3 days to go,worry not dear!..
Masa subiri nigusie machache tu!!
unajua watu wanatofautiana kwenye haya mapenzi. Cha muhimu ni mtu utakayekutana nae mkawa wote kama wapenzi.
Inapendeza kusikilizana pia kwenye kuulizana maswali isiwe kama vile unaishi na 'detective' fulani ndani ya nyumba yako. Au jitahidi ku-twist maswali in a romantic if not a jokey way ili mtu asiwaze analindwa kila saa.
Sometimes mpe mtu nafasi,kama anatoka na rafiki zake out mpe viza yake arudi usiku wa manane hata asubuhi ajue unamjali ila humlindi kupita maelezo. lazima ugusie kuwa awe mwangalifu na vitu kadhaa kiafya na usalama wenu.
Ukimuuliza mtu swali akakujibu kwa hasira ujue umemkera hivyo unaweza kusema yaishe au kuomba msamaha kwa kuona umemkwaza kwa swali lako au jinsi ulivyouliza kwa ghadhabu.
Kila kitu kina raha na karaha zake!..
3 days to go,worry not dear!..
Masa subiri nigusie machache tu!!
unajua watu wanatofautiana kwenye haya mapenzi. Cha muhimu ni mtu utakayekutana nae mkawa wote kama wapenzi.
Inapendeza kusikilizana pia kwenye kuulizana maswali isiwe kama vile unaishi na 'detective' fulani ndani ya nyumba yako. Au jitahidi ku-twist maswali in a romantic if not a jokey way ili mtu asiwaze analindwa kila saa.
Sometimes mpe mtu nafasi,kama anatoka na rafiki zake out mpe viza yake arudi usiku wa manane hata asubuhi ajue unamjali ila humlindi kupita maelezo. lazima ugusie kuwa awe mwangalifu na vitu kadhaa kiafya na usalama wenu.
Ukimuuliza mtu swali akakujibu kwa hasira ujue umemkera hivyo unaweza kusema yaishe au kuomba msamaha kwa kuona umemkwaza kwa swali lako au jinsi ulivyouliza kwa ghadhabu.
Kila kitu kina raha na karaha zake!..
The Following User Says Thank You to BelindaJacob For This Useful Post:
Masanilo (Today)
...sasa mkuu "thanks" peke yake bila kusema lolote maana yake unakubaliana na BJ akeshe nje mpaka kesho yake, au basi tu unakubali kufa na tai yako shingoni? sema bana usikike... mi sipendi unyanyasike bana!
Mazee you have missed it, nadhani Masa ndo wa kupewa hiyo visa ....hata nikirudi asubuhi BJ atakuwa anajua nilikuwa kwenye safe hands! Kama BJ kurudi majogoo hiyo ngumu mpwa wangu!
Busara kama ya Lowassa!
...sipendwi kuulizwa swali ambalo jibu lake lipo obvious!
mfano; mtu anakuona upo 'bize' na JF, anakuuliza " ...hulali leo? ", ebo! kwani mie ni mtoto mdogo nisiyejua time ya kulala?
...au, 'bahati mbaya' ulitoa intro kwa mamsapu kuhusu yule binti mrembo aliyeajiriwa ofisini kwenu. Siku ya siku mmekwaruzana kidogo mamsapu anaanza, "..hajambo yule 'fulani' ?!" ...halafu kila jibu utalolitoa linazaa swali jipya!
Heee hata hii huwa mwataka tuwaambie? Wengine vifua vidogo jamani hamkawii kwenda kuwakwida mashati watongozaji. Wengine marafiki zenu jamani ah!!
MJ1 waambie ndo ukweli!
Jinsi wanavyowatongoza wa wenzao, na wao wanatongozwa hivyohivyo!
Dude its like u opened a page in my relationship..muulize swali yeye utasikia 'i dont need this mara simu zinakatwa mara u stress me' wanawake viumbe vya ajabu..we still love them though.
Mzee akirudi jioni anakwambia unamfahamu mama flani na wewe unaitikie eheee anakwambia ananitaka na ukiangalia mama mwenyewe amejaaliwa kila kitu kuliko wewe,utafanyaje?
