... AND of course it shouldn't do the striking!!!
Hii ni siri, wewe umejuaje?
Bora waipige mapema kabla hawa magaidi hawajamiliki silaha za maangamizi....go Israel go...
wenyewe wanaojiita wayahudi wanawachukia wakristu+waislamu.
Mzee Richard, shukrani kwa assessment yako kuhusu huu mgogoro, lakini nadhani ka-research ka kina kangesherehesha mambo. Binafsi nadhani kwamba Israel hawana uwezo wa kuishambulia Iran peke yao bila kupata okey na msaada wa U.S.A, kwani endapo mambo yataenda kombo, basi ajue kwamba atapata support.Tayari habari zimekwishavuja kwamba Israeli inajiandaa kuishambulia nchi ya Iran endapo nchi za USA na UK zitaendelea kusuasua kutoa uamuzi wa kusadia mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo yatalenga vituo vya kutengeneza madini ya Uranium kwenye eneo ya mji wa Qom ambalo lipo karibu na Israeli, ambapo inaaminika kwamba Iran inajishughulisha na utengenezaji wa mabomu ya nyuklia. Nchi ya Iran imekuwa ikisisitiza siku zote kwamba utengenezaji huo wa nguvu za nyuklia umekuwa ni kwa ajili ya kupata nguvu za umeme tu na si vinginevyo.
Hata hivyo shirika la kudhibiti utengenezaji na utumiaji wa nishati hiyo la International Atomic Energy Agency (IAEA) linatarajiwa kutoa taarifa yake ya upembuzi yakinifu kuhusu kituo hicho na ni kwa kiasi gani nchi ya Iran imehifadhi nishati hiyo na hiyo ndio itakuwa ndio kete ya mwisho kusema vita ifanyike au la.
Hata hivyo nchi za USA na UK zimekuwa kwa muda mrefu zikijiandaa kuishambulia nchi ya Irani zikilenga kituo au vituo vyote ambavyo vinaaminika vinajishughulisha na utengenezaji wa silaha za vyuklia na vituo hivyo zimejengwa chini ya ardhi kwenye maeneo kadhaa ya nchi hiyo. Majasusi kutoka katika nchi hizo pamoja na wale wa France na nchi nyingine shiriki kama Italy ambayo mashamabulizi yatakuwa yakitokea katika kisiwa chake cha Sardinia ambako kuna kituo cha kijeshi cha NATO, wamekuwa wakijishughulisha na udondoaji wa taarifa za siri kupitia nvhi za Afghanstani na Irak ambako bado kuna majeshi na vituo vya kijeshi vya nchi za magharibi na USA.
Baraza la mawaziri la Israeli likiongozwa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi Ehud Barack limekuwa likijadili mashambulizi hayo na tayari ndege za kivita zijulikanazo kama F-16 zimekuwa zikifanya mazoezi ya kujiandaa na mashambulizi hayo, ingawa inasemwa kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida.
Pia Israeli imekuwa (kwa kusaidiana na USA) ikifanya mashambulizi kwenye mtandao wa Internet wa Iran kwa kutumia kirusi iitwayo Stuxnet kuharibu mipango mbalimbali ya kutengeneza nguvu za nyuklia ambazo zimehifadhiwa kwenye server mbalimbali nchi humo. Pia tayari wanasayansi mbalimbali wa Iran wamekufa katika mazingira ya kutatanisha.
Mashambulizi ya safari hii sio kwa sababu tu ya ama nchi ya Iran kumiliki silaha za nyuklia au yale ambayo yalifanywa kwa nchi za Afghanstan na Irak au kwa nchi ya Libya ambapo ilisemwa kwamba ilikuwa ni kwa jili ya kulinda maisha ya raia wa Libya, yote ni kwa sabau ya muanguko wa taratibu wa kiuchumi wa USA na baadhi ya nchi za Ulaya na kuendelea kwa utegemezi wa mafuta na pai kutaka kujipanua zaidi kwenye eneo hilo la mashariki ya kati.
Mwisho kabisa kwa kuishambulia Iran nchi ya USA itakuwa ikizuia jitihada zozote zinazofanywa na nchi za China na Russia za kujikita kwenye nchi hiyo ya Iran kwenye maeneo ya nishati ya gesi na mafuta machafu, ni mwishoe kumiliki tena eneo hilo na kuwa koloni la USA lizalishalo mafuta ambayo yatauzwa bei poa na hakutakuwa na vitu kama OPEC.
Nakaribisha hoja.