Mshirikishe Mungu kabla ya kufanya maamuzi na usimshirikishe Mugu katika kujutia maamuzi uliyoyafanya mwenyewe
Kuongezea hapo,tusisahau kuwa Mungu ametupa akili.
Mtegemee Mungu huku ukizitumia vema akili alizokupa.
Mshirikishe Mungu kabla ya maamuzi,but also remember Mungu anazungumza nawe kupitia akili yako.Ipe akili yako nafasi ya kukuhabarisha na kukushauri.
Take your time kumchunguza huyo mtu na kumjua,kabla hamjafika mbali.
Kwa maelezo yako hapo juu,kinachokuumiza ni tabia ya mtu.Je,wakati mnaanza ulijipa muda wa kumjua kitabia?Ni kawaida ya binadamu kuficha makucha katika early stages za mahusiano,anakuonyesha positive side yake tu,negatives anaficha,wakati kiukweli hakuna binadamu mwenye positives tupu,wote tuna negatives zetu.
Je,ulijipa muda kuzijua negatives zake zote?hii inawezekana iwapo utamchunguza kwa muda mrefu.Je,na wewe ulimuonyesha all your true colours au ulimvutia kwa kujenga taswira isiyokureflect kiuhalisia na ambayo umeshindwa kuidumisha kwa muda mrefu,sasa swaga zimeisha,your true colours appear,na mwenzio anareact to your new image,vurugu zinaanzia hapo.
Ukishajipa muda wa kutosha kumjua mtu,utazijua negatives zake,ukiishazijua,there comes the point,ile ROHO aliyokupa Mungu ndani yako inakushauri nini kuhusu negatives unazoziona kwa huyo mtu?zinavumilika,ni sahihi kuzivumilia au ni ujinga kuzivumilia?ukimpa nafasi unajenga au unajibomoa hadi wewe mwenyewe?
Unajua mahusiano ya ndoa ni kitu tofauti na mahusiano mengine.
Wengi hugeneralize mambo.
Kwenye ndoa ni hekima ukampata mtu mnayeendana kwa mambo yote ya muhimu,hasa tabia.
Huenda Mungu anatushauri lakini hatusikii huo ushauri kwa kuwa tunataka kile tutakacho sisi kitokee,yaani umempenda mtu kwa sura,materials etc,halafu hutaki awe na tabia mbaya,hata ukiziona unasema God will care the rest,mwisho wa siku ukiumia unamlalamikia.
Mungu hatengenezi matatizo,tunayaleta wenyewe katika maisha yetu kwa kutomshirikisha au kumpa nafasi ya kutushauri juu ya kila kitu.
Kumbuka,huyo mwenzio ni binadamu huru mwenye choice zake kama wewe,ni vigumu kuishi na mtu ambaye Mungu si one of his/her choices,huku wewe ukimchagua Mungu kama muhimu kwako.Mtapishana tu na hamtawezana,na atakuumiza.
Ni hekima kujua jambo gani la kuvumilia,na jambo gani la kuachana nalo kabisa.
Na uamuzi wa mapema huepusha hasara.