Iringa Manispaa: Tamisemi, Mkurugenzi Mseo na HR Mmewaibia Walimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iringa Manispaa: Tamisemi, Mkurugenzi Mseo na HR Mmewaibia Walimu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Alexism, Feb 12, 2012.

 1. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Wanajanvi,
  hakuna kitu ambacho kinalitafuna hili taifa kama wizi na ubadhirifu wa mali na pesa za umma.
  Mwaka 2011 January 24 ajira za walimu zilitoka na walaka kuwa mwalimu wa shahada (degree) alipwa pesa za usafirishaji wa mizigo tani tano na kila kilomita ikiwa ni shilingi elfu moja.
  Kitu ambacho kinashangaza katika kulipwa mara ya kwanza walimu walilipwa karibu robo ya hizo pesa.
  Mwaka huu mwezi wa pili tarehe 4 walimu walidai kwa mbinde madai yao yaliyobaki na wakalipwa pesa pungufu yaani tani tatu badala ya tani tano.
  Baada ya kufatilia TAMISEMI wakaambiwa kuwa madai yao ndo hayo yaliyopelekwa na Manispaa.Cha ajabu kuna sehemu kubwa mfano Mbeya vijiji,Bukoba,Songea,Hai walimu wamelipwa hela ya tani tano.Tamisemi,Mkurugenzi,HR na MSEO bila shaka mnajua kuwa manispaa hii inatuhuma kibao kuhusu pesa.Walipeni walimu pesa za kama sivyo mtakuja juta.NAWASILISHA.
   
Loading...