Israel fingerprints all over 9/11 attacks: US lawmaker

Audio recorning za ndege zilizotekwa zimedhiririsha kuwa magaidi waliteka ndege na kuzigongesha kwenye majengo.
Sasa, hao magaidi walitumwa na Israel ??
 

Attachments

  • 911.jpg
    10.1 KB · Views: 44
Na vipi kuhusu Tower 7? Halikupigwa na ndege wala popo ila lilianguka in the exact manner kama zile twin towers.

Tower 7 iliharibiwa na maporomoko makubwa ya kifusi toka tower 1 (north tower). Katikati ya tower 1 na tower 7 kulikuwa na jengo la wtc 6 lililokuwa na ghorofa 8. Hivyo maporomoko ya vifusi toka tower 1 lililokuwa na ghorofa 100 yalivuka wtc 6 na kulifikia tower 7.
Angalia picha hizi hapa chini:-

Picha ya kwanza inaonyesha maporomoko makubwa ya tower 1 (north tower) yakifunika kabisa eneo lote na kufika na hata kupita kabisa tower 7.
Picha ya pili, angalia jinsi maporomoko ya kifusi yakipiga kwenye tower 7. Baada ya hapo tower 7 likawaka moto.
 

Attachments

  • wtc7.jpg
    18.5 KB · Views: 52
  • WTC7_Smoke.jpg
    51.3 KB · Views: 54
Baada ya shambulio hilo la 9/11 nchi zote za kiarabu kulikuwa na shangwe na vifijo na nderemo kushangilia kufauru kwa shambulio hilo kumbe walitumwa na Israel!!!!! hizi ni habari za kusadikika?????au ni janja ya nyani kula embe bichi??????mimi naona mkajipange upya mlete hoja yenye Mshiko na yenye kutushawishi tuukubali uongo huu.
 
ebu funguka mkuu; leta habari zaidi, sijapata picha kamili.

Kwa walio tenda kitendo cha kinyama na wanajificha ili wajulikane kama ni watu wazuri hapa duniani na wanajifanya wao wanaijua haki za kibinaadamu,basi siku yao itafika na watalipwa na mwenyezimungu.
 
Hukujua halafu povu lilikuwa linakumwagika! MiAfrika bana!!! Kha
Daah! pole sana ndugu lakini sidhani kama kuna comment yangu yoyote ambayo imeonesha maudhui ya mimi kumwaga povu kama unavyodai, itakuwa vizuri kama utai-quote maana nimepitia sijaona yaweza kuwa umeghafirika kidogo!
 
Katika masuala ya Ujasusi siwezi kuwaondoa Waisrael katika hili kwani tukio hili lilikuwa na manufaa kwa katika kupata sababu za kuwakabili wapinzani wao kupitia US bila vikwazo vya UN. Nina imani uhusiano wa US na Israel unafahamika kwa wengi ulivyo.

Katika Uzi uliofungwa wa "US Ambassador to Libya has been killed" post #95 niliandika hivi:


Wasiwasi wangu juu Waisrael kuulazimisha kupigwa maadui zake una elekea kuwa kweli kutoka na maneno aliyosema "Rais wa Kihuni" aliyetokana na "wahuni wa Bengharz" huko Afrika ya Libya wakati ana ongea na NBC News. Soma hapa chini alivyosema.

Foreigners involved in attack on US Consulate in Benghazi - Libyan president


By default: Hao foreigners watakuwa wametumwa na Iran kwa hali ilivyo sasa mashariki ya kati. Na Wamarekani washaingia mtegoni mwa waisrael sasa wanajiandaa kwenda kulinda balozi zao huko mashariki ya kati kwa kupeleka askari wa miguu katika nchi zinazoizunguka IRAN. Soma link hii hapa chini kwa maelezo zaidi.

http://rt.com/news/panetta-troops-deployment-riots-192/


Tusubiri Tuone
 
Habari hii haina ukweli hata kidogo.
1) huyu Bwana Duke si mbunge wa Marekani. Ni mbaguzi rangi aliyekuwa kiongozi wa Ku Klux Klan (shirika katika Marekani inayohubiri chuki dhidi ya watu weusi na wayahudi; leo wako wachache lakini walikuwa muhimu sana huko!)

2) Kwa kipindi kifupi alikuwa mbunge wa jimbo la Lousiana (mnamo 1989/90, kwa njia ya by-election).

3) akiwa mbaguzi rangi anayechukia wayahudi si ajabu ya kwamba anatangaza takataka yoyote kuhusu nchi ya Israeli. Si ajabu ya kwamba shirika la Kiislamu inatangaza haya (ingawa inasikitisha!)

4) akiwa mbaguzi rangi anayedharau watu weusi ni kichekesho ya kwamba takataka zake zinasambazwa hapa JF!

