Isidingo yarekodi sehemu ya mwisho ya tamthiliya hiyo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Kwa wale wapenzi wa Tamthiliya ya Isidingo inaelezwa kuwa Waigizaji wa tamthiliya hiyo walikuwa location wakifanya (wakishoot) sehemu ya mwisho (episode) ya tamthiliya hiyo. Tamthiliyo hiyo ni miongoni mwa tamthiliya ndefu sana iliyodumu na kuoneshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni kwa takribani miaka 21.

Kwa nchi ya Tanzania Tamthiliya hiyo ilirushwa kupitia kituo cha ITV sik mbalimbali za wiki.

Aidha, imeelezwa kuwa sehemu hiyo ya mwisho iliyorekodiwa inatarajiwa kuoneshwa mpaka Machi mwaka huu mpaka kufikia tamati ya episode hiyo.

Isidingo kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Twitter wamethibitisha kuwa wiki iliyoisha walikuwa wakirekodi sehemu ya mwisho ya mchezo huo.

"wiki iliyopita tulirekodi sehemu ya mwisho kabisa ya mchezo wetu. Tumebarikiwa na tunajivunia kukaribishwa majumbani kwenu kwa miaka 21. Tunashukuru kwa kukua nasi na kuturuhusu kukusimulia hadithi yako". Walisema

====
Last week we shot our last Isidingo episode ever. We have been blessed and proud to have been welcomed into your homes for the past 21 years. Thank you for growing with us and allowing us to tell YOUR stories. Tune in as we bid you farewell on the 12th March 2020. #Isidingo

1580478013572.png
 
Nakumbuka itv walianza kuirusha baada ya tamthilia ya Egoli na acapuco 1999
Yenyewe ilikuwa inajitegemea, Egoli na Acapuco bay ilikuwa mida ya saa 4 usiku kabla ya kuja ile tamthilia iliyovuta watu ya La mujer de mi vida ya Barbarita na Antonio Dolfo
 
Back
Top Bottom