Ishara ya Kuingia mjini

Ishara ya Kuingia mjini

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,280
Ni saa za alasiri, jua linaanza kuzama na kagiza kanaanza kutanda. Dereva na abiria wake mmoja wako kwenye barabara inayoelekea mji mmoja. Mara abiria anasikia mlio wa bung! bung! ukitokea nje ya gari. Ikafika mahali milio ikawa mingi. Abiria akaona heri amwulize dereva ni nini hicho kinatoa mlio wa bung! kila mara:
ABIRIA: Hiyo bung bung ninayosikia ni nini?
DEREVA: Hiyo bung manaake tumeshaingia mjini.
ABIRIA:Yaani tukiingia mjini ndo mliio ya bung bung itokee? Kwa nini?
DEREVA: Ni watu hao nawagonga!
 
mmmh!huyo dereva kabila gani?maana kuna makabila mengine kuuwa ni sehemu ya maisha!!
 
mmmh!huyo dereva kabila gani?maana kuna makabila mengine kuuwa ni sehemu ya maisha!!

Ni kinyume. Kuna makabila wanapenda kugongwa na gari.Stori hii chanzo chake ni Ethiopia.Wenyeji wa huko, Wahabeshi, wanapenda kugongwa na gari zuri,na jipya kiasi kwamba utawasikia wakitambiana:
MMOJA:Unajua kwa nini huu mguu wangu mevunjika? Mwezi jana bwana. Ikapita pijio moja modeli ya kisasa, rangi moto, nami huyoo, nikajitupa.Ikanitengeneza hvi.
MWENZAKE: Hivyo vitroli vya kifaransa ndo wathubutu kusema! Waona hili kovu kwenye paji la uso?. Kazi ya mjerumani aisee! Benz hilo babu weee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom