Ishini nao kwa akili

Ishini nao kwa akili

KUISHI NA MWANAMKE KWA AKILI..........................
Kabla ya dhambi wote walikua sawa yaani Adamu na Hawa, shetani kwa umbo la nyoka alimdanganya Hawa akamchumia tunda lililokatazwa kuliwa na Hawa akala baada ya kuona hata nyoka amekula lile tunda lakini hakufa. Baada ya kudanganywa na nyoka, Hawa akawa na tamaa ya kutawaliwa maana alionesha udhaifu na kudanganywa hvyo ule usawa ukatoweka kati ya mwanamke na mwanamume.

Hawa nae akampelekea Adamu tunda ili ale, hapo ndipo Hawa alipofanikiwa kudrive akili za Adamu ili Adamu naye akubali kutenda dhambi, naye akala lile tunda.

Lakini Mungu akamrudishia Adamu uwezo wa kumtawala Hawa kiroho, na sio kimwil maana kimwili Adamu alishamruhusu Hawa kumtawala kwa kumshawishi naye kula tunda lile. Kimwili mwanaume hawezi kumtawala mwanamke hata siku moja, lakini kiroho, mwanaume aweza kumtawala mwanamke.

Ok, turudi kwa mada:
Tunapozungumzia Akili inahusianishwa na roho. Maana siku zote mwanadamu akitumia akili bas mwili hauwezi kumuendesha. Hvyo bas, kuishi na mwanamke kwa akili sio kuwa mjanjamjanja, ni kuruhusu Roho ifanye kazi, na roho inahusianishwa sana na Mungu/ mambo ya kiroho. Ukiwa mtu wa kiroho, na kuongozwa na Mungu, hutashindana na mwanamke. UTAMTAWALA.

Sasa bas, tambua kwamba mwanamke ana uwezo mkubwa sana wa kumshawishi mwanaume hata akafanya jambo ambalo asingelifanya kama angetumia akili/ Roho.

KUISHI NA MWANAMKE KWA AKILI, unatakiwa uchuje kile anachokwambia kwa akili/ kwa kiroho zaidi ili usiingizwe sehem ambayo hukuitaka na hukupenda kuwa.

Usishindane na mwanamke wakati umepewa mamlaka ya kumtawala. Mwanaume ukijua ulimwengu wako ( kimajukumu ktk familia) na mwanamke akijua ulimwengu wake (kimajukumu ktk familia), hakuna kitakachoharibika.

Mwanaume kimajukumu anatakiwa ampende mwanamke, na mwanamke amtii mwanaume. Ktk kupenda, kuna mengi sana, ukimpenda; hutampiga
Hutamdharau,
Utamthamini,
Utamjali,
Hutachepuka na kumwacha ndani mkeo,
Utamlinda nk..................
Na ukifanya haya kwa mwanamke automatically atakutii. Hakuna mwanamke atakuwa na kiburi mbele ya mume wake mpenzi anayempenda.

NB: Ndoa ni takatifu na ni taasisi ya kiroho, lakini tunakosea tunapotaka kuipeleka kibinadamu. Na ukiipeleka hvo bas jiandae kuumia siku zote.

Mbarikiwe na Bwana.
 
Wanawake Pasua kichwa sana,kuishi nao kwa akili yataka moyo zaidi mana wana madhaifu yasiyohesabika.
 
Nyie ni viumbe hatari sana.... Huwa siwamalizi nikiwatizama.. Mpaka sasa tumeamua kumuachia Mungu na kamsemo ketu "MUNGU ANAWAONA"
Kweli aisee hawa watu siyo na ndomaana wakinipa papuchi nawachupua ile mbaya
 
Ndoa ni taasisi ambayo ustawi wake na kuimarika kwake kunategemea na wanaounda taasisi hiyo........nguzo kuu zinazoimarisha taasisi hiyo ni UVUMILIVU,KUHESHIMIANA na KUSAMEHEANA......kila panapotokea mtafaruku.......


UVUMILIVU kwa kuwa tumekutanishwa kimwili huku kila mmoja akiwa na tabia yake....kwa lazima kuna mambo mtakuwa mnapingana kimitazamo..... hiyo ili mambo yaende ni lazima mvumiliane....

KUHESHIMIANA.....kwa kuwa heshima ndicho kinachowaweka watu pamoja kwa kuwa penye heshima ni kwamba kila mmoja anatambua mipaka yake.....

KUSAMEHEANA....kwa kuwa hakuna mkamilifu kati yenu...kwa hiyo kukoseana ni sehemu ya maisha lakini maisha hayawezi kuenda kama hamtosameheana....


