Is Tanzania 'almost' impossible to do business!??

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,466
9,028
Nawasalimuni wanajamvi!

Mwaka jana nilikuwa nikimsaidia mgeni mmoja kwenye shughuli za uwekezaji. Mbali na taasisi nyingine, alikatishwa tamaa na utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) pamoja na Mamlaka ya vyakula na madawa (TFDA) na hakuamini kama kweli hawa jamaa wapo kwa ajili ya kujenga nchi yao au kuibomoa kutokana na usumbufu na kutojali walikokuonyesha! Na hakuelewa serikali ilikuwa inafanya nini juu ya hiyo hali maana kila kitu kinaonekana wazi. Hapo ndiyo akatoa kauli hiyo hapo kwenye subject!

Naomba msaada:
Kwa wale wakazi wa Dar es Salaam na hasa maeneo ya Bagamoyo rd na mikocheni tulitangaziwa juu ya mradi wa mall ya DAR VILLAGE pale karibu na bar maarufu ya Rose Garden. Miongoni mwa wapangaji (kama sikosei) ilikuwa ni chain ya supermarkets moja kutoka Kenya.

  • Je, yupo anayejua mustababali (fate) ya hiyo project? Maana nimeona kama umesimama!
  • Je, inaweza ika justify "Is Tanzania 'almost' impossible to do business!??"

Nawakilisha
 
TRA ipo kwa ajili ya makusanyo ya Mafisadi haipo kujenga nchi, ukiwa Mzawa unafanya kabiashara TRA watakufuata mpaka ufilisike ndio roho zitawatiuliwa. TRA inatumiakia mabwana zao wakina Lowassa, RA, Kikwete, Chenge na Mafisadi Mipapa kama Mkapa, Nimrod na wengineo. Kaiz kukusanya pesa na kununua Ma-Vx kwa ajili ya Mafisadi wanaolala Dodoma kwenye ukumbi wa kuzomeana na kupeana mipasho huku watanzania wakiletewa pikipiki za kubebea wake zao wenye mimba
 
Nadhani ule mpango ulipata matatizo wakati wa global economic crisis, credit lines zilikauka.
 
Ni fact "Tanzania is almost impossible to do business" mpaka kiyama kitasimama watanzania tutakufa maskini. TRA nia yao hasa ni kukubana sana usiweze hata kupumua na matokeo yake unafunga biashara na unazidi kuwa maskini.

Nina hamu sana ya kufanya biashara lakini nikiona adha wanazozipata wafanyabiashara kutoka TRA hamu yote inakwisha.

Kwa reference ya mkoa wa Tanga watu wengi sana wamefunga biashara na sababu kubwa ni TRA kuwamalizia mitaji yao kwa malipo ambao hayaeleweki.

Kufanya biashara ni kuchujua risk kubwa kwa sasa kwa nchi kama Tanzania.
 
Back
Top Bottom