Iringa- wamachinga waruhusiwa kuendelea na biashara eneo la mashine tatu

GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,620
4,265
Katika hali ya kustaajabisha, wakati baadhi ya wamachinga kutoka Jijini Mbeya wakijiandaa kuja kulazimisha serikali kuruhusu wenzao wa Iringa kuendelea na mnada wa jumapili eneo la mashine tatu Iringa mjini;

leo takribani wamachinga 40 wameongozana hadi kwa mkurugenzi Mr. Mwamwindi (ofisini) na kumtaka ajiandae kuwaua wote hapo jumapili kwani hawatakubali kamwe kuondolewa.

Lakini kinyume chake, mkurugenzi pamoja na meya wamekuwa wapole, kwanza wakawaambia wafanya biashara hao wawe wapole ili waelewane, ndipo zikanunuliwa soda na maji na mazungumzo kuchukua mkondo wake.

Mwisho Meya na Mkurugenzi wakawakubalia wamachinga hao kuendelea na biashara siku ya jumapili kwa kuwaasa kuepuka vurugu na kuzingatia usafi wa mazingira eneo hilo. Basi ikawa shangwe tupu.

Chanzo: mdogo wangu alikuwepo (mfanyabiashara)

my take:
upo wapi ulazima wa nguvu na rasilimali zilizotumika jumapili iliyopita.
 
wacha bwana! ngoja niwatafute wandugu apo irg wanijuze kinaga-ubaga
mana naona kama ndoto ivi hahahahaa
 
Katika hali ya kustaajabisha, wakati baadhi ya wamachinga kutoka Jijini Mbeya wakijiandaa kuja kulazimisha serikali kuruhusu wenzao wa Iringa kuendelea na mnada wa jumapili eneo la mashine tatu Iringa mjini;

leo takribani wamachinga 40 wameongozana hadi kwa mkurugenzi Mr. Mwamwindi (ofisini) na kumtaka ajiandae kuwaua wote hapo jumapili kwani hawatakubali kamwe kuondolewa.

Lakini kinyume chake, mkurugenzi pamoja na meya wamekuwa wapole, kwanza wakawaambia wafanya biashara hao wawe wapole ili waelewane, ndipo zikanunuliwa soda na maji na mazungumzo kuchukua mkondo wake.

Mwisho Meya na Mkurugenzi wakawakubalia wamachinga hao kuendelea na biashara siku ya jumapili kwa kuwaasa kuepuka vurugu na kuzingatia usafi wa mazingira eneo hilo. Basi ikawa shangwe tupu.

Chanzo: mdogo wangu alikuwepo (mfanyabiashara)

my take:
upo wapi ulazima wa nguvu na rasilimali zilizotumika jumapili iliyopita.

Ni makosa kwa Wamachinga kufanya biashara barabarani lakini sio kosa kwa Rais Mkapa kufanya biashara Ikulu!!!!!!
 
Serikali sikivu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
safi sana mkurugenzi pamoja na meya tunataka viongozi wenye busara kwenye kutatua matatizo ya wananchi wao
 
Hiyo nzuri ingelikuwa haya mazungumzo yanafanyika mapema kabla ya madhara duh! Tungekuwa tumepiga hatua sana hasa ktk kutoa maamuzi yanayowahusu wananchi moja kwa moja.
 
Wanaogopa kuzua mengine majeshi yao yote yapo kusini kwani mwadhan asikali n wengi kiasi hicho huenda wameambiwa wawazugezuge mtwara pakipoa walizue sasa iringa hata mwanza nasikia wamesoma alama za nyakati
 
Umeona mbali mkuu.
 
Back
Top Bottom