Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
KUNDI la wapiganaji la ISIS limemuua kwa kumkata kichwa kijana mmoja baada ya kumkuta akisikiliza muziki wa Pop unaoimbwa na wasanii wa Marekani akiwa kwenye baa ya baba yake.
Kijana huyo, Ayham Hussein (15) alikamatwa mjini Mosul, Iraq baada ya wapiganaji waliokuwa kwenye doria kumsikia akisikiliza muziki huo.
Mauaji hayo yalifanyika nje ya msikiti baada ya Hussein kutiwa hatiani na mwili wake umekabidhiwa kwa wazazi wake kwa taratibu za mazishi.
Mbali na kuuawa Hussein, vijana wengine wawili nao wameuawa kwa kupigwa risasi nje ya msikiti kwa kutohudhuria Swala ya Ijumaa.
ISIS walipiga marufuku miziki ya nchi za magharibi kupigwa kwenye maeneo yao huku sababu kuu ikitajwa kuwa miziki hiyo ni chanzo cha vitendo viovu, majaribu pamoja na kumfanya mtu kushindwa kujifunza Koran hivyo kumsahau Mungu.