Jamani kwa nini tunaletewa hapa takataka tupu??? Je mtu anayeleta hapa kopi-paste hawezi kuchungulia mwenyewe kma kuna ukweli wowote katika site anapoona habari?????

Kuhusu Bwana Duke soma: David Duke - Wikipedia, the free encyclopedia
Kama hujui Ku Klux Klan: Ku Klux Klan - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Na vipi kuhusu Tower 7? Halikupigwa na ndege wala popo ila lilianguka in the exact manner kama zile twin towers.
Unajua mmiliki nani? Baada ya miaka watatoa taarifa tena (taarifa ambazo si siri tena!)
 
Israel nakumbuka kama alishawaonya USA kuwa kuna ugaidi utatokea ila USA walijifanya kicha ngumu haiwezekani ndani ya ardhi yao.. Waisrael wenyewe hawakuingia ndani ya jengo wakawaacha wamarekani wabishi

Alichonifurahisha Muisrael ni kuwa Ataigeuza iran irejee kama zile zama za Stone AGe Hii kitu inayoitwa EMF ndio itawamaliza
 
Haya na tukubali habari hiyo, lakini je ubomokaji wa jengo ni kweli ni ndege peke yake zilisababisha majengo yale yabomoke kwa adabu za ubomoaji?
hebu ingia hapa kwanza: The 9/11 Collapse
 
Haya na tukubali habari hiyo, lakini je ubomokaji wa jengo ni kweli ni ndege peke yake zilisababisha majengo yale yabomoke kwa adabu za ubomoaji?
hebu ingia hapa kwanza: The 9/11 Collapse

Ndiyo, ubomokaji wa jengo ni kweli ni ndege peke yake zilisababisha majengo yale yabomoke kwa adabu za ubomoaji. Kabisa.
SIpenda kupoteza muda wangu na madai serikali ya Marekani ilibomoa nyumba hizi, wala na madai kuwa picha za kufika kwa Armstrong mwezini zilipigwa Hollywood, wala na hofu ya watu eti King Kong atarudi na kula mabinti mazuri.
 
Kwanza mkuu kabla hatujaona tujiulize ni kipi walichokisahau Iraq kinachowafanya watake kurudi? Na je kilichowaondoa Iraq sicho kitakachowahuta kwa Waajemi? Wanachosahau ni kuwa WAAJEMI SIO WAARABU!! Tabia za WAAJEMI ndizo TABIA ZA WAPASHTUNI na MASINGASINGA!
 
Nimekupa hiyo link pitia kisha tumia ubongo wako kuchambua naogopa sana kusema "MARA NYINGI TUNAKUWA BRAIN WASHED NA MATAIFA YA MAGHARIBI" ndio maana mambo yetu mengi tnataka watuamulie wao.. hii imetufikisha kwenye mrahaba wa 3% bado hatuoni ubaya wa wakoloni ama kweli WANATUPENDA na yote wanayotuambia ni kweli!! Kama vyombo vyao vinaema kweli mbona juzi na jana walizima link za video toka Afghanistan zilizokuwa zikionesha kinachoendelea kwenye ile wanaita Green and blue?
 
..... Kama vyombo vyao vinaema kweli mbona juzi na jana walizima link za video toka Afghanistan zilizokuwa zikionesha kinachoendelea kwenye ile wanaita Green and blue?

Mkuu kuuliza sio ujinga, naomba ufafanuzi hapo juu...
 
Mkuu kuuliza sio ujinga, naomba ufafanuzi hapo juu...
Picha za video zilizokuwa uploaded toka Afghanistan kwenda youtube zote zilizuiliwa kuonesha tukio la kushambuliwa kwa base za USA na NATO.. kwa kifupi pokea taarifa kama walivyozitoa wao, kuwa askari wawili, fighterjets 5 zimeangamizwa na nyingine tatu kuharibiwa! Sasa kama wao wanatoa uhuru wa kujieleza na ndio mfano wetu vipi wanatuzuilia uhuru wa kupashwa habari?
 
Ni kweli huwezi kupoteza muda wako kwa sababu unapokea kitu na kuamini kama ulivyoambiwa na unaempenda! haijalishi ni kitu kipi amekuambia.. Mara zote hapa nasema "TUFIKIRIE KWA KUTUMIA AKILI ZETU NA TUSIPENDE KUSIKILIZA MIOYO INATUAMBIA NINI!!" haya nni maneno machungu na ni kama matusi lakini ndio ukweli wenyewe kwani MARA NYINGI MIOYO HUTUPELEKA KUSIKO KWA SABABU YA MAPENZI YAKE NA KUIBAKA AKILI!

