Reuben Challe
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 2,761
- 5,049
Huwa sipendi kulitumia kwa sababu naona kama ni offensive word ila kwa teknolojia ilipofikisha wateja wake acha tu hili neno litumike
Nadhani wote mnaijua kampuni kubwa ya Kimarekani ya Apple ambayo inatengeneza product zenye ubora wa hali ya juu sana. Kampuni hii katika kila league ambayo anaingia lazima awe on the top, kuanzia kwenye simu, laptop, tablet, wireless ear buds, VR headsets na maeneo mengine mengi. Si ajabu hata leo hii Apple angesema atengeneze magari ya umeme, still angekuwa among the top brands tena kundi moja na Tesla au BYD.
Products zao ni very high quality na kwa mtu anayejua nini anataka, Apple products are user friendly
Shida inakuja kwa wateja wake, hata kama Apple ana high quality products ila si kila anayenunua Apple products basi ameshawishika na quality. Wengi wao wanafanya show off tu na wengine hata Apple atengeneze mavi then aweke logo ya Apple utawasikia wanasema "Wow.... this is so innovative". Hawa ndio wanakesha mitandaoni kutukana simu zote za Android na kutoa kila kauli chafu kwa simu ambazo si iPhone. Ukimuuliza nini unachokipenda kwenye iPhone atakuambia security, ukimwambia aelezee hiyo security inavyomsaidia anabaki anang'aa macho. Hawa ndio wanaamini kutumia Android ni umasikini, wapenzi wa macho matatu. Unakuta mtu matumizi yake ni kupiga picha, kutuma message, kuchat WhatsApp, kupiga na kupokea then anasema iPhone iko smooth kuliko Android kwa sababu anaitumia kila siku na haijawahi kumletea shida. Kwa haya matumizi hata Redmi Note 10 inaweza fanya bila shida yoyote. Watu kama hawa ndio tunawaita iSheep
iSheep wanapenda kuponda simu za Android bila fact za msingi na ni wagumu kutetea hoja zao, zaidi wanaleta matusi na kejeli tu.
Hawa ndio vinara wa ku support mambo ya kijinga ambayo Apple anafanya. Kwa mfano tabia ya kutengeneza simu ambazo design zinafanana fanana tu miaka mitano mfululizo. iSheep utawasikia wakisema hamna haja ya kubadili mwonekano sana, huu mwonekano ndio unaipa simu recognition kuwa ni simu ya Apple. Wanasahau mwonekano mmoja kila mwaka unafanya simu i-feel outdated.
Kwa iSheep kila teknolojia mpya kwao sio innovation mpaka siku ambayo Apple atakuja kuitumia, then utasikia sifa tele kwa Apple
Ni kama tu iSheep walivyokuwa wanasema wireless charging sio kitu cha muhimu kwa sababu wanaweza kuchaji simu zao kwa waya na zinajaa vizuri tu, mpaka ilipofika 2017 ndio Apple wanaleta wireless charging na kila mtu akaanza kumwaga sifa tele kuwa Apple ni innovative. Wireless charging, Samsung alikuwa nayo tangu 2012 huko.
Sasahivi kuna teknolojia ya Fast Charging (hapa namaanisha zile za chini ya saa 1 simu imejaa chaji) iSheep watakuambia Fast charging inaharibu betri, kwa sababu tu Apple hawana hiyo technology. Siku itakapokuja iPhone yenye fast charging ya hata dakika 45, kila kona ya forum za tech utakuta watu wanavyomwaga sifa kwa teknolojia mpya ya Fast charging ya Apple.
iSheep wanaamini kuwa simu za Android ndio zinakumbwa na matatizo mengi ya hardware kwa sababu ni simu za kimasikini. Haya, safari hii tumeona iPhone 15 Pro Max ziki overheat na kupata shida mbalimbali kama screen failures. Sasa sijui ni iPhone zipi hizo ambazo hazipati matatizo
Au wanasema Android zina bugs nyingi kwenye software. Kiuhalisia kila simu ina bugs, hata hizo iPhone zinakumbwa na bugs mara nyingi tu. Kama jinsi simu za Android zinavyopata App crash zitakuambia "Unfortunately the app has stopped", na kwenye iPhone inatokea ila haitakuonesha hayo maneno ila ukifungua app hapohapo inajifunga. Haya, screenshot nyingine hii hapa, hii ni notification bug kwenye iOS. Na hakuna watu wanaojua kupuuzia bugs kama watumiaji wa iOS. Wao wakiona bugs wana assume macho yao ndio yamekosea ila iPhones are always right. Lol
Kila kitu ambacho Apple anafanya iSheep hu support tu na hudhani bidhaa za Apple ndio bidhaa bora kuliko zote duniani.
Mfano kwenye simu iSheep hukimbilia kusema iPhone ndio zinaongoza kwa mauzo dunia nzima. Wanasahau kwamba Sisi Android users tuna choice nyingi nyingi Kwa hiyo tunajigawa, wengine wataenda kwa Samsung, wengine Xiaomi, Oppo, Vivo, Google Pixel, etc
Kitu kingine ambacho kinanikera ni kwamba Apple anaendelea kulimit basic specifications za simu bila sababu yoyote ya msingi mfano iPhone 15 bado ina Refresh rate ya 60Hz, wakati midrange kibao za Android zina 120Hz refresh rate. Cha ajabu iSheeps nao wanaona hii ni sawa tu kwa simu expensive kuwa na 60Hz refresh rate, sawa na low end phones
Products za Apple ni high quality ila zina limitations za ajabu na wanachelewa sana kuleta features kwenye products zao
Kampuni ya Apple ndio imesababisha leo hata Samsung na Xiaomi wameondoa 3.5mm jack na SD card slot kwenye flagship zao.
Ila hakuna iSheep ambao wanakera kubishana nao kama wanaosema "Hata mimi nilikuwa napenda Android kama wewe ila sasahivi nimehamia iPhone aisee yani sitamani kurudi Android tena". Hawa wengi wao wametoka kutumia Android za laki 2, wakajichanga wakanunua iPhone 13 Pro Max then wanaanza ku compare. Unakuta anatupia lawama nyingi kwa Android kumbe ni matatizo ya Pop 2 yake aliyokuwa anaitumia kabla ya kununua iPhone 13.
Leo nimeamua kuongelea iSheep kutokana na tabia yao ya kudhani kuwa iPhone ndio simu bora zaidi duniani na hivyo kuponda kampuni za Android kwa dharau na kejeli
If I'm being honest tukiachana na brand recognition sikuhizi hata Chinese phones ni more innovative kuliko Apple.
Oppo Find X7 Ultra, Samsung Galaxy S24 Ultra na Xiaomi 14 Ultra ni product bora kuliko iPhone 15 Pro Max. Najua iSheep hawatoelewa kwa sababu wao wakisikia tu simu ni ya Android basi wanapuuza features zote za humo ndani. Hawataki kabisa kusikia.
Kingine nimekuja kugundua kukosa kwa features kwenye iPhone kunawagusa sana Android users ila iPhone users hata hawajali, wawe nazo wasiwe nazo kwao ni sawa tu.
Hii ni kwa sababu Apple imeshawajengea mindset mbovu vichwani mwao. iSheep wapo tayari teknolojia zote mpya ziwapite na hata hawajali. Watazitumia ikiwa Apple atazileta la sivyo wanazitupilia mbali