Is there no knowledge and experience above him that can control him?

Hujui unachoongea labda unasubiri uteuzi! Angalia hizi kodi kandamizi zilivyosababisha watu kwa malaki kufunga biashara zao, mazao kama mbaazi, mahindi, mtama, ulezi na korosho vinaozea mashambani kwa zuio watu wasiuze! Je hii hali ya hofu iliyotanda nchi nzima je ni rafiki kwa biashara? Au nayo ni fursa wananchi waichangamkie!
Wewe unaejua unachoongea. Unajua ni chombo gani kinapokea malalamiko ya kodi kandamizi hapa Tanzania? Je kwanini bado hayo mazao yatalimwa mwakani kama yamefeli?
 
Hilo swali kwenye sentensi ya mwisho ndo lile 'wanyamwezi' wanaita: "a million dollar question"! Ngoja nibashiri majibu:
1. Ili kununua 'koro show' kila mwaka toka kwa wakulima halisi; kisha itabanguliwa na sido ili wananchi wale.
2. Kumalizia SGR na Steagler gorge ili gas yetu isitumike tena.
3. Kusakafia kaburi la upinzani na kuhakikisha chichiem inatawala milele.
4. Kuhakikisha 'malaika' wote wanaishi kama mashetani milele chini ya chichiem inayotawala milele.
5. Kuweka misingi itakayothibitisha utawala wa kidictator kweli na ambao hautahitaji ushirikiano na jumuia ya kimataifa; koro show tutakula wenyewe, dhahabu 'tutakula' wenyewe na utalii wa ndani utakuwa chanzo kikuu cha mapato ya serikali; wanyonge wote watakula na kusaza na usafiri wao utakuwa ndege na helkopta tu.

Time will tell!
 
Haya anayotufanyia ingekuwa nchi kama kenya asingeweza, kungeishatokea machafuko. Sisi watanzania ni sawa na Zimbabwe ya mugabe
 
Katika awamu hii ya uongozi wa nchi yetu, Sekta binafsi ni wapigadili wanaotakiwa kuishi kama mashetani! Lakini sera zetu za kiuchumi zilizosimikwa na kumwagiliwa vema awamu ya 3 na 4 bado zinasomeka vile vile: sekta binafsi ndiyo injini ya uchumi! Kazi ya miaka ya 20 inabomolewa mbele ya macho ya wahusika na bila ridhaa ya chama chao. Halafu watu wako kimya. Incredible. Nyerere tunayemuenzi angefanya hivi kweli.
Nchi inaingia msukosuko mkubwa kwaajili ya Jiwe na Bashite tu!
 
Takwimu hizi za "wananchi wengi' umezitoa/umezipata wapi?
Hata simtetei JPM ni common sense tu. Kama wananchi wengi wanapenda misaada, hawaingizi kipato, siyo wabunifu, kutwa kulalama na hawajui kutetea haki zao. Unategemea maajabu gani?
 
Viwanda vilivyoko vinaweza kubangua tani ngapi kwa mwaka?

As strange as it may sound, I am with him on this one.

Kama hata kubangua korosho tunalialia hivi, ni kipi tutakachoweza kukifanya sisi!

Acha SIDO watoke jasho na majaribio yao; who knows, may be something good can come out of it!

I want us to dare and be challenged. We need to be shaken up out of this false comfort of dependence for every little problem that confronts us.

Na kama anasoma mafaili ya Mwalimu Nyerere kama unavyodai, basi atakuwa anayasoma kinyumenyume au kivyake kwa sababu sioni mfanano wowote. Nadhani umeliweka hili ili kunogesha hoja yako tu, lakini badala ya kunogesha inatia ukakasi.
 
Hata huyo mropokaji akiondoka, aje Mbowe au Lowassa hawatafanikiwa siyo kwasababu hawana uwezo bali jamii yetu imeshikilia utamaduni na tabia ambazo zinaleta umaskini kuliko utajiri. Kwasasa JPM anapambana mwenyewe tu kutafuta maendeleo kwenye jamii ambayo inapenda starehe kuliko kazi.
Ushauri kutoka kwa MKIMBIZI UCHWARA
 
Korosho is not a problem that confronted us, it is a problem of our own making
As strange as it may sound, I am with him on this one.

Kama hata kubangua korosho tunalialia hivi, ni kipi tutakachoweza kukifanya sisi!

Acha SIDO watoke jasho na majaribio yao; who knows, may be something good can come out of it!

