IS yamshambulia Waziri Mkuu wa Iraq. Yamuita "kibaraka wa Marekani"

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
4,181
2,000
Kundi la wanamgambo linalojiita Dola la Kiislamu, IS limemshambulia Waziri Mkuu mpya wa Iraq, Mustafa al-Kadhimi, kwa kumuita "kibaraka wa Marekani". Aidha IS imekosoa hatua ya kufungwa kwa eneo takatifu zaidi la ibada la Kiislamu katika mji mtakatifu wa Mecca, nchini Saudi Arabia, katika hatua za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Kwenye ujumbe wa sauti uliotolewa na kundi hilo na kusomwa na msemaji wake mkuu Abu Hamza al-Qurayshi jana usiku, msemaji huyo alihoji kwa nini misikiti inafungwa na watu wanazuiwa kuswali kwenye msikiti mkuu wa Mecca, akigusia kuwa Waislamu wana kinga na virusi vya corona, na kutoa mwito kwa wanamgambo hao kuanzisha mashambulizi ya kila siku nchini Syria, Iraq na mataifa mengine.

Ujumbe huu ni wa tatu kutolewa na kundi hilo tangu al-Qurayshi aliposhika madaraka hayo. Waziri mkuu wa Iraq, Mustafa al-Khadhimi, mkuu wa zamani wa idara ya kijasusi aliyeungwa mkono na Marekani aliingia mamlakani mapema mwezi huu.

1.jpg

Mustafa al-Kadhimi.

====


IS blasts Iraq PM as American agent, calls for more attacks

BAGHDAD - The Islamic State group in an audio message blasted Iraq’s new prime minister, calling him an “American agent,” and criticized the closure of Islam’s holiest shrine in the Saudi holy city of Mecca to limit the spread of coronavirus.

In the message allegedly read by the group’s chief spokesman Abu Hamza al-Qurayshi, released late Thursday, al-Qurayshi asked why mosques are being closed and people being prevented from praying at the Grand Mosque in Mecca, hinting that Muslims are immune to the coronavirus.

The virus outbreak disrupted Islamic worship in the Middle East as Saudi Arabia in late March banned its citizens and other residents of the kingdom from performing the minor pilgrimage to Mecca. In other countries in the Middle East, Friday prayers were also suspended to limit the spread of the virus.

Iraq’s new Prime Minister Mustafa al-Kadhimi, a former intelligence chief backed by Washington, took office earlier this month after he played a part for years in the war against IS. The group was declared defeated in Iraq in 2017.

Al-Kadhimi remains the “intelligence’s pointed sword” on the heads of Muslims, al-Qurayshi said, urging IS fighters to launch daily attacks in Syria, Iraq and other countries.

In recent weeks, the extremists have taken advantage of the pandemic to launch deadly attacks in their former self-declared caliphate in parts of Iraq and Syria.

On Wednesday, IS fighters attacked a Syrian government post in northern Syria killing eight soldiers. Russian airstrikes followed killing 11 IS gunmen, according to opposition activists.

A day later, three members of the U.S.-backed Kurdish-led Syria Democratic Forces were found with their throats slit in the eastern province of Deir el-Zour near the Iraqi border, where IS sleeper cells are active, according to the Britain-based Syrian Observatory for Human Rights, an opposition war monitor.

After the death of IS leader Abu Bakr al-Baghdadi in a U.S. raid in northwest Syria late last year, the group named Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi as his successor in October.

The new spokesman, Abu Hamza al-Qurayshi, replaced Abu al-Hassan al-Muhajer who was killed the same month.

Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurayshi has not released any audio messages since assuming his position as IS leader.

Thursday’s audio was apparently the third released by IS spokesman al-Qurayashi since he took office. In January, he said the extremists will start a new phase of attacks that will focus on Israel and blasted the U.S. administration’s plan for resolving the decades-old Israeli-Palestinian conflict.

Sources: DW, ABC News
 

chisluk

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
428
500
Hawa jamaa wanna roho ngumu sana kuna documentary niliona wanavyouwa watu, tena watu wengi karibia 100 kwa pamoja, sidhani kama wana roho za binadamu wa kawaida
 

Flano

JF-Expert Member
Aug 7, 2019
523
1,000
Naona vibaraka wanatajana na kunyoosheana vidole.
US endelea kuchochea kuni moto bado haujakolea vizuri.
 

ruhi

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
2,416
2,000
Hao jamaa hawana Akili nzuri; mbona Waislam wamekufa kwa Corona kama wengine?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom