Iran yafanyia majaribio makombora ya cruise

Iran yafanyia majaribio makombora ya cruise

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
Iran yafanyia majaribio makombora mapya ya cruise

Jeshi la Baharini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanyia majaribio kwa mafanikio makombora yake mapya ya cruise katika luteka ya kijeshi iliyofanyika kaskazini mwa Bahari ya Hindi na katika Bahari ya Oman.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, Jeshi la Majini la Iran limevurumisha makombora ya masafa mafupi na yale ya masafa marefu katika mazoezi hayo ya kijeshi.

Makombora ya masafa marefu ya kizazi kipya yamelenga shabaha kwa mafanikio makubwa hadi umbali wa kilomita 280.

Katika maneva hiyo ya kijeshi ya jana Alkhamisi, makombora ya ardhini hadi baharini na baharini hadi baharini ya Iran ya Kiislamu yamelenga shabaha kwa usahihi mkubwa.

[https://media]Mazoezi ya kijeshi ya Iran

Katika miaka ya hivi karibuni Iran imepata mafanikio makubwa katika sekta ya ulinzi huku ikijitosheleza kwa kiasi kikubwa katika zana za kujihami. Jeshi la Iran hufanya mazoezi ya mara kwa mara kwa ajili ya kuonyesha uwezo wa vikosi vyake na pia kufanyia majaribio zana mpya za kivita.

Jamhuri ya Kiislamu inasisitiza kuwa, uwezo wake wa kijeshi si tishio kwa nchi zingine bali sera yake ya ulinzi imejengeka katika msingi wa kujihami.
 
Hawa jamaa hamtawaweza ndio imeshakua hivyo tena
Wazee wa copy and paste. Vipi ile Manowari toy ya Marekani walioitengeneza washaizamisha?
Screenshot_20200619_163057.jpg
Screenshot_20200619_163006.jpg
20200619_162423.jpg


Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Jitaarisheni wanakuja na Supersonic missiles
Wazee wa copy and paste. Vipi ile Manowari toy ya Marekani walioitengeneza washaizamisha?
For the first time, a military official of #Iran's Navy has announced that Iran plans to produce supersonic cruise missiles. With the production of this type of missile, the combat capability and success rate of the Iran's Navy will be increased significantly in the Persian Gulf.[emoji119]

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Jitaarisheni wanakuja na Supersonic missiles For the first time, a military official of #Iran's Navy has announced that Iran plans to produce supersonic cruise missiles. With the production of this type of missile, the combat capability and success rate of the Iran's Navy will be increased significantly in the Persian Gulf.[emoji119]

Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
Kama zile zilizowalipua wao wenyewe sio?
 
Kuna siku walitengeneza kitoy cha drone na mapicha kibao, wataalam walipokichunguza vizuri ikaonekana wazi huenda ni cha mbao na wala hakikuwa na uwezo wa kupaa.
Nimoja yambinu zakivita hizo japo kama sijakosea zilipigwa marufuku .....
 
Back
Top Bottom