Ishara 10 za manabii na mitume feki waliotapakaa Tanzania

Kubali kujirekebisha mtu wa Mungu, kwani unapungukiwa na nini. Achana na ubishi usio wa lazima. Hayo mambo aliyoainisha ni kweli tupu,ndivyo mnavyofanya,je? Kwa utashi wako unadhani mambo hayo yanampendeza Mungu?.
Nataka unifunulie huo ukweli. Mimi sio mbishi... Funua ukweli ili huo ukweli utuweke huru... Who is authentic then !!!
 
Kajaribu kuwahubiria . Kuna wachawi wangapi uliwahubiria wakaokoka na kuna manabii wangapi uliwahubiria wakagoma ?
wachawi wengi wameokoka kuliko hao wanao jiita manabii,

Yesu alikuja kutuponya na si kukanyagisha watu mafuta, hiyo ni ibada ya sanamu na kafara.

huyu hapa nabii wako :

Alikuwa Shoga, sijui kama ameacha
 
Ndani ya mkoa mmoja unawakuta manabii/mitume zaidi ya 5+, wakati maandiko yanasema nabii akizaliwa ujue nabii aliyekuwa akihudumu eneo hilo hana kitambo kirefu. Na nabii siyo kama machungwa kila mkoa unayo

Dah nimecheka sana mkuu
 
Wanaongoza kwa ushirikina we nimeona kuna gazeti limeandika eti kuna nabii anauza chupi za kike kwa wanawake hivi hapo kuna usalama?
Bora mchawi ana huruma, mkeo akikwambia anakwenda kwa hawa manabii na mitume, kama ni issue ya ndoa lazma aliwe mzigo ndio ahudumiwe;
Hawa jamaa ni matapeli wamejificha kwenye kivuli cha udini.
 
Ni sawa... Tumepewa akili tupime hizo nabii... Lakini kuhukumu sio kazi yetu. Ukiona mafundisho yake hayakufai kaa pembeni. Kuna mwingine kwa mafundisho hayo dhaifu atapata hapo neno litakalomgeuza na kumnusuru na jehenamu !!!
Sawa
 
Unabidii utume utoke wapi nyie jamani dah wakristo mna kazi kweli
 
Noma
Screenshot_20210131-120217_WhatsApp.jpg
 
Hivyo vyeo vya unabii wanapewa na nani alafu wamewateka sana wanawake yaani nabii ana walinzi
 
Waacheni,kila mtu afate anachoamini.
Ata ambao awajiiti manabii na mitume pia wapo waongo na wazushi.
 
Unabii juu ya dunia ulishafungwa, kinachosubiriwa ni mwisho wa dunia sasa hawa jamaa ni unabii gani hasa wanaotoa. Halafu qualification ya kuwa mtume ni kupeleka injili kule ambako haijafika kama alivyofanya mtume Paulo kule Rumi na Asia na namna lilivyofanya kanisa katoliki kupeleka injili karibu dunia nzima. Sasa mtu anajiita mtume wakati yuko hapa hapa bunju ambapo watu wote walishasikia mafundisho ya injili....
 
1. Wapo tayari kuungana katika kutetea kazi za usanii wanaoufanya ndani ya majengo ya makanisa. Lakini hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kutawalika kwa mwingine! Kila mmoja anataka amtawale mwenzake.

2. Huwa wanafanya kazi zao kwa muundoo wa ku-copy & paste. Mfano wakiona kuna Nabii mwenzao ametoa Mapepo kwa kupuliza Upepo Mic na wengine watafanya hayo hayo!

3. Hawafanyi kazi ya Unabii bila Pesa Mkononi. Mhitaji akienda Awe na Pesa ya kumuona Nabii, Awe na Pesa ya kwenda Kusafishiwa Nyota, Pesa ya kutabiria! Unabii wao ni kwa ajili Maisha ya watu tu. Hawana Unabii kwa Taifa wala Ulimwengu kwa ujumla.

