Obamaeli Rutajecha
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 230
- 274
Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema kuwa ana mpango wa kuwa Mchungaji pamoja na kumiliki kanisa lake yeye mwenyewe siku za usoni na kwamba anamuomba Mungu kila siku aweze kutimiza ndoto hizo.
Kauli hii imetoka kinywani mwa msanii huyo pindi alipokuwa akijibu maswali mubashara aliyokuwa anaulizwa na mashabiki zake kupitia katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipindi cha Kikaangoni
"Nina ndoto ya kuwa mchungaji na kila siku huwa nina muomba Mungu anifanikishie suala hilo niweze kutimiza japokuwa sasa hivi bado nipo katika changamoto kubwa ila natumai ndoto zangu zitatimia.
Natamani kuwa pastor ambaye ni mwalimu, niwafundishe watu Mungu anataka nini, lakini sitaki kuanzisha kanisa kama biashara, sitaki kucheza na Mungu, ndiyo maana najipanga kwanza sitaki kukurupuka, nataka niwafundishe watu Mungu anataka nini, na jinsi ya kumuomba Mungu". Alisema Uwoya
Haya sasa mjiandae kwenda kanisani kwa mchungaji Irene Uwoya mkasifu na kuabudu!
Hivi ni wito au ni nini? Alianza Nay wa mitego leo Uwoya..maoni yenu wakuu!