Kungwi wa Arusha, Irene Mbowe afiwa na mumewe

ZABURI 125:1
WAMTUMAINIO BWANA NI KAMA MLIMA WA SAYUNI HAWATATIKISIKA WAKAA MILELE.

Habarini za Asbh Wapendwa wapenzi wangu. Hamjambo?
Ninaomba nitoe shukrani zangu za dhati kwenu. Naomba niwashukuru sana kwa Namna ya pekee kwa jinsi ambavyo mmekuwa Bega kwa bega pamoja na mimi katika Kipindi cha Msiba ulionipata wa kufiwa na Mume wangu Mpenzi Sabastian Mallya ambaye Alitwaliwa Tarehe 21.1.2020 majira ya Saa nane mchana .Na Tukamzika Tarehe 25.1.2020.
Sina Lugha nzuri ya kuandika zaidi ya Kusema ASANTENI SANA KWA MUDA WENU,PESA ZENU,MAOMBI YENU NA MACHOZI YENU NILIYOYAONA MKILIA PAMOJA NA MIMI.

YANI SIJUI HATA NISEME NINI. ASANTENI KWA SAFARI MLIZOFUNGA,MKAACHA MAMBO YENU ETI MKAJA KUNIFARIJI, MKASAFAFIRI KUTOKA MBALI KWA AJILI YA KUJA KUNIONA. WENGINE MKAJA NA WAUME ZENU,MAMA ZENU WAZAZI,BABA ZENU WAZAZI, WAFANYAKAZI WENZENU, MKABEBA NA WATOTO WANAONYONYA ETI TUU KUNIFARIJI, MKALALA NA MIMI SIKU KADHAAA, MMEACHA ALAMA KUBWA NA NZURI MNOOOO NDANI YA MOYO WANGU SIWEZI KUELEZEA. HAKIKA JEHOVA MUNGU WA BWANA WETU YESU KRISTO ATAWALIPA KWA KADRI YA WEMA MLIONIONYESHA. ASANTENI SANA MNOOO.

BWANA AMETOA,BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
LEO NI SIKU YA 21 TANGU KIPENZI CHANGU AMALIZE SAFARI YAKE HAPA DUNIANI. HAIKUWA RAHISI HATA KIDOGO KULIPOKEA. LAKINI HAIJAWA NGUMU KABISA KULIPOKEA.

KATIKA ULIMWENGU WA ROHO,KATIKA AKIBA YA NENO LA MUNGU AMBALO NIMEKUWA NIKILISOMA NIMEIMARISHWA NA KUONA NGUVU HALISI IKINIINUA IKINISHIKA,IKISEMA NA MIMI KWA NAMNA YA AJABU SANA MNOOOO, UJUMBE WA AJABU ULIONATA MOYONI,AKILINI,MAWAZONI KUTOKA KITABU CHA ISAYA 51:3 .

KATIKA HAYA NINI NINALOWEZA KUKUAMBIA?
NENO LA MUNGU NI AFYA MIFUPANI,AKILINI,MAWAZONI,
NENO LA MUNGU NI CHAKULA

NENO LA MUNGU NI YOTE KATIKA YOTE.
NAJUA UMESOMA HABARI ZA DANIEL NDANI YA TUNDU LA SIMBA.
NAJUA UMESOMA HABARI ZA KINA SHEDIRAKI NDANI YA MOTO.
WOTE HAOO WALIKUWA SALAMAAA KABISA HAIJALISHI WALIKUWA KATIKA NYAKATI NGUMU KIASI GANI.

NIKUAMBIE TU KWAMBA NDANI YA "MSIBA MKUBWA NA MZITO NAMNA HIII NINAOUJASIRI WA KUKUAMBIA NIKO SALAMA."

"Nionapo amani kama shwarii, ama nionaaapo shida, Kwa mambo yoote amenijulisha,Ni salama Rohoni Mwangu......

KAMA ILIVYO DESTURI YA WATANZANIA
TUNAZO MILA NA DESTURI ZETU AMBAZO HAZIMTENDI MUNGU DHAMBI KATIKA KUOMBOLEZA.
NINAMUOMBOLEZEA MPENZI WANGU SABASTIAN MALLYA.
KISHA NIRUDI KATIKA MAJUKUMU
YA MAISHA KAMA KAWAIDA. KWA MAANA YA
FAMILIA ,UCHUMI,UKUNGWI ,HUDUMA .
BARIKIWENI SANAAAAA. MNOOO.
TUZIDI KUOMBEANA.
NI MIMI
IRENE MBOWE AKA "KUNGWI LAO"
KUNGWI PEKEE ANAYEFUNDA,KIIMANI,KIUTAMADUNI NA KITANZANIA.
 
Amepost tena leo.kwa kweli msiba si mchezo.sura yake imeporomoka na amezeeka that.kule kunawiri kote kumeisha. Yani amechakaa ghafla sio mchezo kufiwa na mume.
FB_IMG_15828239076057123.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kungwi amerudi kwa kishindo kupita mumewe alivyokuwa hai. Hata mwaka bado lakini Yuko na speed ya ajabu.
 
Back
Top Bottom