4. Ni waoga wa kufa kuliko raia (watu) wanaowahudumia. Imefikia wakati hata Ulinzi wa Nguvu za Mungu hawauamini! Wamekuwa na Walinzi wa Kimwili zaidi. Huwa wana VITISHO sana kwa watu wanaowakosoa kiutendani! Wapo tayari Kushambulia kwa maneno au kushambulia kwa Vitendo, Kupiga mtu, Kutishia watu maisha na hata kutoa kauli za kumuua mtu!

5. Wananena kwa Lugha kwa staili ya maneno yale yale ya KUKARIRI yasiyozidi Kumi (10), yaani Lugha yetu wanayonena haipanuki kimaneno, maneno ni yale yale yaliyopo Dsm, Mwanza, Dodona na Morogoro, hayazidi zaid ya hapo! Na hawajui maana ya yale maneno wanayotamka!

6. Wanaongoza KUSENGENYANA wao kwa wao, lakini wakikutana pamoja ni kama wana Umoja wa Kazi ya Mungu na kumbe ndani yao ipo shida kubwa! Wanapenda Sifa sana, Kusifiwa, Kunyenyekewa na Kuabudiwa kuliko hata Mungu mwenyeqe. Hupenda kila wanalolifanya waonekane na watu! Hata akimsaidia mtu msaada wa nauli ya daladala ya Tshs 1,000/= wanataka Wamchukue picha (Selfee). Wakienda huko Maporini (Mlimani) kwa ajili ya kile wanachokiita Maombi ya Mlimani ndiyo usiseme! Hakuna maombi huko ni Vurudu za picha na Clip za shot Video. Hakuna Mungu huko zaidi ya maingizo ya maombi!

7. Wanapenda kunyang'anyana Waumini ndani ya majengo ya Ibada na hasa pale wanapoalikana Kihuduma. Wanapotoka hapo walipoalikwa kuhudumu huchukua namba za simu za Waumini wa eneo husika ili kuwahamisha na hasa wale wenye kuonekana wana Kipato kifedha! Hupenda sifa zaidi hata Waandishi na Mafarisayo kuwawafikii Mitume na Manabii wa zama hizi kwa sifa. Hupenda mashindano ya kuvaa Masuti ya gharama, Hushindana kula vyakula ya bei mbaya na bila kujua hapo mtaani kwake anapohudumu kuna watu ni Maskini wa kutubwa na wanalala na njaa. Hupenda zaidi kujionyesha kwa watu na hasa pale wanaponunua Magari ya kutembelea.

8. Wengi wao wana vinywa Vilivyojaa matusi na maneno Makali ambayo huwezi kumdhania. Wapo tayari kurusha picha za NGONO au mtu anayekata mauno! Halafu utamsikia mrushaji akisema "JAMANI ANGALIENI HAPA NDIPO DUNIA ILIPOFIKIA" na kumbe yeye ndiye anayependa mambo hayo na yamejaa kwa simu yake! Ukiwa nao na kuwaangalia ni Dakika 10 wanaweza kujifanya wapo Kiroho, lakini dakika chache wanakuwa watu wa Kimwili. Na wapo tayari kwenda kwa WAGANGA WA KIENYEJI ili kukuza Kundi la Watu.

9. Mahubiri yao Mitume na Manabii yameegemea zaidi kwenye AGANO LA KALE na hasa Vitabu vya MALAKI (Fungu la Kumi), ZABURI (Misingi ikiharibika), Urejesho wa nyota, Mafanikio wakimnukuu Ibrahimu Baba wa Imani. Bila kujua kwamba Ibrahimu yeye alishakuwa na mali nyingi kwa sababu ya Juhudi zake. Bali Mungu alichokifanya pale ni kumuongezea tu. Zaidi ya hapo hakuna mahubiri zaidi! Labda hapo yatafuata mahubiri ya Kichwani ya Kufoka (Kukoroma) pasipo na maandiko!

10. Wengi wao hawajui nini maana ya Utume Ki-Biblia wala hawajui maana ya Unabii Ki-Biblia. Hata ukimuuliza juu ya Yesu anaweza hata kukujibu kwamba Yesu siyo Mungu! Ndiyo maana kwa hapa Tanzania Mitume wengi na Manabii ndiyo wamekuwa ni Wachungaji wa Kanisa.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, Nyakati za leo hakuna nabii, tangu ujio wa Yesu, mabii walikuwa wanatumika katika jambo fulani kama misingi ama tamaduni vimeharibiwa na watawala, hapo ndipo manabii walikuwa wanakuja, kazi yao kuu ni kutabiri yajayo, kuonya, nakutoa adhabu moja kwa moja ambayo Mungu amezungumza nao, siku hizi kunawanafunzi wa Yesu tunawaita " second disciples" Neno nabii ni neno zito sana, nabii akikutizama lazima utetemeke manake nikama umekutana na malaika, hao ambao wapo leo ni matapeli wanafanya biashara
 
Mpaka leo hii hakuna nabii wala mtume aliyetuambia corona inaisha lini,,ila wanasubiri wanasayansi wagundue dawa na wao ndo waanze kuponya corona kwa miujiza
 
Leo hawa manabii na mitume wetu wamepewa stahiki yao, kwakweli wanachokifanya sio kitu kizuri, wanatumia changamoto za maisha ya watu, na hasa wanawake, kuwa ndio mitaji yao ya kupigia hela. Wamwogope Mungu Mungu kwakweli
Unabii juu ya dunia ulishafungwa, kinachosubiriwa ni mwisho wa dunia sasa hawa jamaa ni unabii gani hasa wanaotoa. Halafu qualification ya kuwa mtume ni kupeleka injili kule ambako haijafika kama alivyofanya mtume Paulo kule Rumi na Asia na namna lilivyofanya kanisa katoliki kupeleka injili karibu dunia nzima. Sasa mtu anajiita mtume wakati yuko hapa hapa bunju ambapo watu wote walishasikia mafundisho ya injili....
 
Usihalalishe kisicho haki et kwaasabab vingne vinafanywa mkuu....ukiwa logicaly correct na kichwan zimo zile za kwel si za kukariri huwez sikiliza wanachohubiri na kuongea hao jamaa hata kwa dk 10..utaboreka na kuondoka..

Mi gf wangu alikua anasali huko kwa prof nan sjui makongo juu..ni sect ya major 1..yule bushiri.huko ni wanasal matajir tu..

Nilienda nikakaa dk 30 kwa tabu sana kumskiliza jamaa yule..na sikurud teeena

Mahubir yao yako cheap sana kwa intelligent mind.
Atakua Jamaa fulani anajiita Mtalemwa, Son of Major one, anapatikana makongo juu pia huyu jamaa
 
Aiseee mleta uzi umegonga mulemule kwa matapeli wajasilia dini , their are taking advantage of ignorance of the mass .Mimi mwenyewe nikiwa kama dereva wa wazito nimekutana na manabii na mitume uchwara wengi kwa waganga wa kienyeji , wakifuats dawa za kujaza watu na nguvu za kufukuzia mapepo . Ushahidi ninao nitaandika Uzi hapa nikipata muda ili watu waweze kujifunza .
 
Hao tumeishawashitukia,hiyo ni njia ya kupiga hela tu,hakuna kitu hapo,
Kuna bango moja huwa naliona pale Mwenge,Dar,eti "clinic ya yesu'harafu Kuna picha ya kuuzia sura.huwa nacheka sana,
Mwanzoni Hawa manabii walikuwa wakishindana kuweka picha zao kwenye mabango ya matangazo,sasa hv Kuna fasheni imekuja wanaweka picha zao wakiwa wamekumbatia wake zao,
 
Ndani ya mkoa mmoja unawakuta manabii/mitume zaidi ya 5+, wakati maandiko yanasema nabii akizaliwa ujue nabii aliyekuwa akihudumu eneo hilo hana kitambo kirefu. Na nabii siyo kama machungwa kila mkoa unayo🤣🤣🤣
imeandikwa kwny kitabu gani?
 
Back
Top Bottom