Iran: We are ready to develop and deepen our cooperation with Tanzania in various political and economic fields

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,890
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wa Tanzania, Augustine Mahiga yupo nchini Iran kwa safari rasmi ya kikazi.

Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran amesema Dakta Mahiga anaongoza ujumbe wa ngazi za juu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao utakutana na kufanya mazungumzo na maafisa wakuu wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu masuala ya pamoja na kuimarishwa uhusiano wa pande mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania anatazamiwa kukutana na mwenzake wa Iran, Mohammad Javad Zarif na Rais Hassan Rouhani, pamoja na maafisa wengine wakuu serikalini hapa mjini Tehran.

Iran imekuwa ikisisitiza kuwa, kuimarishwa ushirikiano na uhusiano wa pande mbili katika nyuga za siasa, uchumi na utamaduni na nchi za Afrika ni katika ajenda kuu ya sera ya mambo ya nje ya nchi hii.

Mapema Agosti mwaka huu, Maspika wa Bunge la Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar walikutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran. ambapo walisistiza kuwa, kuimarishwa uhusiano wa makundi ya urafiki ya mabunge na kubadilishana tajiriba kunaweza kusaidia katika kuinua na kustawisha kiwango cha uhusiano wa nchi mbili.

Maspika hao wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walikuwa hapa mjini Tehran kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Dakta Rouhani baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Mei.

Radio tehran
 
Kuna issue ya meli za Iran kutumia bendera ya Tanzania zinaingia na kutoka Iran na sehemu zingine duniani....Iran Ina vikwazo vya UN.....sawa na Korea!!! Safari hii sio bure lazima wakaweke mambo sawa maana soon na sisi tutapigwa vikwazo kushirikiana na Iran na NK.....(ki panki)....napita tuuuu
 
Kuna issue ya meli za Iran kutumia bendera ya Tanzania zinaingia na kutoka Iran na sehemu zingine duniani....Iran Ina vikwazo vya UN.....sawa na Korea!!! Safari hii sio bure lazima wakaweke mambo sawa maana soon na sisi tutapigwa vikwazo kushirikiana na Iran na NK.....(ki panki)....napita tuuuu
Awamu ya Kikwete inaonekana tulikuwa tunashirikiana nao kwa mlango wa nyuma.

Awamu hii tunashirikiana nao wazi wazi.... hivyo hata vikwazo tutapewa wazi wazi tujiandae tu kisaikolojia.
 
kigeu geu tu
Baada ya kuvunja mikataba mingi ya wawekezaji kinyume na sheria (including bombadier,wajapan walokua wanajenga barabara,ACACCIA,Meli ya samaki nk) na kutozwa pesa mingi mnajua wazi kwamba nchi hizo zitakua sio marafiki tena kwenye nyanja za uchumi.

Tukio la kutaka kumuua Lissu nalo litaiathiri sana nchi yetu kutoka kwa mataifa makubwa ku uchumi hususan ya Magharibi (mostly wanaishi kudemokrasia na ndio maana wengi wamelaani tukio la Lissu)

Kwa maelezo haya ni dhahiri kwamba tayari serikali imeshaona itatengwa na wawekezaji wakubwa wa dunia hivyo basi uchumi wetu utadorora vibaya.
Wanacho kifanya ni kutafuta wafariji kama hawa wa Iran ambao kimsingi wameshatengwa.hapa watapata vimisaada vidogo tu ila watambue kwamba wanapoteza muda tu
 
Awamu ya Kikwete inaonekana tulikuwa tunashirikiana nao kwa mlango wa nyuma.

Awamu hii tunashirikiana nao wazi wazi.... hivyo hata vikwazo tutapewa wazi wazi tujiandae tu kisaikolojia.
Kama hakuna vikwazo vya kimataifa tutakavyokiuka sioni shida ya kushirikiana nao...dunia ya sasa hakuna uadui bali ni maslahi tu
 
Mahiga anafanya kazi nzuri sana kumuwakilisha JPM nchi za nje. Hivyo kuwezesha rais asilazimike.kusafiri nje ya nchi na kutumia muda wake zaidi kusimamia shughuli za maendeleo ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom