Iringa: Ajinyonga kisa ugumu wa maisha

Iringa: Ajinyonga kisa ugumu wa maisha

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,244
Mkaziwa Ilula Matalawe Mkoani Iringa, Abel Zakayo Mlasu (26) ambaye pia ni Mwigizaji wa Filamu amekutwa amejinyonga kwa kutumia mtandio katika paa la nyumba ambayo alikuwa akiishi yeye na Mama yake huku chanzo kikidai ni ugumu wa maisha uliompelekea kuwa na msongo wa mawazo, Uongozi Mtaa umethibitisha.

Fredy Saimon Nzwaga ni Kiongozi wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Iringa ambaye pia alikuwa ni mtu wa karibu na Abel ambapo ameiambia Ayo TV kuwa Abel alikuwa akiishi na Mama yake na kutokana na changamoto za maisha Abel alianza kubadilika na kuanza kunywa pombe na alionekana kama Mtu mwenye msongo wa mawazo.

Elina Mvela ni Mama mzazi wa Abel ambapo amesema October 18, 2023 Mwanae alitoka kwenye mizunguko yake na kurudi nyumbani lakini alikuwa amebadilika sana na kuwa kama Mtu aliyechanganyikiwa na ndipo alichukua hatua ya kumfunga na kamba na kumfungia chumbani na baada ya muda alimuona ametulia na kumpa chakula .

Siku ya tukio Mama mzazi anasema aliamka na kwenda kwenye mizunguko lakini aliporudi nyumbani alikuta Abel amejifungia mlango na ndipo walipofanya juhudi za kuvunja mlango na kukuta amejinyonga kwa kujitundika katika paa la nyumba .

Abel amejingonga October 21,2023 na kuzikwa jana October 22, 2023 katika makaburi yaliyopo katika eneo la Ilula.

Millard Ayo
 
Umri kama huo wake na mimi nusu nijinyongege kwa ugumu wa maisha, umri wa 20 mpaka 30 sio umri mzuri kiutafutaji kwa sisi vijana wa kimaskini ambao wazazi hawakuandaa maisha yetu ya baadae, ni umri wa mapito makali sana.
 
Kabisa mkuu. Unakuta umemalza chuo una mtaji kazi ni mziki ni hatari aisee.Ni kuomba Mungu tu
Umri kama huo wake na mimi nusu nijinyongege kwa ugumu wa maisha, umri wa 20 mpaka 30 sio umri mzuri kiutafutaji kwa sisi vijana wa kimaskini ambao wazazi hawakuandaa maisha yetu ya baadae, ni umri wa mapito makali sana.
 
Huyo siyo kajinyonga sababu ya DP World kupewa bandari jana?

Hana udugu na mdudu huyo?
 
Back
Top Bottom