Is QT Framework burning to the ground? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Is QT Framework burning to the ground?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Senghor, Jun 29, 2011.

 1. S

  Senghor Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni na majukumu wanajamvi.
  Tunafahamu kuwa kabla ya kununuliwa na NOKIA, QT framework ilikuwa chini ya umiliki wa Torolltech ikiendelezwa na vijana talented kweli wanaojulikana kama 'Trolls'. Baada ya ununuzi, tumeshuhudia ushirikiano kati ya Intel na NOKIA ambao umezaa MeeGo, kukiwa na malengo ya kuwekeza sana kwenye QT na kuifanya MeeGo kuwa OS yenye nguvu na maarufu kwenye Smartphones, Tablets, Netbooks, etc.
  Bado sijaelewa uamuzi wa CEO wa Nokia, Stephen Elop wa kuhamia kwenye WinMo(WP7) na kuifanya kuwa ndio OS tegemeo la baadaye itakayoendesha High-end smartphones za NOKIA, kwa kushirikiana na CEO wa Microsoft, Steve Ballmer.
  Elop ni mwana hisa wa Microsft ambaye ni wa 7 kwa wingi wa hisa alizonazo kwa wanahisa mmoja mmoja.
  Maelezo yaliyotolewa na NOKIA kuwa bado wataendelea kuiunga mkono QT kwa kuajili developers wengi zaidi, kutengeneza simu zaidi kama milioni 150, ku-release NOKIA N9 yenye MeeGo etc. bado hayajawaridhisha maprograma wengi waliokuwa wamewekeza nguvu zao na muda wao kwenye QT, kwani yanaonekana ni kuandaa mazingira ili WP7 iweze kuchukua hatamu!
  Kutokana na sababu za kiushindani bado nashindwa kujua hatima ya QT mikononi mwa Microsoft!!!
  Is it burning to the ground?
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  QT haipo mikononi mwa Microsoft, QT itaendelea kuwepo ila haitatumika kutengeneza program za WP7, itakuwa ni kwa ajili ya Symbian hadi hapo itakapoachwa na Nokia, pia Meego na Desktop. Kama unataka kudevelop for mobile Qt inabidi kuhama muda si mrefu.

  Story ya shares ni mostly nonsense, Elop alikuwa na shares worth just $3 million Microsoft wakati anaondoka, signing bonus yake pekee tu ilikuwa $6 million na sallary ni zaidi ya $1 million a year. Plus share zote za Microsoft ameshaziuza na amenunua za Nokia alikuwa hawezi kuziuza sababu za kisheria hadi sasa.

  Nokia wameitosa Symbian na Meego kwa sababu hata baada ya kuinvest mabillioni ya dolla na kuunguza miaka 7 walikuwa hawana OS na muhimu zaidi developer ecosystem iliyo kwenye level ya Apple iOS au Android na kulikuwa hakuna dalili kuwa wangeweza kuilete kwenye level hiyo any time soon, huku wanapoteza smartphone market share kila siku.

  Microsoft wanakuja na OS ambayo karibia kila mtu anaisifia kwenye UI yake, the best developer tools (Visual Studio), XNA, ecosytem kamili zune, Xbox, apps etc. Nokia wanajua kutengeneza hardware, pamoja wana chance nzuri ya kufanyikiwa.
   
Loading...