Irene Uwoya: Bongo movie hatuna hela, magari na nguo huwa tunaazima na hatuna raha kuwa wasanii

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
2,689
2,000
Msanii wa bongomovie Irene Uwoya amedai wasanii wa Bongo movie hawana hela na vitu na maisha wanayoonekana wanayo ni vya kuazima na sio vya kwao
Amedai inabidi waazima kwa kuwa ni maarufu na wanaona soo kuonekana hawana hela wakati wana majina makubwa na hii inawafanya wakose raha kuwa wasanii

 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,584
2,000
Hii huenda ikawa ni sababu kubwa hawa jamaa wanajiingiza kwenye madawa ya kulevya.

Inauma sana kuigizia kwenye nyumba za kifahari na maisha ya juu wakati kiuhalisia una hali tete. Ndio maana inabidi wajiliwaze kwa mihadarati
 

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,792
2,000
Hii huenda ikawa ni sababu kubwa hawa jamaa wanajiingiza kwenye madawa ya kulevya.

Inauma sana kuigizia kwenye nyumba za kifahari na maisha ya juu wakati kiuhalisia una hali tete. Ndio maana inabidi wajiliwaze kwa mihadarati
Bongo movi kujihushisha na mambo ya kisiasa imewaaribia sana kimapato
 

Dundo_Boy

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,464
2,000
Hilo ni kundi jipya la mapenzi wala si bongo movie km tunavyoielewa. Humo hakuna uigizaji bali kuna mapenzi mubashara
 

mfetere

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
234
225
Ndio maana hata movie zao utaona mtu ameigiza kama zombie halafu anakula mchicha badala ya nyama sijui hata hela ya kununua nyama hawana, haya jini unakuta amevaa t-shirt ya Liverpool jamani sasa movie hizo nani atashawishika kutoa pesa mfukoni na kununua.
 

miwani ya maisha

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
1,739
2,000
Tanzania ya Viwanda inakuja....mkashike jembe acheni kuuza sura mjini!
Ray na wenzake wameanza tayari..."JICHUBUE UCHUBULIWE"!!
TAMU SANA HII!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom