IShowSpeed asitisha Tour yake Nchini Namibia

IShowSpeed asitisha Tour yake Nchini Namibia

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Nyota wa YouTube kutoka Marekani, IShowSpeed, amefutia ratiba ya ziara yake nchini Namibia kama sehemu ya safari yake ya “Speed Does Africa”, baada ya mamlaka za anga kushindwa kutoa vibali vinavyohitajika kwa wakati, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Namibia.

Ziara iliyopangwa kufanyika Namibia, ambayo ilitarajiwa kuwa kituo cha pili katika ziara ya siku 28 barani Afrika ya mtiririshaji huyo, ilifutwa baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Namibia (NCAA) kuthibitisha kuwa haikuweza kushughulikia nyaraka zinazohitajika kwa ndege binafsi (Private Jet) iliyosajiliwa nje ya nchi kutua nchini humo. IShowSpeed anazunguka barani Afrika katika ziara yake kwa kutumia Private Jet.

Kwa mujibu wa NCAA, maombi ya kibali cha mwendeshaji (Rubani) wa kigeni yaliwasilishwa chini ya saa 11 kabla ya muda uliopangwa wa kuwasili, muda ambao haukutosha kabisa kukamilisha mchakato wa kawaida wa mapitio na uidhinishaji wa vibali.

Katika taarifa yake, msemaji wa NCAA, Nelson Ashipala, alisema kuwa taratibu za kimataifa za usafiri wa anga huhusisha uratibu wa shughuli mbalimbali za wadau wengi na wa kawaida ambazo huhitaji hadi siku 14 kupata idhini kamili. Kutokana na taarifa ya muda mfupi na nyaraka zisizokamilika, kibali hakikuweza kutolewa, jambo lililowalazimu waandaaji wa ziara ya "Speed Does Africa" kufuta ziara hiyo.

NCAA pia ilibainisha kuwa hakuna maombi yaliyowasilishwa kwa ajili ya matumizi ya ndege zisizo na rubani (drones), ambazo zilitarajiwa kuwa sehemu ya maudhui ya matangazo ya moja kwa moja (Live Streaming) ya IShowSpeed nchini Namibia.

Bila vibali vinavyohitajika kwa matumizi ya drones—ambavyo nchini Namibia lazima yaombwe mapema—ndege hizo hazikuweza kuruhusiwa.

Kufutwa kwa ziara hiyo kumevunjia moyo mashabiki wa eneo hilo huko nchina namibia, huku baadhi ya wachambuzi wakisema fursa hiyo iliyokosekana imeondoa nafasi ya kupata utangazaji wa kimataifa kwa utalii na utamaduni wa Namibia.

Waandaaji wa ziara ya IShowSpeed bado hawajathibitisha kama kutakuwa na ratiba mpya ya kutembelea Namibia baadaye.

Hata hivyo, ziara ya “Speed Does Africa” inaendelea katika nchi nyingine barani Afrika, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zilizopigwa chini katika Tour hiyo. Na katika ukanda huu wa majirani zetu IShowSpeed atatembelea majirani zetu wote (Mozambique, Zambia, Rwanda, and Kenya) ispokuwa Malawi, DRC Congo, Burundi na Uganda.
 
Labda angepenyeza kitu kidogo!! Siku 14 zote hizo kibali tu.

Yaleyale ya TANESCO miezi mtu unasubiria kuunganishwa umeme!
 
Hapa ndipo tunaposhindwana na Africa mambo mengi yanaenda kishamba
Swala lilikuwa kukagua ndege yake na kutoa kibali hayo mengine ni ushamba mtupu
 
Hapa ndipo tunaposhindwana na Africa mambo mengi yanaenda kishamba
Swala lilikuwa kukagua ndege yake na kutoa kibali hayo mengine ni ushamba mtupu
Shida hata siyo ndege ni drone zake za kurekodia.

Wamekosa revenue za utalii kwa mabilioni kisa kajitu kamoja
 
Shida hata siyo ndege ni drone zake za kurekodia.

Wamekosa revenue za utalii kwa mabilioni kisa kajitu kamoja
Issue kama ni pesa wangemwambia alipe yaani kwamba fanya lolote sisi tunataka pesa
Kama unataka drones basi utalipa kiasi flan cha kufidia huo utalii wanaohisi utapotea achague yeye kama atalipa au ataacha
 
Issue kama ni pesa wangemwambia alipe yaani kwamba fanya lolote sisi tunataka pesa
Kama unataka drones basi utalipa kiasi flan cha kufidia huo utalii wanaohisi utapotea achague yeye kama atalipa au ataacha
Kabisa
 
Mitano tena wako wapi watusaidie kupiga makofi.Mabeberu wanataka kuja kutuchunguza kisirisiri wanatuonea wivu tuna maendeleo makubwa kuwazidi 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom