Vikwazo vya Silaha vyote dhidi ya Iran vinaisha mwezi ujao tujiandae kuiona Iran ikizidi kupaa kijeshi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Vikwazo vya Silaha vyote dhidi ya Iran vinaisha mwezi ujao tujiandae kuiona Iran ikizidi kupaa kijeshi

Waziri wa Ulinzi: Muda wa vikwazo vyote vya silaha dhidi ya Iran utamalizika mwezi ujao wa Oktoba

Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani ametangaza kuwa muda wa vikwazo vyote vya kidhalimu vya silaha ilivyowekewa Jamhuri ya Kiislamu utamalizika mwezi ujao wa Oktoba na kueleza pia utayari wa Iran wa kupanua uhusiano wa kiulinzi na nchi zote zenye misimamo huru.

Katika makala iliyochapishwa na gazeti la Al-Vefagh, Jenerali Ashtiani amebainisha kuwa sera ya ulinzi ya Iran inafuata muelekeo wa "amani, urafiki, uthabiti na usalama" kwa kushirikiana na mataifa yote na kwa ajili ya nchi zote.

Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema, kwa kuzingatia diplomasia amilifu ya ulinzi, wizara ya ulinzi ya Iran, iko tayari kuanzisha na kupanua uhusiano wa kiulinzi na wa kimkakati na nchi zote zenye misimamo huru ..., hususan majirani wa kikanda na mataifa ya Kiislamu kwa msingi wa kulinda usalama kwa pamoja, kuheshimiana na kuimarisha amani na uthabiti.

Jenerali Ashtiani amefafanua: "kwa hivyo, sisi leo tunataka kwa nia ya dhati kupanua diplomasia ya ulinzi wa baina nchi mbili na kimataifa na kushiriki ipasavyo katika mipango ya usalama ya kikanda na kimataifa."

Waziri wa ulinzi wa Iran amedokeza kuwa nchi nyingi zinataka kupanua ushirikiano wa ulinzi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa vile silaha na zana za kijeshi za sekta ya ulinzi ya Iran zimethibitisha ufanisi wake katika medani za vita, hususan katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Mnamo mwezi Juni mwaka huu, shirika la habari la Reuters lilidai kuwa wanadiplomasia wa Ulaya wameiambia Iran kwamba wanapanga kuendeleza vikwazo vya makombora ya balistiki vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Tehran ambavyo vinatarajiwa kumalizika mwezi Oktoba.

Vikwazo vya makombora ya balistiki vya Umoja wa Ulaya vinafikia kikomo tarehe 18 Oktoba chini ya azimio la Umoja wa Mataifa ambalo lilithibitisha mkataba wa nyuklia wa 2015.

Shirika hilo la habari limeashiria vyanzo vinne ambavyo havikutajwa majina yao vikisema kuwa madai kwamba Russia inatumia ndege zisizo na rubani za Iran dhidi ya Ukraine na uwezekano wa kupatiwa nchi hiyo makombora ya balestiki na Jamhuri ya Kiislamu ni miongoni mwa sababu za kurefushwa vikwazo hivyo.

Mkataba wa nyuklia unaojulikana rasmi kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ulisainiwa mwezi Julai 2015 kati ya Iran na nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambazo ni Marekani, Russia, China, Uingereza na Ufaransa pamoja na Ujerumani.

4c3le868626fa22an9p_800C450.jpg
 
Kwanza walioweka vikwazo hawajui vinaisha hiyo October? huko waliko wanaandaa package nyingine ya vikwazo vikiisha tu wanavyo, wa Iran hawatakuwa na nafuu
 
Back
Top Bottom