shekalage
Member
- Apr 26, 2013
- 47
- 3
Iran imetekeleza hukumu ya kunyongwa dhidi ya majasusi wawili waliokuwa wakilifanyia ujasusi Shirika la Kijasusi la Marekani CIA na Shirika la Kijasusi la Israel, Mossad.
Majasusi hao wawili walihukumiwa kifo na Mahakama ya Mapinduzi ya mjini Tehran na hukumu yao imetekelezwa alfajiri ya leo Jumapili.
Jasusi aliyejulikana kwa jina la Mohammad Heidari alipatikana na hatia ya kukutana na majasusi wa Israel nje ya Iran kwa mara kadhaa ya kuwauzia taarifa za siri kuhusu Jamhuri ya Kiislamu.
Jasusi mwingine aliyejulikana kwa jina la Kourosh Ahmadi amepatikana na hatia ya kuwa na mawasiliano na majasusi wa CIA na kuwapa taarifa za siri kuhusu Iran.
Mara kwa mara Iran imekuwa ikiwatia mbaroni majasusi wa Marekani na Israel huku baadhi yao wakiwa ni wale waliohusika na vitendo vya kigaidi nchini Iran kama vile kuwaua kidhulma wanasanyi wa masuala ya nyuklia wa Iran.