Hakuna haja ya kutaka kujua fine details za previous relationship za spouse wako.Kwa mfano,Ashakum si matusi, kuna haja kweli ya kujua former boyfriend wa mkeo anavaa 'kiatu' saizi gani? au demu wa zamani wa mmeo aanavaa sidiria saizi gani?SWALI ZURI. Ngoja nione watu watavyokuja 'kujikaanga' hapa!... 😀
WoS dada we acha ukisikia relationship ujue zipo za aina nyingi.
I have SEEN dada shost yangu nafanya nae kazi yaani huwa namwonea huruma. Si kwamba anadanganya bali ni katika kujaribu kukumbuka vitu alivyofanya mchana huo ili akiulizwa asijeshindwa kujibu maana akishindwa ni ugomvi. Sometimes huwa anaulizwa wakati nimekupigia simu ulipokea ukiwa unacheka, ulikuwa unacheka nini na nani na kwa nini ? au ulikuwa unanicheka mimi kukupigia simu' sasa swali kama hili unaweza kujibu kama alikupigia mara moja mtu mwenyewe ni kila baada ya nusu saa anapiga so itabidi ukumbuke ni simu ya ngapi ndo ulipokea ukiwa unacheka yaani ni adhabu.
Heee hata hii huwa mwataka tuwaambie? Wengine vifua vidogo jamani hamkawii kwenda kuwakwida mashati watongozaji. Wengine marafiki zenu jamani ah!!
na wao wakitongoza wanakuja kutuambia?
Mazee Front short Tail sio dick man! Teh tehwanaume ni animals with a dick, which we can interchangeably use for making love (Not my Bellies)
hahahaha kapinga kwetu wengine itakuwa ngumu asa mfano best friend wa mtu wako anakutokea of coz huwa wanajaribu kwanza ila ukikubali anakula then moto huku akiwa keshakuchafua PR yako. Sasa mfano kama huu akikutokea nawe ukamtolea nje kuna haja ya kukwambia openly kuwa best yako kafanya hivi au tuogope kuwa gombanisha?
...tena ukimkazia macho akuambie ukweli kama hajatongozwa anaanza kujichekesha chekesha! aisee inaudhi wewe! 😡
Duh kaaaazi kweri kweri umenikumbusha zamani kuna BF wangu mmoja aliwahi kunituhumu kuwa na mahusiano na best friend wake kisa huyo shemeji yangu alinitokeaga nikamtukana sana ila sikumwambia BF zaidi ya kuishia kumwambia yule rafiki yako simpendi, ukiulizwa kwa nini nasema basi tu simpendi moyo haunipi kabisa yaani ikiwezekana ukiwa nae usiniite wala msinipitie kazini. Ila alipokuja kusikia toka kwa friend yake mwingine (nadhani that guy alikwenda kumsimulia) asinigeuzie kibao kuwa nilikuwa natoka naye? pamoja na kuelezwa nilivyo mtukana!! Basi nikajifunza tangu siku hiyo huwa nasema halafu watajuana wao.
Kwa kweli ni moja ya mambo yanayoniudhi sana. Nimetoka kibaruani napitia mahala tunaongea na just friends mambo ya kujiendeleza kimaisha. Unafika home my wife anaanza ulikuwa wapi? na nani, mliongea nini? yule dada wa nguo ya njano alikuwa nani kwako,,,, bla bla kibao. Jamani nawaambia UKIITWA MWIZI NA WEWE HUJAIBA sometimes unatamani kuiba ujue kuiba huko kuna nini na pengine uhalalishe wizi huo. Hujafanya kitu unaambiwa umefanya. Hivi kwa nini tusijenge uaminifu kwa wenzetu?
Unakuta hata wanaume mke yuko mbali anafanya kazi anaamua kuja ghafla eti kumfumania mke? Mnatafuta nini? si kama umemchoka mwenzako mwambie! Mweleze ukweli badala ya kutafuta vijisababu. Ama ndo tuseme ni Wivu huo? Inakera sanaa