Isikie kamati ya roho mbaya..

Isikie kamati ya roho mbaya..

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2018
Posts
276
Reaction score
1,428
Kamati ya Roho mbaya inauliza kwanini wazungu wakitunyima misaada wanaitwa Mabeberu, wanyonyaji na wezi wa rasilimali zetu wakati huo huo wakitupa msaada wanaitwa wahisani na watu wenye kuitakia mema nchi yetu?

Kamati ya Roho mbaya inahoji kwanini tunajifunga kwenye mikataba ya kimataifa ambayo tunaamini hatutaki kutekeleza? Kwann tusisimame Kama Taifa huru lenye uwezo wa kujiamulia mambo yake?

Kamati ya Roho mbaya inauliza kwanini tusijifunze kusema NO na tuache kubadilika Kama kinyonga Leo huyu tunamwita mzuri kesho tunamwita mbaya keshokutwa mzuri mtondogooo mbaya.....
 
Cc ni masikini....ujue masikini hanaga msimamo.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Sisi ni bendera.....upepo unavuma kuelekea kila upande.
 
Rais ajae Atakuwa na Kazi kubwa sana kuirudisha nchi kwenye mstari huyu kainyosha hadi imepinda na kukatika kabisa,ajae ana Kazi kubwa sana ya kulipa madeni kupunguza deni la taifa,kuinua uchumi mfu, kurejesha tija na morali ya Kazi kwa Watumishi, kuwasukuma ndani wasiojulikana, kujenga demokrasia, kuvutia na kushawishi wawekezaji, kurejesha diplomasia ya kimataifa, kupunguza ttzo la ajira,kuimarisha shillings yetu, kuujenga upya umoja wa kitaifa,kurejesha imani ya vyombo vya dola kwa wananchi, kufukua makaburi yote na kuwasukuma ndani wote waluotumia vibaya Madaraka, vibaya kodi zetu,kukaa kimya juu ya upotevu wa watu,kuinua elimu,kurejesha mifumo ya haki ya kodi, kuifufua Bandari iwe bize kama zamani,nk.Kazi ni kubwa si ya kitoto.Ajae awe na nyota ya Pesa na mwenye BARAKA kila kitu kitakuwa sawa.
 
Kamati Ya Roho Mbaya (KRM) inapaswa itafakari CHAMA gani kilicho tufikisha hapa tulipo (Miaka 57 sasa), kutokana na viongozi wake;

1) Wenye maamuzi ya ajabu na kukurupuka???

2) Wanao wapa wawekezaji mikataba mibovu??? (Bungeni na Wizarani)

3) Wanaopitisha SHERIA kandamizi na za ajabu bungeni??? (Kama sheria ya makato 75% kwa wastaafu)

4) Wanao ingia mikataba kwa niaba ya nchi halafu wanakuja kukaa kimya??? (Wizara Husika)

5) Kutumia nguvu na jeshi kisiasa???

Hao ndio MAADUI wakubwa kuliko NJAA na UMASIKINI.[emoji18]

Nawasilisha hoja,
 
Kamati ya roho mbaya pia tunauliza fedha anazotoa rahisi bila bunge kuhidhinisha matumizi ya hzo fedha je huwa zinatoka mfukoni mwake au........
 
Huyu jamaa akiendelea na hata mambo yake ya ropo ropo na wazungu kuna kipindi tutahitaji kuchapa noti zetu mpya na makampuni yao yakatugomea teh. {Jokes}
 
As a nation we have permanent interest but not permanent friends. And so are other nations as well!
 
Back
Top Bottom