I want us to dare and be challenged. We need to be shaken up out of this false comfort of dependence for every little problem that confronts us.

Na kama anasoma mafaili ya Mwalimu Nyerere kama unavyodai, basi atakuwa anayasoma kinyumenyume au kivyake kwa sababu sioni mfanano wowote. Nadhani umeliweka hili ili kunogesha hoja yako tu, lakini badala ya kunogesha inatia ukakasi.
 
Garry Neville, jana baada ya kichapo cha 3-1 kwa Man utd kutoka Liverpool, alilalamikia upana/ukubwa wa matatizo ya Man utd.

Mourinho sio tatizo pekee ila ni moja ya matatizo ya timu hiyo kwa sasa.
Na CV yake inamtisha Woodward kiasi kwamba hawezi kumuelekeza chakufanya.

Hivi sisi kama Watanzania, Magufuli ana CV ipi ya kutisha watu wasimuelekeze jambo?
Mwinyi, Mkapa, Kikwete, n.k wanainterest gani kukaa kimya kwenye hii hali?

Mourinho mwenyewe kwenye post match press conference alisema; 'there are qualities you don't have and you can not develop them simply because they are not there'

Yeye aliwaangalia Robertson, Wijnaldum, Salah, Mane, na yule Mbrazil...sorry jina limenitoka. Intensity na physicality yao ilimpagawisha.

Ila statement yake inakula both ways, inammulika hata yeye.

Inawapa nguvu wanaomponda wakisema Mourinho is a manager stack in the past.

Mheshimiwa rais Magufuli, 'there are qualities you don't have and you can not developed them because they are simply not there'!

Nchi inaumia kwa majaribio na maelezo ya makabrasha ya Nyerere ambayo yanasomwa saa nane za usiku mtu akiwa amechoka.Mungu anajua kama yanasomwa kwa usahihi.

Msikilize waziri wako wa viwanda; "Akizungumza mjini hapa jana, Jumamosi Desemba 15, 2018 amesema kwa sasa kiwanda kilichopewa korosho kwa ajili ya ubanguaji ni cha Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) Mtwara kwa majaribio na baadaye watasaini mkataba."

That is what you are doing to us. Unafanyia maisha yetu majaribio.

Alafu unataka kuongoza miaka mingine mitano baada ya 2020, ili ufanye nini?
Ingekuwa taifa la watu wanaojielewa hata huko 2020 mbali sana
 
Matatizo ya serikali ya sasa yanachangiwa sana na wananchi na wafanyakazi wa umma kushindwa kutumia hizi fursa JPM anazotengeza kwa ajili ya manufaa yao. Bado wengi tuna mind set za zamani kama kuamini kwenye misaada ya maendeleo, kutokuwa wabunifu kwenye sekta zetu, kupoteza muda mwingi kwenye kulalamika badala ya kutengeneza pesa, wivu, fitna, majungu, wizi, kukwepa kodi, kushindwa kupigania haki zetu nakadhalika nakadhalika. Ukiona uongozi wa nchi una matatizo fahamu fika hata wananchi wake wana kasoro.
Inaonekana umeshushwa leo. Ambao wapo hapa hapa hawajui kesho itakuwaje, then unataka wawe wabunifu! Nchi imepoteza mwelekeo brother!
 
Inabidi nicheke tu. Nimekumbuka Bongo watu hamkosi majibu.
ndugu zetu waliokuwa ulaya huko ukiwaambia hali ngumu ya nyumbani wanatuambia nyie shida moja wavivu sana mnapenda vitonga, wakirudi nyumbani wao wenyewe wanakiri wanageuza kurudi nchi za watu. Wenzetu mliokuwa huko msituone sisi tumelala sana huku.
 
ndugu zetu waliokuwa ulaya huko ukiwaambia hali ngumu ya nyumbani wanatuambia nyie shida moja wavivu sana mnapenda vitonga, wakirudi nyumbani wao wenyewe wanakiri wanageuza kurudi nchi za watu. Wenzetu mliokuwa huko msituone sisi tumelala sana huku.
Uvivu upo Mkuu lakini kinachowakimbiza watu ni wivu, wizi, uchawi na fitna za nyumbani. Hizo tabia hazijaletwa na Magufuli bali wananchi wenzetu ndiyo maana nasema tamaduni na tabia za kitanzania zinachochea umaskini kuliko maendeleo.
 
Back
Top Bottom