Mimi ni mtu wa LOGIC sasa basi nabomoa hoja zako na uje na hoja za majibu:

1. Kuhusu la Armstrong na wenzake kutua mwezini, kwangu ni mashaka matupu kwa sababu wakati tukio hilo yalifanyika majaribio mengine mpaka mwaka 1972 na kushindwa, na hili lilimletea matatizo rais Kennedy au hili nalo hulijui? Leo hii teknolojia ni bora kuliko mwaka 1969, hivyo basi naamini kabisa spacesuits za miaka hii ni bora zaidi inakuwaje watengeneze ISS kwa gharama kubwa na mwezi uko pale hauhitaji mtaji zaidi ya usafiri? Leo hii ikiwa hapahapa duniani tu deepsea inashindikana mtu kuzamia umbali mrefu bila kuwa ndani ya chombo je vipi mwezini? Ikumbukwe kuwa Warusi walianza kwenda space kabla ya wamarekani na walifanya majaribio kadhaa ya kutembea mwezini kimyakimya toka miaka ya hamsini mpaka mwanzoni mwa miaka ya sitini, na walipoona haiwezekani wakabakiza kufanya tafiti na kutua mwezini kwa kutumia vyombo. na kwa sababu wamarekani walikuwa wanafuatilia uendajiwa space wa warusi wakaona wasijepigwa bao na warusi kwa mafanikio ya mtu kutembea mwezini... hapa ndipo ikafanyika hiyo siasa!! Photoshoping kama inavyoendelea hivi leo.Tazama kwa makini hizi picha kutoka Apollo program - Wikipedia, the free encyclopedia na Apollo 11 Image Gallery kisha TAFAKARI....

Narudia tena tazama kwa makini sana picha hizo na kisha TAFAKARI... zimetoka kwa waheshimiwa wenyewe na sijaweka rasmi picha za wapinzani wa tukio hilo hususan wa Australia ambao wanasema wao walinasa mawimbi ya mawasiliano yanayodaiwa kutumika wakati wa tukio hilo.
2. Holywood inatumika kuaminisha watu au kuogopesha watu.. si chombo cha burudani pekee kama ilivyo bongo movie hapa kwetu.. wenzetu wana malengo.. na ndio maana asilimia 95 ya wamarekani wanajua walishinda vita za vietnam na korea.

Kama unataka kujua technolojia halisi ya marekani tazama Hiroshima na Nagasaki, kisha Afghanistan, Libya na Iraq na ukienda mbali zaidi kisa cha Pwani ya Lulu iliyosababisha kuangamizwa kwa miji ya Japan kina hadithi yake pia!!
 
Ni kweli huwezi kupoteza muda wako kwa sababu unapokea kitu na kuamini kama ulivyoambiwa na unaempenda! haijalishi ni kitu kipi amekuambia..
Mara zote hapa nasema "TUFIKIRIE KWA KUTUMIA AKILI ZETU NA TUSIPENDE KUSIKILIZA MIOYO INATUAMBIA NINI!!"
Mpendwa, asante kwa kunijua kimakini mata moja ingawa tumeanza kujadiliana hapa mara ya kwanza maishani. Ajabu kweli jinsi umejua ni kivipi mimi napokea habari na kuzipenda!
Basi unanijua kuliko mimi mwenyewe??? Hadi sasa sikujua ya kwamba hoja langu juu ya 9-11 lilikuwa jambo la moyo?
Lakini sidhani.
Akili yangu inaridhika maelezo niliyoona; akili yangu imeniambia kweli ni hatari kwa jengo la saruji -feleji kama moto kubwa inawaka ndani yake kwa masaa mengi (jinsi ilivyokuwa huko Tower 7) kwa sababu fizikia inaniambia feleji inapanuka haraka wakati wa joto hivyo inaweza kuvunja saruji . . . . . Ikiwa hii ni tamko pia ya Umoja wa Mamuhandisi wa Ujenzi Marekani naielewa na sioni sababu ya kuwaza ndoto za ajabu.

1. Kuhusu la Armstrong na wenzake kutua mwezini, kwangu ni mashaka matupu kwa sababu wakati tukio hilo yalifanyika majaribio mengine mpaka mwaka 1972 na kushindwa, na hili lilimletea matatizo rais Kennedy au hili nalo hulijui?
Hapana, hii sikujua. Je wewe unajuaje??? Unaongea na malaika wasiofika kwangu? Yaani rais Kennedy aliaga dunia mwaka 1963. Kweli sikujua ya kwamba alihusika na habari za Apollo huko peponi miaka 9 baada ya kifo chake!

(Au: je kuna nadharia ambayo mimi sijui eti Kennedy hakufa bado eti walimwua mwingine aliyefanana naye??? )
 
waislamu mnahangaika nini sasa? Alhaji Osama amesha rest in peace.
 
Ipo siku ukweli utajurikana kuhusu tukio hili 9/11 na dunia mzima itakubaliana na ukweli huo,tuombe mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…