Iringa: Ajinyonga kisa ugumu wa maisha

Iringa: Ajinyonga kisa ugumu wa maisha

Mkaziwa Ilula Matalawe Mkoani Iringa, Abel Zakayo Mlasu (26) ambaye pia ni Mwigizaji wa Filamu amekutwa amejinyonga kwa kutumia mtandio katika paa la nyumba ambayo alikuwa akiishi yeye na Mama yake huku chanzo kikidai ni ugumu wa maisha uliompelekea kuwa na msongo wa mawazo, Uongozi Mtaa umethibitisha.

Fredy Saimon Nzwaga ni Kiongozi wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Iringa ambaye pia alikuwa ni mtu wa karibu na Abel ambapo ameiambia Ayo TV kuwa Abel alikuwa akiishi na Mama yake na kutokana na changamoto za maisha Abel alianza kubadilika na kuanza kunywa pombe na alionekana kama Mtu mwenye msongo wa mawazo.

Elina Mvela ni Mama mzazi wa Abel ambapo amesema October 18, 2023 Mwanae alitoka kwenye mizunguko yake na kurudi nyumbani lakini alikuwa amebadilika sana na kuwa kama Mtu aliyechanganyikiwa na ndipo alichukua hatua ya kumfunga na kamba na kumfungia chumbani na baada ya muda alimuona ametulia na kumpa chakula .

Siku ya tukio Mama mzazi anasema aliamka na kwenda kwenye mizunguko lakini aliporudi nyumbani alikuta Abel amejifungia mlango na ndipo walipofanya juhudi za kuvunja mlango na kukuta amejinyonga kwa kujitundika katika paa la nyumba .

Abel amejingonga October 21,2023 na kuzikwa jana October 22, 2023 katika makaburi yaliyopo katika eneo la Ilula.

Millard Ayo
Mchawi wa haya yote ni ccm.
 
ushawahi kutembea jua kali alafu hata Mia mfukoni hauna?

Mara nyingi sana nilishatembea kwa miguu kutoka Kimara mpaka Kariakoo tena mchana wenye jua kali sana. Mfukoni sikua hata na mia mbovu nahangaikia michongo ambayo haikuwahi kutick!

Nilifikiria kujiua mara moja kutokana na ugumu wa maisha wa wakati ule. Mpaka hapa nilipofika namshukuru Mungu
 
Kabla hujajinyonga tafuta mbususu mnato piga then tafuta kitimoto nusu na ndizi na safari baridi alafu tafuta stick kaa kwenye upepo ufikirie maamuzi yako

Hizo pesa za yote hayo anazitoa wapi?
Wewe hayajakukuta bado
 
Mara nyingi sana nilishatembea kwa miguu kutoka Kimara mpaka Kariakoo tena mchana wenye jua kali sana. Mfukoni sikua hata na mia mbovu nahangaikia michongo ambayo haikuwahi kutick!

Nilifikiria kujiua mara moja kutokana na ugumu wa maisha wa wakati ule. Mpaka hapa nilipofika namshukuru Mungu

Pole sana!! Wakati mwingine ni nguvu ya pepo mchafu inakuvuta kufanya hayo.
Hongera kwa kuyashinda hayo
 
Daaah kizimkazi hata hajui na wala hajali machungu ya watanganyika
 
Mungu tu aingilie kati maana vijana tusio weza kushikwa mikono na mtu yyte tunayo yapitia hayapimik
 
Umri kama huo wake na mimi nusu nijinyongege kwa ugumu wa maisha, umri wa 20 mpaka 30 sio umri mzuri kiutafutaji kwa sisi vijana wa kimaskini ambao wazazi hawakuandaa maisha yetu ya baadae, ni umri wa mapito makali sana.

Ni umri sahihi wa kukuumba kuwa mtu mzima wa baadae.

Jinsi utakavyokabiliana na yote kwenye umri huo ndio utapata tafsiri ni aina gani ya maisha utaishi baadae.


Maamuzi yako ya sasa ndio yanaijenga baadae yako.


Maisha ni safari tamu yenye utamu na uchungu ndani yake. Hata mitihani, majaribu, changamoto ni sehemu ya hayo maisha.





Apumzike kwa amani kijana.
 
Huwa wana misimamo ya kijinga,nimemkumbuka houseboy wetu ,misimamo yake na kiburi ,ni next level,yule akitaka kujinyonga
ni sekunde


Mbali ya misimamo yao, hapo taarifa inasema mama yake mzazi alimfunga kamba na kumfungia chumbani siku chache kabla ya kujinyonga sababu alikua hamuelewi ni Kama kachanyakiwa.


Sasa Kama mtu anapitia kipindi kigumu katika maisha yake na bado umri wake ni mdogo maana yake ni kwamba bado hana uzoefu mzuri wa maisha kwa ujumla.

Mama mtu badala ya kusimama Kama nguzo kwa mwanae na kumjaza moyo wa kuendelea kupambana huku akimtuliza na kumuondolea uwoga as a mother should be, lakini yeye ndio kaenda kumfunga kamba kabisa!


It’s easy kuona kapata wapi motivation ya kujiua.
 
Wahehe kujinyonga ni km tu kukohoa... Kwao very simple sana
 
Back
Top Bottom