Kuishi na mwanamke kwa akili kwanza kunatakiwa utambue mwanamke ni kiumbe wa aina gani....na anahitaji nini ili kuendelea kuwa karibu yake na kufaidi pendo lake.......
Kila mmoja wetu anajisikia raha na burudani...anapojua kuwa kuna mtu pembeni yake anayemjali na kumpenda kwa dhati.....lazima mtu huyo atajiona wa kipekee ulimwenguni.....na huko hakutokani na maneno mengi bali kwa matendo ya kuonesha kuwa kweli unampenda na kumjali......
Na hicho ndicho kitu pekee wanacho kikosa wanawake wa leo kutoka kwa wanaume.......wanaume wengi upendo wao kwa wake zao umebaki midomoni na sio kwenye vitendo.......hapa nadhani wakubwa wameshanielewa....

Akili zilizo maanishwa hapa sio zile za kiwango cha juu cha elimu....bali ni akili za kiwango cha juu cha utambuzi wa mwanamke kuwa anahitaji nini na kwa wakati gani.......!!??

Ukishayatambua hayo kamwe hutakaa ugombane na mkeo...au mpenzi wako......kwani kutambua mtu anataka nini na kwa wakati gani kutafanya wewe ufanye mambo kwa usahihi na kwa wakati muafaka......ni kama vile kumpa maji mwenye kiu.....au kumpa chakula mtu mwenye....lazima atakithamini ulichompa kwa kuwa umempa kwa waakati sahihi......

Ndio maana tukaambiwa tuishi nao kwa akili......na hizo ndizo akili zenyewe.....

Nawasilisha.....
 
KUISHI NA MWANAMKE KWA AKILI..........................
Kabla ya dhambi wote walikua sawa yaani Adamu na Hawa, shetani kwa umbo la nyoka alimdanganya Hawa akamchumia tunda lililokatazwa kuliwa na Hawa akala baada ya kuona hata nyoka amekula lile tunda lakini hakufa. Baada ya kudanganywa na nyoka, Hawa akawa na tamaa ya kutawaliwa maana alionesha udhaifu na kudanganywa hvyo ule usawa ukatoweka kati ya mwanamke na mwanamume.

Hawa nae akampelekea Adamu tunda ili ale, hapo ndipo Hawa alipofanikiwa kudrive akili za Adamu ili Adamu naye akubali kutenda dhambi, naye akala lile tunda.

Lakini Mungu akamrudishia Adamu uwezo wa kumtawala Hawa kiroho, na sio kimwil maana kimwili Adamu alishamruhusu Hawa kumtawala kwa kumshawishi naye kula tunda lile. Kimwili mwanaume hawezi kumtawala mwanamke hata siku moja, lakini kiroho, mwanaume aweza kumtawala mwanamke.

Ok, turudi kwa mada:
Tunapozungumzia Akili inahusianishwa na roho. Maana siku zote mwanadamu akitumia akili bas mwili hauwezi kumuendesha. Hvyo bas, kuishi na mwanamke kwa akili sio kuwa mjanjamjanja, ni kuruhusu Roho ifanye kazi, na roho inahusianishwa sana na Mungu/ mambo ya kiroho. Ukiwa mtu wa kiroho, na kuongozwa na Mungu, hutashindana na mwanamke. UTAMTAWALA.

Sasa bas, tambua kwamba mwanamke ana uwezo mkubwa sana wa kumshawishi mwanaume hata akafanya jambo ambalo asingelifanya kama angetumia akili/ Roho.

KUISHI NA MWANAMKE KWA AKILI, unatakiwa uchuje kile anachokwambia kwa akili/ kwa kiroho zaidi ili usiingizwe sehem ambayo hukuitaka na hukupenda kuwa.

Usishindane na mwanamke wakati umepewa mamlaka ya kumtawala. Mwanaume ukijua ulimwengu wako ( kimajukumu ktk familia) na mwanamke akijua ulimwengu wake (kimajukumu ktk familia), hakuna kitakachoharibika.

Mwanaume kimajukumu anatakiwa ampende mwanamke, na mwanamke amtii mwanaume. Ktk kupenda, kuna mengi sana, ukimpenda; hutampiga
Hutamdharau,
Utamthamini,
Utamjali,
Hutachepuka na kumwacha ndani mkeo,
Utamlinda nk..................
Na ukifanya haya kwa mwanamke automatically atakutii. Hakuna mwanamke atakuwa na kiburi mbele ya mume wake mpenzi anayempenda.

NB: Ndoa ni takatifu na ni taasisi ya kiroho, lakini tunakosea tunapotaka kuipeleka kibinadamu. Na ukiipeleka hvo bas jiandae kuumia siku zote.

Mbarikiwe na Bwana.
ADAM, kwa HAWA. LUTHU kwa MKEWE. SAMSON kwa DELILA. AYOUB kwa mkewe walipungukiwa nini ktk sifa ulizoorodhesha hapo hata yakatokea hayo. 2 Kwamba ukifanya hayo atakutii unaamini wanawake wote NI wema
 
Back
Top Bottom