Mama Samia hana political base.
Anatafuta waislamu wa kumpa tafu.
Anageuza taasisi nyingi kuongozwa na wazanzibari au waislamu.
Hii kity Rsis Mwinyi hakuwahi ksbisa kufanya.
Binafsi nitatofautiana kidogo na wewe; hata bila ya kuwa na nia ya kumtetea Samia Suluhu Hassan kwa anayoyafanya sasa.
Hili tatizo la mvutano wa dini tumekuwa nalo miaka yote, hata wakati wa kupigania uhuru, lilikuwepo ingawa halikuwa wazi.
Wale wazee wa Kariakoo, baba na babu zake Mohamed Said ambao amefanya juhudi kubwa sana kuwatengenezea umaarufu wa kupigania uhuru, misingi yao ilikuwa kwenye udini. Lakini kwa vile hawakuwa na kisomo na wala ushawishi/uwezo wa kufanya mipango ya harakati za kutafuta uhuru kwa kupambana na Mwingereza, juhudi zao zikawa ni ngumu na kubidi kutegemea watu wa dini nyingine hata kabla ya Mwalimu Nyerere kushika hatamu.
Hata juhudi za kupigania uhuru zilipokaza, hao wazee walitamani sana kumshawishi Mwalimu Nyerere abadili dini; kwa hiyo wao juhudi zao ziliegemea zaidi kuukuza uislam katika mapambano hayo; na Mwalimu alijuwa nia hiyo, na ndiyo sababu ililazimu ashirikiane na watu kama Rashid Kawawa, na akina Fundikira ambao walijuwa maana ya kuwa uhuru siyo sehemu ya dini.
Ni sababu hizo hizo zilizofanya paundwe na chombo BAKWATA kuepukana na mlengo uliokuwa umejizamisha zaidi kwenye udini badala ya umoja wa kitaifa.
Kwa hiyo, juhudi ziliendelea kufanyika kuzima malalamiko ya hawa ambao udini ndilo lilikuwa jambo muhimu zaidi kwao kuliko muungano wa watu kama taifa; ndiyo maana malalamiko ya waislam kutokuwa na shule za kutosha na bila ya kuwaingiza kwenye mfumio wa pamoja ttaifa lingeendelea kutengana kwa misingi ya kidini.
Viongozi wa kiislam ambao hawakuwa na vigezo vya hata kushika vyeo vya uwaziri, lakini walikuwa ni watu wenye busara, kama Omari Muhaji wakapata kuteuliwa kuwa mawaziri ili kujenga umoja.
Juhudi zote hizo zilizofanywa kitaifa, bado hazikuwa na maana yoyote ya kuzima hicho kikundi cha wenye uislam kupewa umuhimu zaidi kuliko umoja wa kitaifa wetu. Kwa hiyo chokochoko zilikuwepo na ziliendelea wakati wote ila uongozi wa kitaifa uliokuwa imara ulififisha chokochoko hizo. Watu wakaanza kufikiri mambo yta udini na ukabila tumeyamaliza Tanzania; hadi walipoingia akina Kikwete walioanza kuupalilia utengano wetu kwa misingi za kidini na mingineyo.
Ni Kikwete ndiye aliyetoa tuzo ya heshima kwa hao wazee wa Kariakoo.
Sasa wakati huu tunapozungumzia CCM kutekwa na uislam, ni wazi kabisa kutekwa huko kunatokea wapi.
BAKWATA kwa vile ni sehemu ya CCM, hawa wenye ajenda yao wakaona waingirie huko, kupitia BAKWATA. Badala ya kushindana na BAKWATA wakiwa nje, ikawa rahisi kuitumia wakiwa ndani. Kwa hiyo, hiyo ndiyo imekuwa barabara ya kuingilia CCM na kuiteka.
Samia ametumia mwanya huo, kwa sababu hana njia nyingine yoyote ya ushawishi kupata kundi la kumuunga mkono.