Kuna kipi cha kufanana kati ya Angelina Jolie na Irene Paul?

AVRAM

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
616
882
Pengine nilikua najidanganya, mara zote ninapoangalia picha ya msanii mmoja kati ya hawa wawili, nilijisemea moyoni kwamba kuna kitu wanafanana, sio kwa rangi kiasi lakini kipo wanachoshare kama wasanii wa maagizo.

Kuna kipi cha kufanana kati ya hollywood movie star Angelina Jollie na nyota wa Bongo movie Irene Paul katika maisha yao ya kawaida mtaani, maisha ya kisanii na kazi kwa ujumla, elimu na ujuzi walionao pengine na maisha ya mahusiano na maisha ya familia kwa ujumla.

Jolie nilibahatika kumuona kwenye movie moja inakwenda kwa jina la SALT, na nyengine ambazo niliziona kidogo kidogo bila kuzifuatilia sana ni the tourist, Bosnian war na Unbroken ila huyu ana nyingi sana katika orodha yake; nilimuona namna ya anavyocheza, ni wakiwango cha nyota tano, ni haki yao kwa wanawake wengine kujifananisha nae, ameandikwa sana kwenye magazeti na kuzungumzwa vya kutosha katika TV na Radio sio za Marekani tu lakini kimataifa kwa ujumla pamoja na mazungumzo ya wapenda movie kwenye mitandao.

Irene Paul niliwahi kumuona katika movie moja inaitwa MAJUTO kama sijaisahau maana sio mpenzi wa movie za nyumbani sana kiasi ya kutokumfahamu sama Paul kivile, ila baada ya kutafuta niliona amesha igiza movies kadha ambazo mm binafsi sijawahi kuzitazam, katika orodha yake Paul ameigiza movie ya Mama ntilie, nipe nikupe na nyingi nyenginezo, kwa namna hii utagunduwa kuwa nae pia kibongo bongo ni msanii wa kuigwa na kupigiwa mfano, ni wa nyota tano pia kwa ubora ukilinganisha na wasanii wenzake wa bongo, ana kipaji kizuri na ni msani hodari kwenye kazi yake. Ila kwa kuwa sio walimataifa kivile sikubahatika kusomaachapisho mingi kiasi ya kufahamu maisha yake na kazi zake alizowahi kuzifanya kwa undani. Na hii hasa ndio sababu iloyonifanya niandike uzi huu kupata kumfahamu Irene Paul huku nikimlinganisha na Jollie.

Kwa kipaji alichonacho Paul naamini akiwa na adabu na kujiongeza katika kazi ya uigizaji na yeye pia kuna siku atafika level za Jollie ila sio rahisi kivile, mfano wa wasanii waliojipambanua na kuweka bidii ya kutosha hadi kupata tunzo za maana kimataifa ni ndugu yetu mkenya - mmexican Lupita Nyong'o niliwahi kumuona kwenye tamthilia ikijuilikana kwa jina SHUGA, na kwenye movie ya 12 years a slave na nyengine kadhaa kama vile Black panther, Queen of katwe na the Jungle book, ingawa huwezi kumuweka kiwanja kimoja na Paul lakini kiuwezo katika uigizani yupo mule mule kwa akina Paul, anachomzidi ni dhamira na uthubutu alonao pengine na ufundi na utaalamu alonao kwa kuwa Lupita kazi ya uigizaji ameisomea na sio kipaji kitupu kama tulivyozowea kibongo bongo kijisifia vipaji tulivyonavyo, vipaji ambavyo mara zote hukosa ubunifu wa kiwango kizuri, kasoro hii ukiangalia huchagizwa na ukosefu wa taaluma na ufundi wa fani tunazosema tuna vipaji nazo, hali hii inajitokeza katika kila nyanja ya sanaa hapa petu Tanzania.

Kila la kheir Irene, una nafasi na bahati kubwa ya kufanya uonekane kimataifa, Tanzania wasanii wana kazi kubwa ya kujitangaza kimataifa ila wengi wao huridhika na sifa wanazopewa na wananchi kiulimbukeni limbukeni zaidi.

Tafadhali watanzania tuwambie wasanii wetu kweli ambayo mara zote inauma kwa mtu mpumbavu asietaka kufahamu udhaifu wake. Wasanii kama wema na irene uwoya na wengine ambao sijabahatika kuwaona vyema hawana skills na taaluma ya uigizaji wanabebwa na umaarufu zaidi na kwa kuwa wapenzi wao hawafaham katika viwango vya kimataifa kunatakiwa kitu gani, ndio utakuta zogo kubwa sana wakiwasifia watu wasiostahiki sifa wanazowapa.

Wapo wasanii kama akina yule anaeitwa gabo, angalau anaonesha dhamira wa kuwa wa kimataifa, lakini wengine ni masihara zaidi kulikoni kazi.
 

Attachments

  • IMG_20180712_214320_441.JPG
    IMG_20180712_214320_441.JPG
    25.7 KB · Views: 148
  • IMG_20180712_213906_196.JPG
    IMG_20180712_213906_196.JPG
    26.7 KB · Views: 151
  • IMG_20180712_214242_883.JPG
    IMG_20180712_214242_883.JPG
    23.2 KB · Views: 122
  • IMG_20180712_213731_159.JPG
    IMG_20180712_213731_159.JPG
    26.2 KB · Views: 151
  • IMG_20180712_214033_169.JPG
    IMG_20180712_214033_169.JPG
    25 KB · Views: 122
  • IMG_20180712_213943_344.JPG
    IMG_20180712_213943_344.JPG
    23.1 KB · Views: 115
Nadhani itakuwa ni jinsia zao kuwa sawa tofauti na hapo hakuna chochote kinacholingana. Si haiba, siha, uwezo wa kuigiza ama uwezo wa kipato.
 
wanafanana kitu komoja tu, wote wana K, lakini mfanano mwingine hakuna hata asilimia sifuri, sio kwa muonekano wala ubora wa kazi.
Inawezekana K zikafanana kwa picha ya black and white lakini zikiwa za rangi lazima zitofautiane, ladha ndio usiseme kbs ni ndimu na Asali maana huyu wa mbele ni star wa dunia ilhali huyu wetu ni star wa mtaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom