Iron Mike..

Mama mae! Botha kapigwa kono moja la kulia zito, chali...

Mchezo gani huu, hauna hata kutegeme, ndio maana mie nikaukimbia🤣.

Kiukweli mie nilikuwa mpenzi haswa wa tyson, ukija kwenye timing zake ana mikono mfululu, combination zake migumi mizito.
 
Kupata mtu wa Amina yake itachukua muda sana,watu tulikuwa hatulali,alafu pambano anamaliza within seconds
 
Mohamed ali alikuwa ana uwezo wa kukuweka chini mapema tu but alikuwa anaburudisha kizazi chake na formen joe frazier ni kumbukumbu tosha namna mchezo ulivyokuwa na msisimko ukija kwa mwamba huu hakuwa mtu wa kubembeleza yeye hata sekunde ya kwanza anamaliza kimsingi ndio bondia wangu wa mwisho kumshabikia sikuhizi heavyweight mtu anatoka penye pambano haendi hata kukoga anakwenda disco coz hana ngeu wala hajavimba uso.
 
Huyu mwamba nimeona anajipanga kutaka kurudi tena ulingoni,sijui kama atafua dafu,ila nadhani anajua atatengeneza pesa nyingi sana kwenye huo mpambano hata kama atashindwa,kwahiyo hatajali kupoteza pambano anaangalia zaidi mkwanja...

Sent using Jamii Forums mobile app
Aangalie na kifo pia sababu akili ipo ila mwili hauta mkubalia kirahisi rahisi hivyo sababu hata waqt wa uhai wake wa ndondi hakuwa mvumilivu wa kucheza mizunguuko (rounds )nyingi sasa asiweke njaa penye mfuko wa rambo aah imepigwa marufuku hii
 
Back
Top Bottom