Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
RC HAPI AWASHUKIA KINANA, MAKAMBA, MEMBE
Asema muda wao wa utumishi umekwisha ni vema wanyamaze kumuacha Rais Magufuli afanye kazi.
“Shambulio dhidi ya Rais ni shambulio letu sote, ni shambulio la serikali nzima. Hivyo kama Mkuu wa Mkoa, kijana na mzalendo siwezi kukaa kimya. Tutamlinda Rais wetu kwa gharama yoyote”
”Yanayoendelea na kufanywa na wastaafu sisi kama vijana tunaowaheshimu sana tunasikitika na kushangaa.Imekuaje leo wamesahau mafundisho ambayo wamekua wanatufundisha miaka yote? Subira, uvumilivu, kutii mamlaka na kuheshimu utaratibu vimepotelea wapi??
Wana maslahi gani yaliyojificha??”
”Shambulio dhidi ya umoja na mshikamano wetu ni shambulio letu sote. Vijana tutajibu mapigo.”
”Wanataka kumuondoa Rais Magufuli kwenye shabaha yake kwa nchi. Wanataka kumpotezea dira aache kushughulika na shida za wananchi ashughulike na mambo ya hovyo. Hatuwezi kuruhusu hilo litokee.”
”Njama zao dhidi ya nchi yetu tunazijua. Wengine ubinafsi na kukosa Urais mwaka 2015 bado kunawatesa.”
”Hakuna mtu muongo nchi hii kama Bernard Membe. Akiwa waziri aliwahadaa umma wote wakiwemo mawaziri wenzie kuwa yeye ndiye Rais ajaye anayesubiri muda tu na kwamba wengine wote wanapoteza muda. Lakini tangu kakosa uRais bado hajaamini, amechanganyikiwa.”
”MEMBE alipoanza kumshambulia Rais Magufuli January 22,23 mwaka 2016 akiwa MNEC, nafasi kubwa kabisa, hakuna mzee aliyekemea wala kutoa waraka wa kutaka suala hilo lijadiliwe. Wakati huo Rais Magufuli hakuwa Mwenyekiti wa CCM bado.”
”Nape aliyekuwa mwenezi hakutoa tamko kumuonya MEMBE wala Katibu Mkuu Kinana. Wote walikaa kimya huku Rais Magufuli akishambuliwa tena na mjumbe wa NEC, kikao kikubwa kabisa cha Chama. Hawa wote walimlea MEMBE na alikua hagusiki. Leo hii wao wamestaafu wamesemwa wanataka Chama kikae vikao kujibu.”
”Nilipojitolea kumjibu Membe na kumtetea Mhe Rais tarehe 24/1/2016 nikiwa Katibu Msaidizi wa CCM pale Lumumba nilishughulikiwa sana na hawa kina NAPE huku maelekezo yakitolewa kuwa nivuliwe nafasi zangu za uongozi wa kitengo cha Vyuo vikuu na nipelekwe vijijini niondolewe Lumumba. Hao ndio kina Nape.”
”Namuomba Rais wala asiwajibu hawa watu, atuachie hiyo kazi sisi. Yeye abaki kwenye focus ya nchi maana lengo Lao ovu ni kumtoa kwenye mstari.”
”Membe alishindwa mapambano akiwa Waziri wa mambo ya nje, akijipambanua kuwa Waziri mpendwa wa awamu ya nne (the beloved minister), leo hawezi kutusumbua akiwa mstaafu.”
”Wazee wastaafu ni muhimu wakae kimya, wamuache Rais afanye kazi aliyopewa na watanzania. Ukistaafu kusemwa ni kawaida na wao sio wa kwanza.”
”Mzee Mkapa aliwahi kusema mwanasiasa nguli wa shughuli za serikali ni yule aliyestaafu kisha akachunga ulimi wake. Wazee Hawa wachukue busara hii ya mzee Mkapa itawasaidia.”
”Vijana tutamlinda Rais wetu, ili yeye ajikite kwenye kazi ya kujenga nchi hasa katika kipindi hiki cha mageuzi makubwa ndani ya taifa letu.”
RC Hapi