Ni kweli ila sie waafrika tuna vijitabia vya hajabu sana kwani huwa hatupendi ukweli. Kabla ya kombe la dunia kuanza karibia ya wataalam wote na wadau wa soka duniani waliipa Ivory Coast nafasi ya kushinda kundi lao kutokana na kuwa na wachezaji wenye vipaji kulinganisha na nchi nyingine kwenye lile kundi. Leo wamechemsha watu wanatafuta mchawi ni nani, ndiyo maana mpira wetu hapa nyumbani haukui, kila kukicha tunatafuta visingizio wakati ukweli ni kwamba hatuchagui wachezaji wenye vipaji Taifa Stars bali wasanii wa Simba na Yanga ambao ni wachawi na sote twaelewa mchawi hafundishiki. Wadau, tutafika kweli? Ebu angalieni Tanzania ya leo inafungwa na nchi kama Rwanda au Burundi, kwa vipaji vipi? Tubadirike jamani.