econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 22,138
- 32,716
Mimi nasimama na Israel kwenye mapigano haya, ila tu kwa niliyoyaona Jana naweza kushauri kwamba Sasa inatosha. Nadhani kwa Sasa Israel isistishe mapigano na Hamas maana kwa Sasa wanaoumia sio Hamas ni raia wa kawaida wa Gaza. Kama ni kisasi kimeshalipwa. Maana mpaka Sasa wameuawa wapalestina 11,500. Ambao watoto waliokwisha uawa wanakaribia 5,000 hii inaumiza Sana.
IDF kashamsambaratisha Hamas sidhani Kama Kuna haja ya kuendelea na mashambulizi. Kwa Sasa Hamas Hana nguvu na wapalestina wamejifunza kwamba mbeleni wasifanye uchokozi kwa Israel wa aina ile.
Kuna mambo matatu nimeyaona yamenifanya nifikirie hivyo.
1. Kwanza, Jana Israel kashambulia na kuilipua kwa makombora shule ya watoto na kuua watu hamsini ikiwemo watoto wadogo. Shule hiyo inaitwa Al Buraq, na inasemekana mjukuu wa kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh aliuawa kwenye mashambulizi hayo.
Sababu kuu ya IDF kuishambulia shule hiyo ni baada ya kamanda wa Hamas Ahmed Siam aliyekuwa kwenye mapambano na IDF kwenye eneo la Hospitali ya Rantisi Kuzidiwa na kwenda kujificha kwenye shule hiyo. Hivyo Israel ikaona immalize pamoja na watoto waliokuwemo humo. Kwa kweli niliumia kuona watoto wasiokuwa na hatia wakiuawa kwa ujinga wa Hamas. Nikawaza itakuwaje kwa huko mbeleni?.
2. Pili, Kuna Jambo la kusikitisha kwenye Hospitali ya Al Shifa. Ni kwamba IDF imeizunguka hiyo Hospitali na kuanza mashambulizi. Tatizo ni kwamba Kuna vitoto vichanga karibia 39 vimo humo ndani, ndio kwanza vipo kwenye incubator. Sasa ninachoogopa IDF asije akailipua Hospitali nzima na kuua hao watoto.
Nasema hivyo kwa sababu IDF anaweza kuilipua Hospitali nzima ya Al Shifa kwa kuwa kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar kajificha humo pamoja Viongozi wachache waliobakia.
Kingine ni kwamba ndani ya Hospitali hiyo Kuna wagonjwa wengi mahtuti na wazee. Hivyo kuilipua itasababisha mauaji ya halaiki.
3. Tatu, iwapo IDF itailipua Hospitali hiyo Kuna uwezekano wa Mataifa ya kiarabu kulazimishwa kuingilia kati na kuendeleza mgogoro kuwa mkubwa na kupelekwa hata vita vya tatu vya dunia.
Maana Al Shifa imekuwa Kama mtego. Ndio maana Hamas wameruhusu watu wengi wawe pale ili Israel asipate nafasi ya kuishambulia. Maana lile ndio eneo la mwisho kabisa kwa Hamas kujilinda. Hivyo hakuna haja ya kumwaga damu nyingi. Wakubaliane Israel asogee nyuma na Hamas wawaachie mateka basi. Mambo mengine yaendelee.
Hivyo basi, naishauri Israel ifanye yafuatayo.
1. Kutangaza kusitisha haya mapigano, maana wanaoadhirika ni watoto, wanawake na wazee na sio Hamas Tena.
2. Israel atangaze kuwepo na Kambi ya jeshi itakayosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Kambi hiyo iwe kilometa ishirini kati ya mpaka wa Israel na Gaza.
3. Israel ifanye makubaliano na Hamas ya kuondoka Al Shifa na Hamas wawaachie mateka waliowashika. Na makubaliano haya yasimamiwe na Umoja wa Mataifa.
4. Jukumu la kuisimamia Gaza liwe chini ya Mahmoud Abbas ambaye kisheria ndio Rais wa Palestina, Gaza ikiwemo. Ili kuendeleza makubaliano ya Oslo ya mwaka 1993 ili mchakato wa kuanzisha taifa la Palestine lianze..
4. Nanshauri kuwepo na makubaliano kati ya Palestina kwa niaba ya Hamas na Israel upande mwingine , kwamba hawatovamiana Tena.