalozi wa Israel jijini Kigali kutaimarisha uhusiano baina ya nchi hizo.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, ubalozi huo huenda utafunguliwa Juni- Julai mwakani. Kwa mujibu wa Waziri Nduhungirehe, pamoja na mambo mengine, ubalozi huo utaongeza fursa kwa wafanyabiashara wa Rwanda na Israel.

Waziri Nduhungirehe alisema ubalozi huo pia unatarajiwa kuwezesha kuanzishwa kwa safari za ndege kati ya Kigali na Tel Aviv. “Israel na Rwanda zimekuwa na uhusiano mzuri na zimeshirikiana kwenye mambo mengi.

Uamuzi wa kufungua ofisi umefanywa wakati mwafaka na utakuza ushirikiano,” alisema. Novemba 28 mwaka huu, Netanyahu alikwenda Nairobi, Kenya kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta na alizungumza na wakuu mbalimbali wa nchi za Afrika.

Wakati akizungumza kwenye Ikulu ya Kenya alisema, Israel iliomba kupewa hadhi ya kuwa mtazamaji kwenye Umoja wa Afrika (AU) kwa kuwa inataka kufanya kazi na Afrika.
 
Wamewachonganisha Waarabu wee wakafanikiwa, daha sasa wanataka kuja kwetu Daah twafwa
Na kwanini hao waarabu wakubali kuchonganishwa wakati Ni wafuas was dini ya kweli? Kwanini wakubali kuchonganishwa Na kuuwana hovyo hovyo wao kwa wao. Kwanini hao waarabu wasiwachonganishe waisrael wauwane wenyewe kwa wenyewe???
 
Na kwanini hao waarabu wakubali kuchonganishwa wakati Ni wafuas was dini ya kweli? Kwanini wakubali kuchonganishwa Na kuuwana hovyo hovyo wao kwa wao. Kwanini hao waarabu wasiwachonganishe waisrael wauwane wenyewe kwa wenyewe???

Wamezidiwa M M
 
Hawa si walikuwa wamepewa Uganda kwanza ili waje waishi? Ngoja waje waidai rasmi


Hawa si wanaamini ardhi yote kati ya Nile na Tigris ni yao?, ngoja waje waanze kudai bonde la mto nile
 
Israel apewe nafasi haraka sana iwezekanavyo! Sababu zilizokuwepo enzi hizo za kuitenga hazipo tena wala hazina mashiko. Zilikuwa propaganda mfu tu za waarabu ambao wamekuja kudhihirika baadaye "sio watu" zaidi ya urafiki wa kinafiki kwa manufaa yao.
 
Na kwanini hao waarabu wakubali kuchonganishwa wakati Ni wafuas was dini ya kweli? Kwanini wakubali kuchonganishwa Na kuuwana hovyo hovyo wao kwa wao. Kwanini hao waarabu wasiwachonganishe waisrael wauwane wenyewe kwa wenyewe???
Subiri kwako yatengemae ndiyo utajuwa utamu na Uchungu wa Israel or Rwanda !!
 
Back
Top Bottom