Israel na Pegasus spyware

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,151
33,335
Dah Mimi sio mtaalam kabisa wa mambo haya. Mambo ya udukuzi.lakini nimeingiwa na hofu Sana.
Pegasus Ni kifaa kilichotengenezwa na kampuni binafsi ya Israel.
Pegasus spyware inaweza kupenya kwenye simu za smart na kufyonza ujumbe wote,picha zote na kurekodi mazungumzo.

Pegasus imeshatumika kulenga Marais kumi na Moja Waziri Mkuu mmoja na mfalme mmoja..
Pia wanasiasa wa vyama vya Upinzani hawakubaki salama.

Serikali zilizouziwa kifaa hiki zimekitumia kuwachunguza watu ambao serikali iliwaona Ni kero kwake.

Pegasus imekua ikiuzwa kwa Siri Sana na kampuni hiyo kwa nchi zilizofanyiwa uchunguzi wa kutosha.
Hofu niliyonayo Ni usalama wa uhuru wetu,wa viongozi wetu na hasa viongozi wetu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Hivi najiuliza kweli Tuko salama?
Pegasus imekua ikitumiaka kunasa mawasiliani ya viongozi wa kisiasa wa upande wa Upinzani huko kote ilikouzwa,watu maarufu na hasa viongozi.

Rais wa Ufaransa ametoa anti uchunguzi ufanyike juu ya uwepo wa kifaa hiki.

Habari hii nimeipata kutoka Al Jazeera.

Wataalam wa hizi mambo karibu hapa.
 
Mkuu hayo ni mambo ya kawaida mno kwenye ulimwengu wa kijasusi,kuna mazito zaidi ya hayo siwezi kuyasema hapa.
 
Nakupa moja iliyotumika nchi moja ya afrika mashariki.

Alikuja mgeni mmoja mashuhuri ile convoy yake ya usalama ilipoingia ikulu kumbe viatu yao vilikuwa vinaacha gadgets zenye ncha kwenye mazulia ya ikulu hizo gadgets zilichongoka chini mithili ya sindano yenye ncha Kali na ziliachwa Pini nyingi Sana kuanzia za kusikiliza mpka za kuingilia mifumo ya kompyuta za ikulu kilichotokea nyuma ni disaster.
 
Bro, unaweza kuwa specific hii ilitokea wapi exactly namaanisha nchi gani!!? Maana niliona Mwaka juzi wachina walijenga makazi ya rais kule Burundi na Pierre alienda kuzindua.
Sasa msitake kuniambia kama alihamia mule na kuanza kufanya kazi za kiserikali mule, maana akifanya hivyo hatuwezi jua wachina wamepandikiza nini mule
 
Wachina ni balaa!! Si ulisikia kilichotokea kwenye jengo la AU? walijenga bure kama msaada kumbe wameacha mambo yao usiku data zotee zinakuwa transferred kwenda Shangai...imekuja kushtukiwa baada ya mwaka na nusu
 
Hiyo inatajwa ni kampuni binafsi,lakini ikija kuchimbwa zaidi unaezakuja kuta ni kampuni yenye mafungamano Ya kutosha na mashirika makubwa Ya kijasusi .....
 
...ulimwengu wa kijasusi una mengi ya kushangaza, ila kwa dunia ya Sasa ya kiteknolojia huwezi kuzuia kwa asilimia 100 kudukuliwa.
 
Hii hainishangazi Waisraeli kuwa na hii program, tena zipo nyingi watu hawajazijua na haishtui ulimwengu wa ujasusi. Ndio maana Osama bin Laden hakuwa anatumia simu wala kompyuta, ni mwendo wa barua na wajumbe

Miaka ya 1970s na 80s Wasovieti chini ya KGB walikuwa na vifaa vya kudukua visivyofikirika. Walienda nje ya jengo la ubalozi la Marekani nchini kwao nje wakaweka kisiki cha mti cha bandia, humo wakaweka vifaa vya kudukua mawasiliano ubalozini kilikaa muda kabla hawajakigundua

Nyingine kuna siku balozi wa Marekani alitembelea nursery school mjini Moscow akapewa sanamu la mbao la ngao ya Marekani ile yenye ndege tai. Balozi akakurupuka kuiweka ofisini maana ilichongwa kwa ustadi na hawakuitilia shaka kisa imetolewa na mtoto. Haikuwa inafanya transmission kila muda ili isijulikane na isiishe chaji, Warusi walikuwa wanapita na gari nje ya ubalozi kila siku kadhaa, wanaiactivate inatuma data zote faster. Kitendo cha gari kupita mbele ya ubalozi wala bila kusimama washakusanya mazungumzo yaliyofanyika ofisi ya balozi na kwenda nayo

Siku hizi majasusi wababe hamna maana vita baridi haipo. Hii Pegasus ni wafanyabiashara hata nchi njaa kali wanaweza iuzia huu mfumo. Miaka ile Marekani ilikuwa haiwezi kuipatia Uingereza baadhi ya mifumo sembuse kuiuza
 
Hiyo inatajwa ni kampuni binafsi,lakini ikija kuchimbwa zaidi unaezakuja kuta ni kampuni yenye mafungamano Ya kutosha na mashirika makubwa Ya kijasusi .....

Ni Co. binafsi ila haiuzi hizo products bila clearance kutoka Wizara ya ulinzi.
 
Kwa hiyo hata wale waliovujishwa taarifa za kumsema Jiwe ilitumika hii?
 
Back
Top Bottom