Iringa: Ajinyonga baada ya kuzidiwa na Madeni ya VICOBA

Iringa: Ajinyonga baada ya kuzidiwa na Madeni ya VICOBA

Kujiua sio suluhisho, alikuwa na mwenza, wangekaa na kujadili namna ya kurejesha fedha za watu
 
Huyu Mkwawa huyu , urithi aliouacha kwenye kabila lake ni wa ajabu na wa hovyo sana
 
Hatari sana, unaweza kuta alipopewa akatapeliwa au ameona uwezo wa marejesho haupo, si rahisi mtu kuchukua maamuzi ya kujitoa uhai kirahisi hivyo
 
Ukiona mkeo anajiunga na Vikoba mpe talaka kabisa,muda sio mrefu wanao watabaki yatima na ww mume kupata gharama za jeneza pamoja na kulisha watu msibani.
 
Tozo kila kona alafu watu wanapeana posho za 250k kujadili tozo.

Eeh mungu mrudishe mwanao fasta utuokoe na hili janga
Wa
Tozo kila kona alafu watu wanapeana posho za 250k kujadili tozo.

Eeh mungu mrudishe mwanao fasta utuokoe na hili janga
Waendao hawarudi best....tuombe Mungu atupe was kufanana nae. Mungu husikia maombi yetu,atatujibu kwa wakati
 
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Enea Mkimbo (55) Mkazi wa Kihesa Kilolo Manispaa ya Iringa, amejinyonga leo September 14, 2022 chanzo kikidaiwa kuwa ni kuzidiwa na madeni ya VICOBA na usumbufu kutoka kwa wanakikundi wenzie.

Mwenyekiti wa mtaa huo Michael Mlalwe amesema marehemu Enea ambaye ameacha mume na watoto watano, jana September 13, 2022 alifuatwa na wanakikundi wakimshinikiza kutoa pesa, ambapo baada ya tukio hilo Enea alimuaga mumewe kuwa anaenda kulala kwa mama yake mzazi eneo la Ilembila na badala yake aliingia jikoni na kujinyonga kwa kutumia kitenge.

Mwenyekiti huyo amesema serikali ya mtaa inapanga kuwaita wanakikundi ili kujua walizungumza nini na Enea mpaka kufikia hatua ya kujitoa uhai wake.

Kufuatia tukio hilo wananchi wa mtaa huo wameiomba serikali kuangalia upya uwepo wa taasisi zinazotoa mikopo kwa riba kubwa inayoumiza wananchi maarufu kama mikopo ya moto ambayo imekua ikichangia watu kujitoa uhai.


Millard Ayo
Riba iangaliwe mana hata benk hakuna riba hizo sijuwi serikali hapo inatumia vigezo gani.Lakini kwa upande mwingine wanaume wanawatuma wake zao kukopa na hawawasaidii kulipa,au wanawake wanakopa kwa kiburi bila kushirikisha mume,pia kukopa bila mipango madhubuti.Kuna mtu jirani yangu alikopa kumuandalia mume wake birth day ulibukeni kama huu ukipelekea kifo tutasemaje hapa?
 
Back
Top Bottom